Chelsea FC (The Blues) | Special Thread

lampard apewe muda

au nasema uongo ndugu zangu?
Mitano tena
 
Chelsea fc under LAMPARD

Werner flop
Ziyech flop
Pulisic flop
Odoi flop
Kante flop
Joginho flop
Azipu flop
Kovacic flop
Keppa flop
Rudger flop
Barkley flop
Abraham flop
Harvetz flop

Basi Lampard apewe pesa ya usajili anunue wachezaji 8 wapya.
Shida sio wachezaji shida ni kocha ndie anawafanya wachezaji waonekane wameflop
Unategemea aje kocha mkubwa tu unategemea tutakuwa tunapoteza point kirahisi rahis

Uwezo wa lampard ni mdogo sana kuifundisha hii timu, yule ingefaa akae kwanza huko alipokuwepo kabla hajaja
Mwangalie mwenzake Gerrard yupo rangers sahiv hawakamatiki kule scotland kwa sababu katulia kule ila lampard alihisi ukiwa na wachezaji wazuri hata bila mbinu atapata mafanikio ni kitu ambacho hakipo

Mbinu za kocha ni muhimu
 
Havertz sidhan kama shida ni kuwa legelege bali ni jinsi lampard anavyomtumia
Havertz sio mchezaj anayepaswa kukaba kwa uchezaj wake, uchezaji wake ni kama wa ozil vile sio wakabaji

Ila ukiangalia lampard anavyomtumia havertz sio kabisa, ukiangalia hata kule leverkusen nyuma ya havertz kulikuwa na 2 dm ambao kazi kubwa ya kukaba walikuwa wanafanya wao havertz yeye alikuwa anapokea mipira kuipeleka sehem sahihi

Wakina oscar walikuwa legelege ila jinsi walivyokuwa wanatumika waliweza kungara

Kingine kinachoonekana baadhi ya wachezaji wanaconsisten ni kucheza mara kwa mara
Thiago,mendy,mount na zouma hawa mechi nyingi wanacheza ni tofauti na wengine mechi hii wamo mechi ijayo hawamo
Soon zouma na yeye ataingia katika huo mkondo labda arudi tena kikosin mechi zinazofata ila kama ndio ile leo upo kesho haupo tutegemee kuona yale makosa yake ya mara kwa mara

Lampard ndie anawafanya wacheza wasiwe na consistency kila mechi lazima kuwe na mabadiliko
 
Wachezaji wenu ni wa LIGI NDOGO.... vimechi kama. Hivi na Luton utasikia HatTrick ya mchezaji wenu KALAVATI MAVUZI sijui Havezi

#COYG
#COYG
 
Mnatakiwa kushinda leo. Maana kuna surprise ya Wolves inawajia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…