X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,620
- 1,796
Nakumbuka miaka michache nyuma nilibahatika kutembelea shule moja ya chekechea au kwa jina maarufu Vidudu, sielewi haswa kwa nini shule hizi za chekechea zinaitwa kwa jina hili la vidudu. Swala hili wacha niwaachie wataalam wa kiswahili.
Kwa taarifa nilizo ambiwa ni kuwa hiyo shule ni katika shule za watoto wenye vipaji maalun. Yaani wanatarajiwa kuwa ni ma' geneus wa kesho.
Baada ya kutembezwa na kuonyeshwa kazi mbali mbali zinazofanyika pale shuleni, nikakaribishwa kwenye darasa moja ambalo wanatarajiwa kuingia darasa la kwanza mwakani.
Nakumbuka niliwauliza maswali machache kulingana na upeo wao, na mmoja wao akaniuliza swali ambalo mimi niliwatupia wao wenyewe kama wanaweza kulijibu na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:
Mwanafunzi_1: Paster Kwanini mwezi unapokaribia asubuhi unatoweka?
Mimi: Kuna yeyote anayeweza kujibu swali hili?
Mwanafunzi_2: (Akanyoosha kidole na kujibu): kwa thababu... kwa thababu eti... etii.. unakwenda kunywa thai na kupumthika....
Darasa zima likapiga makofi....!!