Chekechea

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Nakumbuka miaka michache nyuma nilibahatika kutembelea shule moja ya chekechea au kwa jina maarufu Vidudu, sielewi haswa kwa nini shule hizi za chekechea zinaitwa kwa jina hili la vidudu. Swala hili wacha niwaachie wataalam wa kiswahili.

Kwa taarifa nilizo ambiwa ni kuwa hiyo shule ni katika shule za watoto wenye vipaji maalun. Yaani wanatarajiwa kuwa ni ma' geneus wa kesho.

Baada ya kutembezwa na kuonyeshwa kazi mbali mbali zinazofanyika pale shuleni, nikakaribishwa kwenye darasa moja ambalo wanatarajiwa kuingia darasa la kwanza mwakani.

Nakumbuka niliwauliza maswali machache kulingana na upeo wao, na mmoja wao akaniuliza swali ambalo mimi niliwatupia wao wenyewe kama wanaweza kulijibu na mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwanafunzi_1: Paster Kwanini mwezi unapokaribia asubuhi unatoweka?

Mimi: Kuna yeyote anayeweza kujibu swali hili?

Mwanafunzi_2: (Akanyoosha kidole na kujibu): kwa thababu... kwa thababu eti... etii.. unakwenda kunywa thai na kupumthika....

Darasa zima likapiga makofi....!!
 
Kwa level ya huyu mtoto alikuwa very geneous!!! I.e Kipanga. Kuweza kufikiria chapuchapu na kuona asubuhi tunapata kinywa na mwezi nao, na kuona kwa kuwa hauonekani unakuwa umepumzika!!!

Watoto kwa kawaida wanakumbuka sana vitu ambavyo wanakuwa wamefundishwa na sayansi yao ni body (parts of the body, body cleaninless), animals (domestic animals and wild animals), water (sources of water -simple ones like taps, river, springs, etc), plants (flowers), vegetables and fruits (naming). Sasa wewe ulikuwa unataka aweze kujibu swali kama hilo?? Hawakujua ndiyo maana walikuuliza? Na watoto huwa wanapenda majibu, na si kuwauliza tena swali kama lile lile hawaelewi. Na topic kama hiyo not covered hadi upper Primary tena kwa briefly sana in Geography. Secondary ndipo wanajifunza a bit. Nafurahi hawakusema sijui, they tried!! Ukizingatia mri wao (range 4.5-6 years preparatory class!!!)
 
Kweli huyo mtoto ana akili za ajabu, manake ameweza kufikiria fasta fasta na akapata jibu ambalo kwa logic ya kitoto lina-make sense.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom