Cheka, simulia, lakini usiombe yakukute

Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
706
Points
500
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
706 500
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined
Aug 12, 2011
Messages
5,810
Points
2,000
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined Aug 12, 2011
5,810 2,000
Long time no see Bishop. Mupo? Silioni lile gazeti letu pendwa. Afisi bado iko palepale Migomigo? Nataka nije kumiisalimuni.
Gazeti lipo ila limebadilishwa style, hivi sasa halitolewi kama zamani kibiashara bali ni kama NGO magazine fulani kwa ajili ya uhamasishaji wa mambo fulani fulani. Ofisi ilihama MIgomigo tangu 2007, siku hizi ipo jirani na viwanja vya Leaders Club, inatazamana na Ubalozi wa Kenya. Kwa sasa kampuni imekua sana kwani wana-produce mpaka TV Magazines, documentaries na feature films, pia inamiliki chuo cha sanaa (Gaba Arts Centre)...
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
706
Points
500
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
706 500
Gazeti lipo ila limebadilishwa style, hivi sasa halitolewi kama zamani kibiashara bali ni kama NGO magazine fulani kwa ajili ya uhamasishaji wa mambo fulani fulani. Ofisi ilihama MIgomigo tangu 2007, siku hizi ipo jirani na viwanja vya Leaders Club, inatazamana na Ubalozi wa Kenya. Kwa sasa kampuni imekua sana kwani wana-produce mpaka TV Magazines, documentaries na feature films, pia inamiliki chuo cha sanaa (Gaba Arts Centre)...
Haya ni maendeleo makubwa. Napitaga sana barabarani mitaa hiyo.. Nitawatembelea karibuni panapo majaliwa.
 
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined
Aug 12, 2011
Messages
5,810
Points
2,000
Bishop Hiluka

Bishop Hiluka

Verified Member
Joined Aug 12, 2011
5,810 2,000
Haya ni maendeleo makubwa. Napitaga sana barabarani mitaa hiyo.. Nitawatembelea karibuni panapo majaliwa.
Karibu, japo mimi nilishaondoka huko miaka mingi, ila nina mawasiliano nao ya mara kwa mara...
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
706
Points
500
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
706 500
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 13

Viguu vya Grego vilitetemeka wakati muda wa maakuli ulipojiri. Majeraha yake, iwavyo vyovyote vile, itakuwa yalishakuwa yamepona kabisa. Hakujihisi mapungufu yoyote kuihusu. Hili lilimstaajabisha na kulitafakari, namna zaidi ya mwezi mmoja uliopita alijikata kidogo kidoleni kwa kisu na namna jeraha hilo lilivyokuwa likimuuma yaani mpaka hata juzi.

“Yaelekea hisia zitanipungua,” aliwaza, huku akifyonza jibini kwa pupa, ambayo ilimvutia bila kusita, zaidi ya vyakula vyote vengine.

Harakaharaka na huku macho yake kodo kwa kuridhika, alikula jibini moja baada ya nyingine, ilhali mbogamboga, mchuzi, ugali, hakuviona aslan kuwa na ladha. Hakuweza kustahimili harufu zake na hata ikambidi abebe vile alivyotaka kuvila mbali navyo kidogo.

Kufikia muda dada yake polepole anazungusha ufunguo kama alama ya kumuashiria aondoke, Grego zamani alikuwa ameshamaliza kula na sasa alilala kivivu palepale alipokuwapo. Sauti hiyo ilimchanganya Grego, licha ya ukweli kwamba usingizi ulikuwa karibu umeshampitia, na akaharakia kujificha chini ya kochi.

Lakini alijizuia sana kuweza kubakia mulemule chini ya kochi, japo kwa muda mfupi dada yake alipokuwa chumbani, kwa vile alikuwa sasa ameshiba mlo maridhawa aliokula punde, na nafasi ile finyu ilimbana kiasi cha kuvuta pumzi kwa taabu.

Wakati hali ya kukosa pumzi ikiendelea kumshambulia Grego, alimtazama dada yake macho kodo, wakati dada yake asiye na habari akiendelea kufagia chumbani kwa fagio, siyo tu makombo ya chakula, bali hata vile vyakula vingine ambavyo Grego hakuvigusa kabisa, kana kwamba navyo sasa havikuwa na matumizi, na kisha kutupa kila kitu kwa haraka kwenye ndoo, aliyoifunika kwa mfuniko wa mbao, na kuvipeleka vyote nje ya chumba.

Kabla hata dada hakufika mbali, Grego alikuwa tayari keshajikongoja kutoka chini ya kochi, akajinyoosha, na kuuachia mwili wake ukae vizuri.

ITAENDELEA
 
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined
Oct 31, 2006
Messages
706
Points
500
Mlenge

Mlenge

Verified Member
Joined Oct 31, 2006
706 500
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 14


Ni kwa namna hiyo Grego alijipatia mlo wake kila siku, mara moja asubuhi, wakati wazazi wake na msaidizi wa nyumbani wakiwa bado wamelala, na mara ya pili punde baada ya mlo wa mchana, kwani wazazi wake, kama ilivyokuwa kawaida yao, huwa wameuchapa usingizi wa mchana kwa muda kidogo, na dada wa kazi huwa ametumwa na dada kwenye majukumu yake mbalimbali.

Bila shaka hawakutaka Grego afe njaa, lakini pengine hawakupenda tafrani ya kufahamu ni nini alichokula kwa njia nyingine zaidi ya kupitia maneno ya kusikia.

Pengine dada yake alitaka kuwaepusha na kile ambacho pengine kilikuwa ni kausumbufu tu kadogo, kwani tayari walikuwa wameshateseka sana.

Ni visingizio vipi walivitumia asubuhi ile ya kwanza kuwaondosha daktari na fundi wa kitasa, Grego hakuweza kubaini kwa hakika. Na kwa vile alikuwa haeleweki anachokiongea, hakuwepo yoyote, hata dada yake, aliyewaza kwamba huenda Grego akawa na uwezo wa kuelewa mazungumzo yao.

Hivyo, wakati dada yake akiwa chumbani, Grego ilimbidi atosheke na kusikiliza mara hii au ile, dada yake akigumia na kusali kwa watakatifu wa kale.

Ni pale tu baadae, wakati alipoanza kuzoea kila kitu kiaina (kwa kweli hapawezi kuwepo kwa mazungumzo ya dada kuzoea kabisa hali ile)


Wakati mwingine Grego alibamba neno la kumzungumzia, lililokusudiwa kuwa jema au ambalo linaweza kutafsiriwa hivyo.

“Mh, leo kakiona chakula ni kitamu,” alisema dada yake, kama Grego alifagia sahani ya mlo aliopewa; wakati ambapo, ikiwa ni kinyume chake, ambayo polepole ilizidi kujirudia mara kwa mara, dada alizoea kusema kwa huzuni, “sasa kila kitu kimesita tena.”

Japo Grego hakuweza kupata taarifa mpya moja kwa moja, alisikia mengi kutoka kwenye chumba jirani, kwani pindi asikiapo sauti, aliharakia kwenye mlango husika na kukandamiza mwili wake wote hapo.

Hasa kwa siku za mwanzoni, hapakuwa na maongezi ambayo hayakumhusu kwa namna moja au nyingine, ngaa kwa siri.

Kwa siku mbili wakati wa maakuli yote gumzo lilikuwa ni nini sasa kila mtu awe anafanya; lakini pia walizungumza pia hayohayo kwenye mida baina ya milo, kwani muda wote nyumbani palikuwa na walau watu wawili, kwa vile hakuwepo yoyote ambaye alikubali kubaki nyumbani peke yake na watu hawakuweza kuondoka nyumbani na kuacha nyumba bila mtu kwa sababu yoyote ile.


Na kana kwamba hiyo haitoshi, siku ileile ya kwanza, dada wa kazi (haijulikani ni nini na kwa kiasi gani alikuwa anafahamu yaliyokuwa yanaendelea), akiwa amepiga magoti alimbembeleza mama Grego amwachishe kazi mara moja, na alipokuwa akiaga takriban dakika kumi na tano baadaye, aliwashukuru kwa machozi kwa kumwachisha kazi, kana kwamba alikuwa akipokea hisani kubwa wenyeji waliyomfanyia, na aliapa kwa hofu kuu, pasipo kuambiwa na mtu, kiapo cha kutomsaliti yoyote, hata kwa kiasi kidogo.

Dada yake sasa ilimbidi aunganishe nguvu na mama yake katika masuala ya upishi, japo hilo halikuleta taabu kubwa kwa vile watu ni kama walikuwa hawali kitu.


ITAENDELEA
 

Forum statistics

Threads 1,325,742
Members 509,278
Posts 32,201,600
Top