Cheka, simulia, lakini usiombe yakukute

Umesoma hadithi hii mwanzo hadi mwisho?

  • Ndio

    Votes: 3 50.0%
  • Hapana

    Votes: 3 50.0%

  • Total voters
    6
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 34


Hivyo walikuja na kusimama kuuzunguka mwili wa Grego, mikono yao ikiwa mifukoni mwa makoti yao machovuchovu, kwenye chumba, ambacho tayari kilikuwa na mwanga mwingi.

Kisha mlango wa kutokea chumba kingine ulifunguliwa, na Bwana Samsa alitokea akiwa amevaa yunifomu yake, mkewe akiwa amemshika kwa mkono mmoja, na dada kwa mwingine.

Wote walikuwa na vijialama vya machozi. Mara kwa mara Grete alikandamiza uso wake kwenye mkono wa baba.

“Ondokeni nyumbani kwangu sasa hivi,” alisema Bwana Samsa na kufungua mlango, bila kuacha kuwashika wanawake wale.

“Una maana gani?” alisema yule mpangaji wa kati, kiasi akiwa amechukizwa na akitabasamu kwa ubaya. Wale wengine waliweka mikono nyuma na kuisugua, kama wategemeao kwa furaha pambano kubwa wanalotegemea kuibuka washindi.

“Namaanisha hicho nilichokisema,” alijibu Bwana Samsa na kwenda moja kwa moja, akiwa na wanawake wawili, kwa yule mpangaji.


Huyo kwanza alisimama palepale alipokuwepo bila kujongea na akitazama sakafu, kana kwamba mambo yalikuwa yakijipanga upya kichwani mwake.

“Sawa, haya tunaondoka,” alisema na kumwangalia Bwana Samsa kana kwamba, ghafla akiwa amekumbwa na unyenyekevu, alikuwa akiomba ruksa mpya kwa ajili ya uamuzi huu.

Bwana Samsa yeye aliendelea kuitikia tu kwa kichwa huku macho yamemtoka.

Kufuatia hayo, mpangaji alichukua hatua ndefundefu kuelekea sebuleni. Marafiki zake walikuwa tayari wanasikiliza kwa muda huku mikono yao ikiwa imetulia hivi, na sasa walijongea kumfuata, kana kwamba wakihofia Bwana Samsa anaweza kuwafuata hukohuko sebuleni na kutibua kujiunga kwao upya na kiongozi wao.

Kule sebuleni, wote watatu walichukua kofia zao kutoka cha kutundikia makoti, wakavuta mikongojo yao kutoka kwenye kitunzia mikongojo, wakainama kimyakimya kama watoao hishma, na kuondoka kwenye nyumba.


Katika kilichojidhihirisha kwamba ni wasiwasi usio na msingi, Bwana Samsa alishuka ngazi akiwa na wale wanawake wawili, akaegemea kingo za ngazi, na kuangalia chini kadiri wale wapangaji watatu polepole lakini kwa mpangilio wakizidi kushuka ngazi zile ndefu, na kutokomea kwenye kila mzunguko wa ngazi na sekunde chache kuonekana tena. Kadiri walivyozidi kutokomea, ndivyo na familia ya Samsa ilivyopoteza hamasa ya kuwafuatilia, na alipokuja chinga auzaye nyama na trei lake kichwani alipopanda ngazi, Bwana Samsa, pamoja na wale wanawake waliondoka walipo, na wote wakarejea, kama waliofurahia, mpaka ndani nyumbani.

Waliamua kutumia siku hiyo kupumzika na kwenda matembezi. Siyo tu walistahili mapumziko kwa kazi, lakini hakukuwa na swali kwamba walihitaji hilo sana.

Hivyo walikaa mezani na kuandika barua tatu za udhuru: Bwana Samsa kwa bosi wake, Bibi Samsa kwa mteja wake, na Grete kwa tajiri wake.

Wakati wakiandika, mama wa usafi aliingia kusema anaondoka kwa leo, kwa vile kazi yake ya asubuhi ilikuwa imeisha.

Wale waandikao watatu kwanza waliitikia tu kwa kichwa, bila kuangalia juu. Ni pale tu wakati yule mama wa usafi alipokuwa bado hataki kuondoka, ndipo walipoangalia kwa hasira.

“Nini tena?” aliuliza Bwana Samsa. Mama wa usafi alisimama akitabasamu mlangoni, kama ambaye ana habari kubwa sana nzuri ya kusema lakini atafanya hivyo tu endapo ataulizwa moja kwa moja.

Lile nyoya dogo la mbuni lililokuwa takriban wima kwenye kofia yake, ambalo lilimkera Bwana Samsa muda wote tangia ameanza kazi kwao, lilinesa kidogo huku na kule.

“Haya basi, nini hasa unataka?” aliuliza Bibi Samsa, ambaye mama wa usafi kwa kawaida alimheshimu.

“Sawa,” alijibu mama wa usafi (akitabasamu kwa furaha sana kiasi kwamba hakuweza kuendelea kusema mara ileile), “ni kuhusu lile takataka kwenye chumba kile ambalo linabidi litupwe, msijisumbue nalo. Nimeshalishughulikia.”

Bibi Samsa na Grete waliinamia barua zao, kana kwamba wanataka kuendelea kuziandika; Bwana Samsa, ambaye alibaini kwamba mama wa usafi alitaka kuanza kuelezea kila kitu kwa kirefu, aliwahi kunyoosha mkono na kumzuia.

Lakini kwa vile hakuruhusiwa kutoa maelezo, alikumbuka kwa haraka kwamba bado alikuwa ndani, na akasema, wazi akiwa ameudhika, “Bai bai, kila mmoja”, na kugeuka kwa hasira na kuondoka nyumbani huku akiubamiza mlango vibaya.

“Jioni hii tutamwachisha kazi,” alisema Bwana Samsa, lakini hakupata jibu kutoka kwa mkewe wala kwa bintiye, kwani mama wa usafi yaelekea alikuwa ameshatibua utulivu waliokuwa wameupata punde tu.

Waliinuka, wakaenda dirishani na kubakia hapo, mikono yao imeshikana. Bwana Samsa aligeuka kitini pake kuwaelekea na kuwaangalia akiwa kimya kwa muda.

Kisha akasema, “Haya basi, mje hapa. Acha hatimaye tuondoe vitu vya zamani. Na mnifikirie na mimi kidogo.”

Wale wanawake wakaenda kwake mara moja. Waliharakia kumfikia, wakamshika, na kwa haraka wakahitimisha barua zao.


Kisha wote watatu wakaondoka nyumbani pamoja, kitu ambacho hawakukifanya kwa miezi sasa, na kupanda treni ya mwendokasi kwenda kupata hewa ya nje ya jiji.

Behewa ambamo walikuwa wameketi wenyewe tu lilikuwa limezingwa na jua la motomoto.

Waliongeleshana wenyewe kwa wenyewe, wakiegemea kwa raha kwenye siti zao, kuhusu matarajio ya yajayo, na waligundua kwamba, ukiangalia vizuri, hayo hayakuwa mabaya kabisa, kwani wote watatu walikuwa na ajira, ambazo kuzihusu hawakuulizana kabisa, ipi ambayo ilikuwa ni zuri na yenye matazamio makubwa.

Maboresho makubwa kuliko yote katika hali yao ya sasa, bila shaka, yangekuja kutokana na kubadilisha makaazi. Sasa walitaka kupanga kwenye nyumba ndogo na ya gharama nafuu zaidi, lakini iliyo pazuri na inayoenda na uhalisia kuliko ya sasa, ambayo Grego aliitafuta.

Wakati wakiendelea kuyatafakari haya kwa furaha, ghafla Bwana na Bibi Samsa karibia kwa pamoja walibaini namna binti yao, ambaye alikuwa akizidi kufurahi muda wote, alikuwa hivi karibuni amechanua, licha ya matatizo yote yaliyotukia na kumuacha mashavu yake yakiwa yamepauka, na kuwa binti mrembo na mkubwa apendezaye.


ITAENDELEA
 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 35

Wakizidi kuwa kimya na kama vile wanaoweza kuelewana kwa kuangaliana tu, walidhani kuwa sasa ulikuwa ni wakati muafaka kutafuta mtu aliye mwaminifu na mwadilifu anayeweza kumuoa.

Na ilikuwa ni kama vile uthibitisho wa njozi zao mpya na nia zao njema pale ambapo mwishoni mwa safari yao binti aliinuka na kujinyoosha mwili wake wenye ujana.

MWISHO




Jiandae kusoma hadithi nyingine iitwayo Mfuga Kunguru
 
Pitia na hadithi hii ya KADI

 
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 35

Wakizidi kuwa kimya na kama vile wanaoweza kuelewana kwa kuangaliana tu, walidhani kuwa sasa ulikuwa ni wakati muafaka kutafuta mtu aliye mwaminifu na mwadilifu anayeweza kumuoa.

Na ilikuwa ni kama vile uthibitisho wa njozi zao mpya na nia zao njema pale ambapo mwishoni mwa safari yao binti aliinuka na kujinyoosha mwili wake wenye ujana.

MWISHO




Jiandae kusoma hadithi nyingine iitwayo Mfuga Kunguru

Safi sana...

Chapter Closed...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom