Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
- Thread starter
- #81
Cheka, Simulia, Lakini Usiombe Yakukute - 26
Kwenye kaya hii iliyofanya kazi sana na kuchoka mno nani ambaye alikuwa na muda tena wa kumfikiria Grego isipokuwa tu pale ilipomlazimu?
Kaya ilikuwa ikizidi kuwa ndogo. Yule dada wa kazi aliachwa aende zake. Mama mtu mzima, mwembamba, nywele zake zenye mvi zikinesa huku na kule kichwani pote alikuja asubuhi na jioni kufanya kazi ngumu kuzidi.
Mama alifanya kazi zote nyingine zilizobaki zikiwa ni nyongeza kwa kazi yake muhimu ya ufumaji.
Yaani ilitokea kwamba hata vipande kadhaa vya urembo vyenye thamani, mali ya familia, ambavyo zamani mama na dada walifurahi mno kuvivaa kwenye matukio maalum ya kijamii na sikukuu, viliuzwa, kama ambavyo Grego alibaini jioni kutokana na mazungumzo ya ujumla ya bei zilizopata.
Lakini malalamishi makubwa yalibaki kuwa hawangeweza kuiacha nyumba hii, ambayo ilikuwa ni kubwa kuliko uwezo wao wa kifedha, kwani ilikuwa ni vigumu kufikiria ni namna gani Grego atasafirishwa.
Lakini Grego alitambua fika kwamba haikuwa kumfikiria yeye pekee ndiko kulikozuia wasihame (kwani angeweza kusafirishwa kirahisi ndani ya boksi maalum lenye matundu machache ya kupitisha hewa); kitu kikuu kilichoizuia familia isibadili makaazi zaidi kilikuwa ni kukata tamaa kwao na pia fikra kwamba wamekutwa na masaibu ambayo hakuna yeyote kwenye orodha nzima ya ndugu na jamaa aliyefikwa na kama hayo.
Kile ambacho dunia hukitarajia toka kwa watu masikini ndicho walichokifanya kupindukia. Baba alipeleka kiamsha kinywa kwa watumishi wa benki, mama alijitoa muhanga kwa ajili ya nguo za ndani za watu wengine, dada alikuwa dawatini muda wowote akiwa tayari kuwa msaada kwa wateja, lakini mwamko kwenye familia haukuongezeka hata kidogo.
Na lile jeraha mgongoni mwake lilianza kumsumbua Grego tena na tena, wakati ambapo mama na dada, baada ya kumsindikiza baba kitandani, walirejea, wakatua kazi zao, wakasogeleana, na kukaa pamoja, na pale mama sasa aliposema, akiashiria uelekeo wa chumba cha Grego, “Kafunge mlango, Grete,” na pale ambapo Grego alikuwa tena kizani, wakati jirani wale akinamama machozi yao yaligusana au, kwa macho makavu kabisa, waliishangalia meza.
Grego alitumia muda wake wa usiku na mchana karibu sawa na bila kulala. Mara nyingine alidhani kwamba mlango utakapofunguliwa mara inayofuata atashiriki kwenye mipangilio ya kikaya kama ilivyokuwa zamani.
Kwenye fikra zake walijitokeza tena, baada ya muda mrefu, mwajiri wake na bosi wake na wafanyakazi wanagenzi, yule mhudumu juha kabisa, marafiki zake wawili au watatu wa kampuni zingine, mhudumu wa hoteli fulani mikoani, kumbukumbu maridhawa fupi, keshia wa kike wa kwenye duka la kofia, ambaye Grego alitamtangazia nia kidhati, japo polepole mno – wote walijitokeza wakichanganyika na watu asiowajua au asiowakumbuka, lakini badala ya kumsaidia yeye na familia yake, wote hawakufikika, na alifurahia kuona wakitoweka.
Lakini tena Grego hakuwa na wakati ya kuwazia familia yake. Alikuwa amejaa ghadhabu juu ya huduma mbovu aliyokuwa akipata, japokuwa hakuweza kufikiria chochote ambacho kingempa hamu ya kula.
Hata hivyo, bado alipanga mipango ya namna ipi atajichukulia toka kwenye kabati la chakula kile ambacho kwa vyovyote vile anastahili, hata kama hakuwa na njaa.
ITAENDELEA