Check mtihani wa Hisabati enzi za wakoloni (1946) kwa kanda ya Kaskazini; babu zetu hawakupita kirahisi...

Wanafunzi wa shule za msingi hata na wa sekondari jaribuni kupima number zenu hapa:
View attachment 1015132
Mbona mtihani rahisi sana huo, sasa kama umesoma darasani hilo paper unapiga vizuri sana.Nikikosa sana labda 85% lakini mtihani huo siyo mgumu.Hata saivi baaada ya miaka miiiingi nikifanya roughly sipati chini ya 50%.Hahahahahaaa
 
Lakini waliosoma darasa la mkoloni walikuwa vizuri sana Clerk wa Mkoloni aliongea kingereza sadifu na alijua hesabu vizuri sana na ndio vilikuwa vigezo vya kupata kazi wakati wa mkoloni ulikua upati kazi kama ujawa mbobezi wa kazi husika hata kama ilikuwa kunyosha nguo za Mzungu let alone Mangi.
 
Darasa la nane ni Form one? Kama ni sawa na Form one huo mtihani ni mgumu.Ila Kwa vile walifundishwa Kwa kiwango kinachostahili hayo maswali naamini huo mtihani ni wa kawaida tu,wapo wa kufaulu na wapo wa kufeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo mtihani ningepass with flying colors.

Imagine hakuna instagram, whatsapp, facebook, xbox, playstation, laptop, iphone, ipad n.k. Kilichokuwepo ni radio tu na station ni BBC tu na Radio Tanzania. Inshort hakuna destruction ya namna yeyote unayopata ukiwa masomoni maana hata kupigana miti ilikuwa ni kosa la jinai na huo mda unaupata saa ngapi. Mkitoka shule mnawaza baba na mama tu home.

Kizazi cha sasa ndio kina wakati mgumu sana mashuleni japo mambo yamerahisishwa ila concetrating ni ngumu sana! Kuna mambo mengi sana ya kumvuruga mtoto masomoni.
 
Shule ya kwanza kujengwa Tanganyika ilijengwa na Wakoloni huko Kijiji cha Magila mkoani Tanga wakati shule ya Pili ni Tukuyu Polisi iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Sipati picha shule hizi zingekuwa zimejengwa mkoani Kilimanjaro hali ingekuwaje humu.
Haha tusingekunywa hata maji
 
Siku hizi mtoto anakutana na maswali kama hivi:

Fill in blanks:
1.Rais wa kwanza wa Tanganyika ni Nye_____

2. Moringe Sokoine alikufa kwa ajali ya ga____



Sent using Jamii Forums mobile app

Nadhani siku hizi kwenye mazingira ya Google, Wikipedia na YouTube, watoto wengi hawafanyi effort ya kutosha kuweka concentration kwa yale wanayofundishwa darasani. Nimewahi kukwaruzana sana na wanafunzi wanaposhindwa homework halafu wanalalamika kuwa kuwa wame-search interent na Youtube yote hawakupata majibu, wakati homework yenyewe imetokana na yale niliyofundisha darasani. Miezi michache iliyopita niliwapa wanafunzi mtihani ambao niliutoa mwaka 2002 bila mabadiliko yoyote, darasa zima likafanya vibaya na kulalamika kuwa ni mgumu sana wakati mambo niliyofundisha mwaka 2002 ndiyo hayo hayo niliyokuwa nimefundisha mwaka huu na darasa la 2002 lilikuwa limefanya vizuri. Nimekuwa nafikiri namna mpya ya kufundisha watoto wa siku hizi ili waongeze concentration lakini sijapa majibu mazuri; nitaendelea kuweka effort na nikipata solutiona nitashare na waalimu wote duniani, hasa kwenye nchi zenye internet sana. Internet is both a blessing and a curse kwa upande wa elimu.
 
Back
Top Bottom