Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini yadhamini madhimisho ya Siku ya Hisabati Duniani

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
156
112
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa, akiwa na wanafunzi wa kike waliofanya vizuri katika somo la hisabati muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi za laptop kutoka Barrick.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk. Franklin Rwezimula (kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa kwa niaba ya kampuni.


Mmoja wa wasichana waliofanya vizuri katika somo la hisabati, kutoka sekondari akipongezwa baada ya kupokea zawadi la Laptop kutoka Barrick


Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani Morogoro walishiriki katika maadhimisho hayo


Wanafunzi wakishiriki kujibu maswali ya chemshabongo katika hafla hiyo.
---
Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini, imedhamini madhimisho ya Siku ya Hisabati Duniani ambapo kwa hapa nchini yalifanyika mkoani Morogoro kwa kuandaliwa na Chama cha Hisabati Tanzania ambacho kinashirikiana na Serikali kuongeza ufaulu wa masomo ya hisabati katika shule za msingi na Sekondari nchini.

Kwenye kilele cha maadhimisho hayo , Barrick ilieleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha elimu nchini ikiwemo kufanikisha ufaulu wa masomo ya sayansi na TEHEMA mashuleni ili taifa lisibaki nyuma katika ulimwengu wa sayansi ya teknolojia

Pia imedhamiria kutoa hamasa na motisha kwa watoto wa kike watakaofanya vizuri katika masomo ya sayansi na kutoa wito kwa wasichana kujiamini na kuondoa dhana ya kwamba masomo ya sayansi ni kwa ajili ya wavulana.

Katika hafla hiyo wanafunzi wa kike watatu waliofanya vizuri katika somo la hisabati lililoandaliwa na Chama cha Hisabati nchini mwaka jana walizawadiwa na laptop za kisasa kila mmoja na kampuni ya Barrick .Wanafunzi hao wanatokea katika sekondari za Lumumba-Zanzibar,Canosa na Marian.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk.Franklin Rwezimula, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, alisema Serikali inaendeea kufanya mikakati mbalimbali kuhakikisha ufaulu wa somo la hesabu na masomo mengine ya sayansi unaongezeka na aliwapongeza wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za Serikali katika kufanikisha suala hili.
 
Nafikiri hii inatukumbusha kuwa, hatuna waalimu wenye sifa ya kufundisha somo la Hesabu kwa shule za msingi kwa kama asilimia 90% hivyo tuamke! hata sijui tutafikaje huko kwenye Sayansi & Tech bila Hesabu
 
Back
Top Bottom