Kizazi cha hisabati (mathematics) kinapotea taratibu kutokana na Kubadilishwa kwa Mitaala ya Elimu nchini

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,736
Kila nikimkumbuka mwalimu wangu wa Hisabati Mwalimu Msiagi alivyokuwa akitujengea confidence katika somo la Hisabati zikiwemo test za asubuhi pamoja na kuielewa table na kuiweka kichwani hakika ilitujenga sana.

Lakini Sasa mtaala umebadilisha kuwa mitihani ya hesabu shule ya msingi Wanachagua yaani tayali wamewekewa majibu kabisa.

Mfano 3+4 (a) 2 (b) 4 (c) 7.

Huu mfumo umetengeneza vijana wavivu sana, wanafunzi hawataki kufikiria kabisa pamoja na kukokotoa anachokifanya ni kufumba macho na kuotea tu.

Msingi wa mtoto kupenda hesabu ni kuanzia chini kabisa yaani shule ya msingi ule mfumo wa mwanzo ulikua Bora sana tofauti na mfumo wa Sasa maana umetengeneza kizazi Cha kubashiri (kubeti).

Hivi Sasa ukikagua mitihani ya mtoto haswa ya hesabu unakuta swali Fulani kapata lakini swali Hilo Hilo ukimwambia alifanye kwa njia hawezi hata kidogo kumbe yeye aliotea tu na kwa kuwa ni bingwa wa kuotea basi anaonekana Bora mbele ya wale wasiokuwa Bora katika zoezi la kubashiri.

Mfumo wa Zamani ukikutana na kipanga wa Hisabati anakuwa ni kipanga kweli kweli lakini hivi Sasa kwa shule ya msingi kutokana na huo mfumo wakuchagua naona kabisa kizazi Cha Hisabati kinapotea taratibu kinabaki kizazi Cha kubeti.

Ombi langu kwa Wizara ya Elimu iangalie upya huu mtaala wa shule ya msingi haswa somo la Hisabati wafute huo muundo wa kuchagua ili kunusuru kizazi Cha Hisabati (mathematics)

Nawasilisha hoja.
 
SAHIHISHO:Tanzania hakujawahi kuwa na kizazi Cha mathematics.

hao ni wazee wa kukariri ndo maana hakuna impact ya aina yeyote
Nakubaloana na wewe kabisa. Ukikutana mao huku mitaani na kule maofisini badala ya kuonyesha impact ya mathematics kwenye utendaji, wao wamejaa simulizi za majivuno jinsi walivyokua wanakimbiza
 
Mimi nilipata A mwaka 2010 darasa la 12 so I wish watu wangepambana hesabu za pesa huko shuleni kuliko za darasani.
Safi sana mkuu, mi nilipataga C ,ila nilikua na A za chemistry, Language na Biology

Hio C hapo ndo nimefaulu yaani 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom