Chatu amshinda Mamba nguvu Australia

Chatu amshinda Mamba nguvu Australia

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,087
Reaction score
34,884
140303121731_snake.jpg

Nyoka huyo alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa


Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.

Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.
140303121747_snake2.jpg


Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji


140303121659_snake_3.jpg


Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi


140303121716_snake_4.jpg


Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake


Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.
''Sio kitu unachoweza kuona kila siku,'' alisema Alyce.

chanzo.bbc
 
Duuh.. Mie niliona kwenye documentary channel ya Nat Geo Wild mamba akiliwa na chatu..! Yaani ni scene ambayo inasisimua sana..
 
Huyo Nyoka ni hatari sana, sasa vipi kuhusu ngozi ya Mamba humo tumboni itayeyushwa kweli.!
 
Mamba mbona alikuwa bado kinda huyo,nadhani angekutana na mamba kama wapale mto kagera asingetoka chatu nadhani
 
huyo chatu naye alikuwa na njaa sana,mamba na ligozi lake lile yeye kamla,huyo chatu kwa njaa yake hata ungempa mawe aina ya kokoto angekula tu!
 
Halafu huyo hawezi kuwa chatu..chatu si ana madoadoa..? au specie nyingine ya chatu wa Australia
 
Nakukubali sana mkuu,huwa una habari moto moto
lkn naomba kuuliza,inasemekana mamba huwa na nyongo yenye sumu kali kiasi kwamba akifia sehemu inabidi azikwe mbali,sasa je akiliwa na nyongo yake haina madhara kwa mlaji namaanisha huyo nyoka? au naye atakufa baadaye.
 
Mamba mbona alikuwa bado kinda huyo,nadhani angekutana na mamba kama wapale mto kagera asingetoka chatu nadhani

Mkuu Ingenja, tuko pamoja hapa. Huyo alikuwa mamba mtoto hata kwa muonekano tu. Chezea mamba wewe.

Tiba
 
Sasa hapo itakuwaje maana nyongo ya mamba ni sumu kali sana, hata ukichinja mamba lazima uliport police wake wachukue nyongo.
 
Halafu huyo hawezi kuwa chatu..chatu si ana madoadoa..? au specie nyingine ya chatu wa Australia

Huyo ni jamii ya chatu pia mkuu, chatu wapo wa muonekano tofauti tofauti
 
huyo chatu naye alikuwa na njaa sana,mamba na ligozi lake lile yeye kamla,huyo chatu kwa njaa yake hata ungempa mawe aina ya kokoto angekula tu!

Nyoka huwa ana kawaida ya kumeza halafu digestive juices zinafanya kazi ya kumeng'enya alichomeza...

Umejiuliza tu habari ya ngozi lakini mbona hujauliza habari ya mifupa?
 
inasemekana mamba huwa na nyongo yenye sumu kali kiasi kwamba akifia sehemu inabidi azikwe mbali,sasa je akiliwa na nyongo yake haina madhara kwa mlaji namaanisha huyo nyoka? au naye atakufa baadaye.

Sasa hapo itakuwaje maana nyongo ya mamba ni sumu kali sana, hata ukichinja mamba lazima uliport police wake wachukue nyongo.

Kwa kadiri nijuavyo, nyongo ya mamba sio sumu...

Nilipata kuona documentary moja ikiwaonesha watu wa Zimbabwe huko ambao wao hula mamba...

Walikuwa wakitoa shuhuda kuwa ni mara kadhaa nyama wanazokula hujikuta zimepakazwa nyongo ya mamba...

Isipokuwa kama zilivyo nyongo za wanyama hata hii ya mamba ni chungu na hata nyama iliyomwagikiwa na nyongo huwa chungu pia...
 
Nyoka huwa ana kawaida ya kumeza halafu digestive juices zinafanya kazi ya kumeng'enya alichomeza...

Umejiuliza tu habari ya ngozi lakini mbona hujauliza habari ya mifupa?

mifupa binadamu hata sisi tunayo na anatumezaga!huyu chatu naye njaa kali ilikuwa inamsumbua,nahisi hata angekuwapo chatu mwenzake mdogo angemmeza tu!
 
Alipomaliza kumla mamba akaenda Zake kumbe cku hzi chatu akimeza mnyama huwa anatembea au cku hzi chatu amekuwa anakonda? Sheme on u beliaver

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom