Mamba aliemla mtoto apasuliwa tumbo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Maafisa wa Idara ya Huduma ya Wanyamapori (KWS) siku ya Jana Ijumaa walifanikiwa kumuua mamba aliyemla mtoto wa miaka 11 katika kijiji cha Manyuru, kaunti ndogo ya Ndhiwa Nchini Kenya.

Katika tukio hilo, mtoto huyo, Felix Odongo wa Gredi ya Pili alikuwa anachota maji na wenzake Mto Kuja wakati alipovamiwa na mamba huyo.

Mama mzazi wa mtoto huyo, Janet Auma alisema alikuwa nyumbani wakati mkasa huo ulipotokea.

“Nilitaka ale kwanza kabla kwenda mtoni lakini alisisitiza kwamba lazima amalize kazi za nyumbani kwanza kabla ya kula,” alisema mama huyo ilikuwa siku ya Alhamisi.

Akiwa nyumbani, mama huyo anasema alisikia mayowe mtoni. Mayowe hayo yalikuwa ya watoto wengine waliokuwa wanaita kuomba msaada baada ya mwenzake kukamatwa na mamba huyo.

Alipofika kwenye mto, Bi Auma anasema aliona mamba huyo akiogelea na kutoweka na mwanawe. Alikimbia kando kando ya mto kujaribu kumwokoa mtoto wake. “Nilijawa na mshtuko usioelezeka nilipoona mamba huyo akiyoyomea majini na mwanangu,” alihadithia akiwa na majonzi mengi.

Hapo siku ya Jana Ijumaa, maafisa hao walifanikiwa kumpata mamba huyo baada ya majaribio kadhaa ya kumpiga risasi bila mafanikio awali. Wakazi walifurika kumwona mamba huyo alipotolewa mtoni na huzuni ilijaa zaidi pale alipopasuliwa tumboni mwili wa mtoto huyo ulipotolewa.

Source - CloudsTv
 
Acheni uongo, Mamba sio chatu,
Hawezi kuuumeza mwili mzima wa Mtoto wa miaka 11.
wamekosea tu kuweka lugha walitakiwa wasema vipande vya mwili vilitolewa.
Ila mamba huwa hajui kutafuta kuna uwezekano unakuta mguu mzima kabisa,mikono hata kichwa kama ni kidogo
 
Back
Top Bottom