Chato: Rais Samia kuongoza kumbukizi mwaka mmoja kifo cha Magufuli

hii ni mara 4250 anaenda kanda ya ziwa.
👇🏿
 
Hahahahaha

Taifa letu huenda linaongoza kwa Unafiki Duniani kwa sasa

Namsoma Lemutuz muda huu anamuasa Makonda kutulia kwa kuwa sasa hivi analipia gharama za udhalimu wake wakati enzi zile ilikuwa haipiti siku hajaandika Le commandant Field Mashal sijui kanyaga twende tumechelewa sana na fyoko fyoko zingine kibao…walio madarakani wana cha kujifunza
Lemutuz ni kama malaya wa kona bar yeye lolote kwake lenye ulaji ndio hutembea nalo,alikua chawa kindakindaki wa bashite
 
Sio mbaya kuchangamsha Uchumi

Wakati wa Great depression ya America 1929-1933 moja ya vitu walivyofanya kutoka huko ni kuruhusu vishughuli hivi vya kijinga jinga ki boost mzunguko wa fedha
UONGO
 
Unafiki ni dhambi baya sana, ccm unafiki wenu hata shetani anawashangaa
Hapo zamani: Edward Lowassa ni Fisadi Namba moja

Baada ya Umatemate: Kwa hali hii ya Umaskini wa Nchi hii jawabu pekee ni kumpa kura za Ndio Kamanda Edward Lowassa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Rais Samia Suluhu kuongoza kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Magufuli itakayofanyika kwenye uwanja vya Magufuli uliopo Chato, March 17 mwaka huu.

Naona ndugu kmbwembwe sasa atashiriki mwaka mmoja wa Samia..

========

Geita. Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Geita katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli itakayofanyika Machi 17, 2022 katika Uwanja wa Magufuli uliopo mjini Chato.

Baadhi ya viongozi watakaoshiriki hafla hiyo ni makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Machi 13, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyemule wakati akiwasalimia waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Upendo mjini hapa na kuwataka wajitokeze kushiriki hafla hiyo.

Senyamule amesema Serikali kwa kushirikiana na familia ya hayati Magufuli wamekusudia kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja ikiwa ni njia ya kumkumbuka kiongozi huyo.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es salaam baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Mwananchi
Si iwe public holiday tulale nyumbani tu.
 
Lupaso ilifanyika, ila hakukuwa na utitili wa wanafiki (wanasiasa)

Ilikuwa ni ya kiroho zaidi, ikihusisha familia na ndugu wa Ben, jamii yake, na viongozi wa imani yake Ben (Katoliki)
Familia ya Ben inajitambua na hufanya kumbukumbu kama suala la familia ,ndugu na jamii yake.Hujiepusha na unafiki wa binadamu!
 
Back
Top Bottom