Chato: Rais Samia kuongoza kumbukizi mwaka mmoja kifo cha Magufuli

Maamuzi mabaya yasiyo na tija kwa taifa. Garama ,risk ajali misafara ; mileage magari lukuki ya umma.
Pangefanyika uwakilishi wa wachache, kwa protocol hiyo serikali nzima na mihimili yake inahamia Chato.
 
Rais Samia Suluhu kuongoza kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Magufuli itakayofanyika kwenye uwanja vya Magufuli uliopo Chato, March 17 mwaka huu.

Naona ndugu kmbwembwe sasa atashiriki mwaka mmoja wa Samia..

========

Geita. Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Geita katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli itakayofanyika Machi 17, 2022 katika Uwanja wa Magufuli uliopo mjini Chato.

Baadhi ya viongozi watakaoshiriki hafla hiyo ni makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Machi 13, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyemule wakati akiwasalimia waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Upendo mjini hapa na kuwataka wajitokeze kushiriki hafla hiyo.

Senyamule amesema Serikali kwa kushirikiana na familia ya hayati Magufuli wamekusudia kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja ikiwa ni njia ya kumkumbuka kiongozi huyo.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es salaam baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Mwananchi
Na ile ya kumpongeza yeye vipi maana ilipewa uzito mkubwa kuliko hii iliyompandisha status, au ni ile ya wakatoliki wa Mwanza imesaidia
 
Public funds ni mjumuiko wa vitu vingi kwa kukusaidia tu ni kile unachotoa kila siku (kodi).

Unaponunua salio huko Vodacom na wengineo kuna breakdown ya VAT hiyo nayo ndio inaendesha hizo gari za kifahari kwenda huko chato .

Hizo tozo ndio zinafanya kina Makonda wakawa wanavimba vifua mjini bila hizo serikali haina pesa.

Kuna investments, pesa za vibali, riba za mikopo na kadhalika.

So ni kodi yako ndio inaenda kuteketezwa tu ilhali wangemkubuka bila msafara wa wapiga dili.

Binafsi siwezi kumkumbuka dikteta na matendo yake , uwe na usiku mwema huko ardhi ya nyumbani.
Unaweweseka sana, na bado.
 
Rais Samia Suluhu kuongoza kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Magufuli itakayofanyika kwenye uwanja vya Magufuli uliopo Chato, March 17 mwaka huu.

Naona ndugu kmbwembwe sasa atashiriki mwaka mmoja wa Samia..

========

Geita. Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Geita katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli itakayofanyika Machi 17, 2022 katika Uwanja wa Magufuli uliopo mjini Chato.

Baadhi ya viongozi watakaoshiriki hafla hiyo ni makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Machi 13, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyemule wakati akiwasalimia waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Upendo mjini hapa na kuwataka wajitokeze kushiriki hafla hiyo.

Senyamule amesema Serikali kwa kushirikiana na familia ya hayati Magufuli wamekusudia kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja ikiwa ni njia ya kumkumbuka kiongozi huyo.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es salaam baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Mwananchi
KKT na Magufuli wapi na wapi
 
Back
Top Bottom