Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili Wote Duniani!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,718
Wanabodi,

Angalizo: Naomba kuanza bandiko hili kwa kutoa angalizo muhimu kuwa hapa simzungumzii mtu yeyote specific, bali naendesha somo la psychoanalysis ya hypothetical situation ya hulka za watu wenye tabia za udikiteta katili, kitu kinachoitwa "character assassinations" ndio "modus operandi" ya madikiteta wote katili duniani, na huanza kwa kuwa populist leaders kwa kuonyesha heroic actions hivyo kushangiliwa sana na umati za watu, kama viongozi mashujaa na kupendwa sana na watu!, tena watafanya actions nyingi za utu na huruma ila kiukweli ni machoni tuu ni kama watu lakini mioyoni ni ma sadist.

Sababu za Watu Kuwa Madikiteta ni Deep Rooted Neurosis

Hulka hizo za udikiteta zinatokana na kitu kinachoitwa "deep rooted neurosis" kwa baadhi ya madikiteta hawa kuwa waliteswa sana utotoni!, baadhi yao walikataliwa ndani ya familia zao!, na hii hutokea pale baba anapohisi huenda mtoto huyo sii wa kwake kwa kumhisi mkewe alichepuka!, mama naye kamwe hawezi kukiri kuwa alichepuka hata kama ni kweli alichepuka, (ukweli mwingine ni bora usisemwe kamwe), hivyo baba anakuwa anamtesa sana mtoto huyo, huku mama hawezi kuingilia kwa sababu anaujua ukweli!.

Madikiteta Wengi, Wamekulia Kwenye Mazingira Magumu ya Mateso na Rejection

Mtoto wa aina hiyo anakuwa amekulia katika mateso makubwa ya ukatili, mateso ya kisaokolojia, mateso ya kutumikishwa hadi mateso ya mwili, vitu vyote hivi ukivijumlisha, vinamletea mtoto huyu usongo mkubwa wa mawazo, na kumbukumbu za mateso haya huhifadhiwa kwenye subconscious mind, hivyo unaomtia hasira kusoma kwa bidii na huku ana visasi ili kuonyesha mateso hayo ni jambo la kupita tuu!.

Watoto Wa Mazingira Magumu, Hufanikiwa Sana

Na kweli wengi wa watoto wa aina hii, huja kufanikiwa sana kimaisha, na wakiishafika at the top!, ndipo ile "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya mateso ya utotoni iliyohifadhiwa kwenye "sub conscious mind" inaibuka na kupelekea kumfanya mtu huyo kuwa katili!, sadist, kuongea kwa ukali, kuongea kwa hasira, kutokushaurika, na kutawaliwa na u mimi, mimi ndio kila kitu, etc, na hufikia stage ya ku inflict pain kwa njia za cruelty, torture or character assassinations, anaumiza na akiona mtu anaumia yeye ndio anapata furaha na gratification!,

Sometimes ukatili huu huingia hata katika familia kwa baba au mama kuwa mkali kupindukia, kuchapa sana watoto, na ukatili huu huingia hadi katika mapenzi kwa kumpiga sana mpenzi wake au mke wake, baadhi ya wanaume wanakuwa ni wabakaji, huku wanawake wakipenda kubakwa au kupigwa kwanza kabla ya tendo. Hii ya ukatili kwenye mapenzi inaitwa masochism, wahusika wanaitwa masochistic, au macho men & women.

Madikiteta wa Roma ya Kale Walifanya Nini?

Madikiteta wa Roma ya kale, waliandaa michezo ya kupigana ya ma gladiators mnapigana hadi mmoja afe!. yule gladiators mwenye nguvu kuliko wote, anakuja kuletwa pale kwenye Colosium (stadium) na kusakiziwa simba watatu wenye njaa ya siku 7, huku watu wamejaa kushuhudia jinsi binadamu anavyoraruwa na simba, damu kutapakaa huku watu wanashangilia!.

Batista, Hitler na Musolini Walifanya Nini?

Adolf Hitler yeye alikuwa akinyoosha mistari ya jeshi lake kwa risasi za moto, anayepindisha tuu, anakula hapo hapo!. Idi Amini Dada yeye alikuwa anatumia kikosi kinachoitwa "firing squad", lengo ni kuogofya!.

Dalili ya Kwanza ya Kuelekea Kwenye Udikiteta ni Ku Crush The Opposition

Hivyo wandugu, tusije wote tukawa washangiliaji wa hiki kinachoendelea sasa nchini mwetu kwa utawala wa kuogofya tukitaraji tutafika mwisho mwema na wote watanyooka, kumbe huu ukawa ndio kwanza ni mwanzo tuu wa makubwa yajayo!.

Naomba kumalizia kwa msisitizo, kuna aina mbili za madikiteta!. Kuna Madikiteta Katili na Madikiteta wazuri!. Mada hii inawazungumzia madikiteta katili!, hivyo nawaomba wachangiaji msije kuanza kuchanganya madawa mkaanza kuwadhania watu humu!.

Namalizia kwa swali, jee wote tunaoshagilia hizi character assassination za sasa, ambazo we take them as "the sweet", jee tuko tayari to "to take the bitter with the sweet" ambao huu ni wakati tunashangilia kuwa hivi vidonge vitamu, tunavimeza kwa furaha na raha zetu huku tukishangilia!, jee wakati wa vidonge vichungu ukifika, pia tutavimeza kwa uchungu huku tukilia?, au tutaendelea tuu kuchagua ni vidoge gani tumeze!, vile vidonge vitamu tuu ndio tumeze, lakini vile vidoge vichungu tuteme?!.

Kwa sasa tuendelee kuuchekea huu udikiteta huku tukiushangilia kwa furaha, ila ukifikia wakati wa kulia, naombeni sana tusianze kulalamika, pia tulie kwa furaha maana tulipoanza kuyaona, tulishangilia, yakitukuta ya kutukuta, pia tushangilie!.

Sisi wengine wenzenu ni waona mbali.
Nawatakia Jumatatu Njema.

Paskali
Update
 
Samahani, nilichogundua na kwa mtu yeyote mwenye fikra pevu ni unafiki uliorembwa na kujificha katika uzi wako. Para ya mwisho inai-cancel para ya kwanza na rangi zako zinadhihirika waziwazi. Licha ya kipaji maridhawa cha uandishi sina shaka unatumiwa na kikundi cha watu kama character assasin kwa malipo. Unayemlenga ni dhahiri. Take care, wengi wana uchungu na walikotoka na sasa wanaona mwanga japo kidogo at the end of the tunnel.
 
Maelezo yako yote yamehitimishwa na paragraph ya tano.

Tanzania ilipofika na mazingira yaliyopo hatuwezi kufika huko unakodhani. Huu ni woga ambao ulitegemewa kwa sababu kinachofanywa na Rais kwa sasa kiko nje ya comfort zone za baadhi ya watu.

Ninafahamu ni wachache sana waliamini kama Rais Magufuli anaweza kumtumbua Kitwanga achilia mbali kumtumbua kwa aina kama ile huku Ikulu ikitoa Press Release yenye paragraph mbili ambazo ni fupi. Hii imekuwa ni shock hasa ikichuliwa kuna wengine walisha bet na kusema watavua nguo au watatembea uchi kama Kitwanga atafukuzwa kazi.

Watu wanaomfahamu kwa karibu Rais Magufuli hawashangai kwa kile anachokifanya.

Ninakuhakikishia subiri mahakama ya mafisadi ianze utashangaa watakao kamatwa na kushitakiwa.

Hizi unazoziita character assassination itabidi wazizoee na njia ya kuepuka fanya kazi kama mkataba wako unavyotaka au achana na public sector ili uingie kwenye private sector huku ukifuata sheria za nchi.

Rais Magufuli ni mtu anayechukia sana uonevu na uzembe lakini anaheshimu sana watenda mema kwa jamii hasa ya chini. Kwa sasa kuna watu hali zao kifikra ni mbaya sana kwa sababu hawafahamu hatima yao kutokana na madhambi yao.

Kama kuna watu wanadhani wanaweza kupambana naye ili kumkwamisha ni bora wasahau hilo wazo kwa faida ya freedom zao.

Yes, as human being, Rais Magufuli ana mapungufu yake ambayo ni tone dogo sana kulinganisha na mazuri yake. By the way, hatukuchagua Maraika na hatutegemei awe kama Maraika.
 
uko wazi Sana kuelezea uchungu wako "character assassination ". Lakini huna historia ya assassins . Pia huna historia ya victimized characters.
Nchi yetu haijafikia huko kwenye character assassination . The assassins you refer is neither an assassin but an upright personality in malformed personality. Deviant character ,that is what they are! (Majizi, mafisadi, maongo, malevi, Mazinzi etc )
or
Mafisadi kushika hatamu
What do you call this?
Negative attribute
Hayo ni majipu tu .
Yatumbuliwe ili true character ya yule anaye tumbuliwa ionekane.
 
Nadhani anaelezea udikiteta mzuri
 
Ha haaaaa mkuu Pasco leo una uchungu sana, lakini nakuhakikishia kwa Tanzania hatuwezi kufika huko. Hii inaitwa One Man Show tu, just kuonyesha kuwa mtu mmoja amedhamiria kuwarekebisha watu ambao hawarekebishiki. Sidhani kama katika historia ya nchi yetu iliwahi kutokea kiongozi wa ngazi ya waziri kuingia bungeni amelewa chakari!!! Kwa hiyo mkuu Pasco lazima ukubali kuwa alichofanya poti wako hakikuwa sahihi na ni dharau kwa poti wake. Na poti wake akaamua ku pull the trigger, end of the story
 
Kwa kumtumbua Kitwanga sasa naamini JPM means business.

Tunachokitaka sasa ni

1. Bunge Live
2. Mahakama ya mafisadi
3. Mipango kamambe ya Uchumi
4. Sauti za wananchi kuheshimiwa kwenye chaguzi ( yaliyotokea Zanzibar ni aibu, kamwe yasitokee tena)
 
 

hii ni kweli kabisa. inabidi vyama vinapofanya uteuzi wawe wanachunguza vizuri hadi makuzi ya wagombea tangu utotoni.
 
Kwa kumtumbua Kitwanga sasa naamini JPM means business.

Tunachokitaka sasa ni

1. Bunge Live
2. Mahakama ya mafisadi
3. Mipango kamambe ya Uchumi
4. Sauti za wananchi kuheshimiwa kwenye chaguzi ( yaliyotokea Zanzibar ni aibu, kamwe yasitokee tena)

Yote hayo hayana maana yoyote bila katiba bora inayo akisi maoni ya Wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…