Chanzo cha wivu wa kimapenzi ni nini!?

Chanzo cha wivu wa kimapenzi ni nini!?

Wana MMU, wazima wote!?

Nimeleta swali hilo ili niweze kufahamishwa na wataalamu, hususani wa kisaikolojia.

Kwanini wanadamu sisi, wake kwa waume tunakuwa na wivu mkali unaopelekea hasira zinazoweza kuleta madhara mabaya, hata kutoa roho ya mtu, pale tunapoona wapenzi wetu wakiwa na watu wengine!?

Hata mimi pia, huwa siwi kawaida pale ninapoona mpenzi wangu akichepuka.

Je ni kwanini tunaumia!?

Kwani akichepuka na mtu mwingine, mpenzi huyo atabadirika rangi au atakuwaje!?

Jamani, kwa anayejua sababu ziletazo maumivu hayo, atupatie hapa.

Karibuni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mungu mwenyewe ana wivu..hataki tupende au tuwe na miungu mingine,,,wivu ni nature,,, wivu ni ile kutaka mtu wako awe wako tu akupende wewe tu kama ambavyo Mungu anataka awe yeye tu

Ila sababu za wivu hata me sizifahamu
 
Kudos to you!
Wivu katika asili yake ni hisia hasi ndani ya nafsi ya mtu. Hisia hii hujidhihirisha
pale ambapo mwenye kuwa na wivu anapokuwa mbinafsi kwa maana ya kujihisi yeye bora zaidi au kujidhani anastahili kuliko wengine wanaomzunguka.

Jambo jingine linalochochea wivu ni “kutokujisikia salama”(insecurity) kwa maana ya kuwa na hofu ya kupoteza heshima, umaarufu au maslahi fulani.
 
Kama wewe ni Mkristo, wivu ni dhambi.
Umeambiwa uishi kwa akili na mwanamke, usiishi nae kwa hisia, wivu ni hisia
"Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu"
Kutoka 34:14

Kama Mungu, tu anawivu sembuse mwanadamu?
Wivi nao ni sehemu ya upendo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu anasema yeye ana wivu linapokuja swala la kumfananisha na miungu mingine.
Kwake wivu sio udhaifu ila ni sifa yake ya utambulisho.
Mungu hana wivu wa mapenzi/ husuda mliyonayo nyie wazinzi wa uzao wa nyoka
"Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu"
Kutoka 34:14

Kama Mungu, tu anawivu sembuse mwanadamu?
Wivi nao ni sehemu ya upendo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana MMU, wazima wote!?

Nimeleta swali hilo ili niweze kufahamishwa na wataalamu, hususani wa kisaikolojia.

Kwanini wanadamu sisi, wake kwa waume tunakuwa na wivu mkali unaopelekea hasira zinazoweza kuleta madhara mabaya, hata kutoa roho ya mtu, pale tunapoona wapenzi wetu wakiwa na watu wengine!?

Hata mimi pia, huwa siwi kawaida pale ninapoona mpenzi wangu akichepuka.

Je ni kwanini tunaumia!?

Kwani akichepuka na mtu mwingine, mpenzi huyo atabadirika rangi au atakuwaje!?

Jamani, kwa anayejua sababu ziletazo maumivu hayo, atupatie hapa.

Karibuni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wivu ni hisia chanya(+)/nzuri/hitaji la upekee au utofauti wa Mtu ktk kumiliki vitu, mali, viumbe halisi kama Mke/Mume au livestock(ukulima na ufugaji) na sababu kubwa sana ni kuleta maendeleo bora ktk mazingira anayoishi Mtu kwa kutumia mbinu/maarifa sahihi/halali za utafutaji.

Husuda ni hisia hasi(-)/mbaya/hitaji la upekee au utofauti wa Mtu kumiliki vitu, mali, viumbe halisi kama Mke/Mume au livestock(ukulima na ufugaji) na hujikita ktk matokeo mapovu sana sababu hubeba chembe chembe za chuki, fitina, majungu na hata kusababisha watu kuhitilafiana, kugombana hadi kuuana kwa kutumia mbinu/maarifa yasiyo sahihi/halali za utafutaji.

CHANZO CHA WIVU hutokana na Abeli aliyemtolea Mungu sadaka nyingi ili abarikiwe zaidi kuliko ndugu yake Kaini(BARAKA) lakini CHANZO CHA HUSUDA ni shetani alipotaka kumshinda Mungu kimaendeleo lakini kupitia chuki, fitina na majungu kwa njia zisizo halali(HUSUDA) na hiyo roho chafu ya shetani ilimuambukiza Kaini na inarithi kizazi na kizazi isipokuwa inashindwa kwa Mungu kupitia maombi pekee, sala na kufunga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom