Chanzo cha wivu wa kimapenzi ni nini!?

mpatto

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
748
1,000
Wana MMU, wazima wote!?

Nimeleta swali hilo ili niweze kufahamishwa na wataalamu, hususani wa kisaikolojia.

Kwanini wanadamu sisi, wake kwa waume tunakuwa na wivu mkali unaopelekea hasira zinazoweza kuleta madhara mabaya, hata kutoa roho ya mtu, pale tunapoona wapenzi wetu wakiwa na watu wengine!?

Hata mimi pia, huwa siwi kawaida pale ninapoona mpenzi wangu akichepuka.

Je ni kwanini tunaumia!?

Kwani akichepuka na mtu mwingine, mpenzi huyo atabadirika rangi au atakuwaje!?

Jamani, kwa anayejua sababu ziletazo maumivu hayo, atupatie hapa.

Karibuni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nokia83

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
24,651
2,000
Wivu ndio penzi lenyewe sasa huwezi kumpenda mtu halaf usiwe na wivu...mm najijua nina wivu sana haswa pale napopenda. Wenzangu wenye vimada humu mnawezaje kuvumilia pale unapoona kipenzi chako anamuita baby mtu mwingine?!
 
Kwanini tunaumia sana tunapoona wapenzi wetu wakiwaita watu wengine maneno ya kimahaba kama vile 'baby'!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
55,881
2,000
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
55,881
2,000
Kuhusu ni kuwa na wivu, wivu ni dhambi
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
 
ledada

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
14,438

Hili ni andiko kwenye misahafu!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom