Habari za jioni Great Thinkers.
Huu unaweza kuwa si wakati sahihi kwangu kuandika kuhusu jambo hili, ila kwa sababu ya tafsiri hasi miongoni mwetu sina budi kulizumgumzia.
Uhaba wa wanaume waoaji (Husband Scarcity) ni jambo ambalo limekuwa moja ya changamoto kwa dada zetu siku hizi.
Ukiende kwenye nyumba za ibada nyingi utawakuta wanawake wengi ambao lengo lao si kumcha muumba bali ni kutaka kuombewa ili wapate wenzi wao wa maisha.
Turejee enzi za mababu zetu, je kulikuwa na uhaba wa wanaume waoaji? Kama jibu ni hapana, unadhani kwamba enzi hizo wanaume walikuwa wengi kuliko wanawake au kulikuwa na uwiano sawa kati ya jinsia hizo mbili? Hapana
Nadhani enzi hizo wanawake walikuwa na thamani kubwa sana na walikuwa wameandaliwa kujenga familia zilizo bora nna maisha Mazuri na sio kutafuta familia zilizo na maisha bora ili waende huko.
Enzi za mababu zetu kijana akiwa na uwezo wa kujihudumia na kumhudumia mke, basi alianza kutafuta mwezi wa maisha na mwanamke ambae alimpata, mwanamke huyo ali mu appreciate kijana na kumsaidia kujenga maisha yao ya baadae.
Ninachojaribu kuzungumzia hapa ni kwamba dada zetu ndio wamesababisha hili tatizo la ukosefu wa wanaume waoaji.
Kwanini niseme dada zetu ndio wamejitengenezea hili tatizo?
Leo ukimuuliza mwanamke / Binti kwamba anamtaka mume wa ainagani? Atakuambia anataka mwanaume mbae:
- Awe handsome
- Awe na degree
- Awe mwajiliwa au mjasiliamali
- Awe presentable nam mengine kama hayo (tunayasikia humu kila siku)
- na Ili asionekane worldly anaongezea Awe mcha Mungu.
Utamsikia mwanadada anasema, “siwezi kuteseka kwetu pia nikateseke kwa mwanaume” what a wonderful dream?
Sikatai unaweza kuwa umetoka kwenye life bomba na ukaolewa na mtu amabe yuko vizuri na baadae kwenye ndoa the table turns around na shida zikaanza? Je Utakimbia?
Kwa mfano.- Ukiangalia idadi ya hawa dada zetu na sisi wanaume tunao wazunguka katika maeneo yetu ujumlishe ma vigezo vyao utagundua kuna tatizo na tatizo hili nikwamba vigezo ambavyo wadada wanavitaja utakuta wanaume wengi hawana.
Tuchukulie mfano kati wanawake 50 wanatoa vigezo ambavyo anayvyo mwanaume moja tu, sasa kama huyo mwanaume 1 mwenye vigezo akioa mwanamke moja kati ya 50 unadhani nini kitatoke kwa 49 walio baki?
Nisiseme mengi ila dada zetu naomba niwashaurini. Its beter to start small and end up big than starting big and end up small.
Kiuhalisia ni vigumu kumpata mwanaume ambae amefikisha muda wa kuo na anavigezo vyote unavyovitaka. Wapo wachache sana.
Jamani punguzene vigezo kwa sababu hivyo vigezo vinawafanya muruke mikojo na kikanyaga kinyesi, alafu mwisho wa siku mkiwa disaponted mnakuja na kamsemo kenu kuwa wanaume wote ndivyo walivyo
Njia Rahisi ya kupata mwenza wa maisha ama mume bora ni kubadilisha mtazamo wenu on who a husband is
A husband is not a poverty alleviation program jamani
Angalizo:
Sijawashauri mchukue mwanaume yeyote la hasha, si kila mwanaume ni husband material, jarubuni kuangalia what make him to be who he is na si vitu anavyomiliki ama muonekano wake.
Nawakilisha…
Mapovu Ruksa