Chanzo cha Taifa Stars Kuchukiwa na kuchangia kufanya vibaya

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,745
Kumekuwa na hili swali watu wengi wamekuwa wakiuliza kuhusiana na team yetu ya Taifa. Ambayo imekuwa mara nyingi ikichukiwa na baadhi ya watu.

Kwa nchi nyingine teams zao za Taifa zimekuwa chanzo cha upatanisho kwa wananchi. Yaani inapocheza wanasahau tofauti zao za kisiasa, kiimani, kiitikadi na kuwa kitu kimoja

Tanzania inakuwa kinyume. Siasa imeingizwa mpaka kwenye teams na hata team ya Taifa. Na kuwagawanya wananchi kiasi kumekuwa na chuki ya wazi kwa hii team na watu kuiombea ifungwe. Hili linasababisha hata wachezaji wacheze pasipo morali au uzalendo. Ndani ya team bila shaka wapo wachezaji wenye itikadi tofauti kisiasa. Ilipaswa hii team ibaki ni ya Taifa na si ya chama.

Leo inaanza match yake ya kwanza AFCON. tizama watu watakavyofurahi ikifungwa. Huwezi walaumu. Sababu ikitokea ikashinda anaenda kupewa pongezi mtu au chama jambo ambalo si sahihi.

Michezo itumike kuunganisha watu si kugawanya.
 
Screenshot_20211118-123339_Instagram.jpg
 
shida timu zikifanya ovyo za wananchi ila matokeo yakiwa mazuri wanasiasa wanaingilia na kupitisha siasa zao humohumo, bora tukose wote,,,,,,hawa wakienda mbali yataanza tena maswala sijui ya bao la nani milioni 70,,,,mwanzo hapa wananchi tunapitishiwa hadi namba za kuchangia timu tuipe sapoti ,wakienda mbele inakua timu ya wanasiasa ,bora na sie wananchi tufaidi mie nabet leo tunapigwa naweka buku 50
 
Leo inaanza match yake ya kwanza AFCON. tizama watu watakavyofurahi ikifungwa. Huwezi walaumu. Sababu ikitokea ikashinda anaenda kupewa pongezi mtu au chama jambo ambalo si sahihi.
Hapa ndio umesema ukweli, leo ni siku kubwa kwa Taifa ila hakuna chochote cha maana kinachoashiria ukubwa wa tukio hili.
 
Back
Top Bottom