Chanzo cha ajali ya chopa iliyombeba Filikunjombe

Chanzo cha ajali ya chopa iliyombeba Filikunjombe

wingu la CB (Cumulonimbus clouds) ni hatari kwa ndege ndogo na sio kwa helcopter kwa sababu linaonekana toka mbali ni jeusi na linasimama vertical kama nguzo, hivyo linakwepeka kwa choper!.

Pasco
Hilo wingu(CB) ni hatari kwa hata ndege kubwa ila ndege za kisasa zina vifaa vya kumsaidi rubani ku-detect uwepo wa hilo wingu na hivyo kulikwepa.

Pia,rubani hupewa taarifa ya hali ya hewa(Meater report) kabla ya kuruka na wakati wa kukaribia kutua na hilo wingu kama lipo lazima liwe reported.

Ni "low cloud" hatari kuliko yote katika maswala ya aviation.
 
Mkuu mara nyingi vyombo vya anga huwa havina hitilafu kama za magari. Sio hii tu nishawahi kusoma makala moja ili prove hilo jambo. unaweza usimuelewa lakini endelea kufuatilia. uzembe wa rubani,hali ya hewa,kutunguliwa ama kuhujumiwa.

....kutunguliwa ama kuhujumiwa (?)
 
Engine gani hapa duniani isiyowezapata tatizo la kiufundi?
Hebu acheni kudanganya na kudanganyika!

Hawataki kusema Chopa za ccm alizokodisha J.Makamba sio chakavu. Kumsingizia rubani ambaye ni marehemu kwa sasa na hawezi kujitetea ni uonevu.
 
Nimeisoma hiyo story kwenye gazeti la Mwananchi. Nikajiuliza kwanini hawa wanaojiita wataalamu wanatufanye Watanzania wajinga kiasi hicho? Anasoma eti ndege haiwezi kuanguka kwa ubovu mbali makosa ya rubani. Shenz type na mjinga sana huyo mtalaamu

Sidhani malaamu anaweza ksea maneno haya. Hapa ni tatizo la mwandishi na mhariri wake. Ninavyowafahamu waandishi wa Tanzania huenda amenukuu vibaya. Halafu kwa stori sensitive kama hii gazeti au mwandishi ilibidi wapate sources wengi
 
Nimeisoma hiyo story kwenye gazeti la Mwananchi. Nikajiuliza kwanini hawa wanaojiita wataalamu wanatufanye Watanzania wajinga kiasi hicho? Anasoma eti ndege haiwezi kuanguka kwa ubovu mbali makosa ya rubani. Shenz type na mjinga sana huyo mtalaamu

wataalamu kama hawa wanapata nguvu kwa sababu wanaona jinsi viongozi wanavyo saini mikataba na wanchi wanasema oyeeee
 
Ripoti Inanukia U-KGB fulani hivi. It's too soon to fast kujua. Chopa zina flight data recorder hata haijapatikana jamaa kashatia conclusion. Not FAIR for the families.
 
Huyo anayejiita mtaalamu wa vyombo vya anga ni muongo,mzandiki na mnafiki wa hali ya juu,haiwezekani hata siku moja eti chopa haiwezi kuanguka kwa matatizo ya engine,kuna engine ambayo huwa haipati hitilafu? Huyu ni mshenzi na pumbavu wa hali ya juu,manina zake *¥§>¥&# anatumika na ccm huyu mtaalamu feki,nasema tena ni muongo na mzandiki mkubwa sana tena hafai,kama ni kosa la rubani huyo rubani anakosa gani la kuendesha ndege hadi ianguke? Wamekodi midege mibovu halafu inaua watu anakuja mshenzi mmoja eti ni kosa la rubani na siyo chopa,shenz zake mjinga huyu,kwa kuwa rubani amekufa na hawezi kujitetea ndo analeta huu ujinga hapa? Au anamaanisha ni kosa la rubani kwa kuwa alikubali kurusha chopa chakavu? Nyambafu ccm!

Nimepitia habari nzima ya post namba moja sijaona neno "engine" likitajwa na mleta mada wala kunukuliwa mtaalam.

Wewe umelitoa wapi?

Muongo na mzandik ni wewe.
 
SATURDAY, OCTOBER 17, 2015


ajali.jpg



Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah (Kushoto) na rafiki wa karibu wa marehemu Deo Filikunjombe,Zitto Kabwe wakiwa na huzuni katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam jana wakati wamapokezi ya miili ya marehemu wanne wa ajali ya helikopta iliyotokea juzi mkoani Morogoro katikaMbuga ya Selous. Picha na Venance Nestory



By Boniface Meena, Mwananchi-Dar es Salaam.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa(CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamoKepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali yahelikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa nakosa la kibinadamu la rubani.Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwawalipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watuwote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifarikidunia.

Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam janajioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidizilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi.

Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi chamiaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010,akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze.

Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwakajana ikimuhusisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Makamu wa RaisDk Mohammed Gharib Bilal na kamanda wa Kanda Maalumu ya ya Dar es Salaam, SuleimanKova.

Chopa nyingine ilianguka Februari mwaka jana mkoani Mwanza ikiwa imebeba wanajeshiambao wote walifariki na nyingine ilianguka Kipunguni Novemba, 2014 ikiwa imebebamarubani watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao pia walifariki.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliiona chopa hiyo ikiwa umbali wa kilomita nne nabaadaye wakaona imeshika moto kabla ya kusikia kishindo kikubwa.Sababu za ajali za chopaHakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuelezea chanzo cha ajali iliyochukua maisha yaFilikunjombe na wenzake, lakini Mwananchi iliongea na mtaalamu wa mambo ya ajali zaanga kutaka kujua sababu za ajali za chopa.

"Hakuna chopa inayoanguka kwa sababu ya ubovu wake," anasema mtaalamu wa ajali zandege, John Nyamwiura alipoulizwa na Mwananchi kuhusu chanzo cha ajali za chopa."Mara nyingi ajali hizo husababishwa na makosa ya rubani. Ubora wa chopa haujawahi kuwachanzo cha ajali, chanzo kikubwa ni makosa ya rubani yanayochagizwa na hali ya hewa."

Silaa, baba wa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa, ndiye aliyekuwarubani wa helikopta hiyo iliyoondoka jijini hapa jana jioni kuelekea Ludewa mkoani Iringa.

Hiyo ni ajali ya pili kwa rubani huyo wa kampuni ya General Aviation Services baada yakunusurika katika ajali nyingine ya chopa iliyotokea mkoani Arusha, akiwa amemchukuambunge wa Arumeru Mashariki, Nasari na watu wengine.

Katika ajali ya Arusha, rubani huyo alifanikiwa kuipeleka chopa hiyo hadi juu ya mti ambakoilinasa na hivyo kuokoa maisha ya wote waliokuwa kwenye chombo hicho

Filikunjombe, ambaye alijipatia umaarufu wakati wa sakata la Akaunti ya Escrow mwishonimwa mwaka jana, alikuwa makamu mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alipata umaarufu kutokana na msimamo wake wa kutaka wahusika wote kwenye kashfa hiyoiliyohusisha uchotwaji wa zaidi ya Sh306 bilioni, wachukuliwe hatua, akiwamo Waziri MkuuMizengo Pinda.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitishakutokea kwa ajali hiyo, alisema mapema jana kuwa chopa hiyo iliangukia sehemu ambayo sirahisi kuifikia na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya watu waliotumwa eneo hilo kufika.


Viongozi wamlilia Filikunjombe

Taarifa za kifo chake zilienea kwa kasi kuanzia juzi usiku na baada ya kuthibitika, viongozimbalimbali walianza kutuma salamu za rambirambi wakieleza kuwa Taifa limepoteza mtumuhimu.

"Kwa hakika, nimeshtushwa na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya Filikunjombe naSilaa ambavyo nimetaarifiwa kuwa vimetokea kwa ajali ya helikopta," alisema Dk Magufulikatika taarifa yake.

"Filikunjombe alikuwa mbunge mwenzangu katika Bunge lililomaliza muda wake mwakahuu. Nimefanya kazi naye kwa karibu na kwa miaka mitano ndani ya bunge letu. Tutakosautumishi wake mahiri sana."

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa alisema kifo chaFilikunjombe ni cha kushtua kwa kuwa alikuwa mwanasiasa chipukizi na jasiri.

"Ni pigo jingine kubwa ambalo katika kipindi kifupi Taifa limepata, huku bado likiwa nakidonda cha kuondokewa na wana siasa wengine mahiri, marehemu (Celina) Kombani, Dk(Abdallah) Kigoda na Dk (Emmanuel) Makaidi aliyefariki jana (juzi)."

Msemaji wa kampeni za CCM, January Makamba alisema Filikunjombe ameondokamapema."Tunaambiwa tusihoji matakwa ya Mungu, lakini kuna nyakati inakuwa ngumu. Pole pia kwaNdugu Jerry Silaa kwa kuondokewa na baba mzazi."Zitto Kabwe, ambaye alikuwa mwenyekiti wa PAC pamoja na Filikunjombe alikuwa namasikitiko baada ya mbunge huyo wa Ludewa kufariki dunia."Nimepoteza rafiki. Nimepoteza ndugu. Nimepoteza mtu mtiifu kabisa kuwahi kuwa naye.Sina ya kueleza. Mungu ana mipango yake," alisema Zitto Kabwe.Mgombea ubunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba aliyeandika kwenye ukurasawake wa Twitter akisema: "Ni masikitiko, ni pigo, ni pengo lisiloweza kuzibika.

DeoFilikunjombe ametutoka, Taifa linahuzunika."Filikunjombe anakuwa mgombea ubunge wa sita kupoteza maisha tangu kampeni zianzeAgosti 22. Mgombea wa Jimbo la Lushoto kwa tiketi ya Chadema, Fredy Mtoi alikuwa wakwanza kupoteza maisha baada ya kampeni kuanza.Baadaye Kombani, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi waUmma), alifariki akiwa nchini India ambako alikuwa akitibiwa. Alikuwa anatetea ubunge waJimbo la Ulanga Mashariki.

Kifo chake kilifuatiwa na mgombea wa Jimbo la Arusha Mjini, Estomih Mallah aliyefarikiakiwa KCMC mkoani Kilimanjaro alikokuwa akitibiwa shinikizo la damu, na kufuatiwa nakifo cha Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda ambaye alikuwa mgombea waJimbo la Handeni.

Dk Makaidi alikuwa akigombea ubunge Jimbo la Masasi.HabariPia mwanasiasa maarufu nchini, Mchungaji Christopher Mtikila alifariki kwa ajali ya gari wiki mbili zilizopita.

Miili yawasili, imeharibika vibaya Mwili wa Filikunjombe na wenzake iliwasili jana saa 10:30 jioni kwenye Uwanja wa Ndegewa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na viongozi mbalimbali, akiwamo Spika AnneMakinda, Kashililah na baadhi ya wabunge.Baada ya kupokewa, askari waliipakia miili kwenye magari matatu tofauti na msafara wamagari 15 ulielekea Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, ambako ilihifadhiwa kusubiri taratibu nyingine.

Zitto, ambaye ni msemaji wa familia, alisema kwa kuwa miili hiyo imeharibika sana na hivyotaratibu za mazishi hazitachukua muda mrefu."Itachukua siku moja au mbili, kwa sasa madaktari wanaifanyia uchunguzi kuitambua,"alisema.

Habari za ziada na Fidelis Butahe
 
Mkuu mara nyingi vyombo vya anga huwa havina hitilafu kama za magari. Sio hii tu nishawahi kusoma makala moja ili prove hilo jambo. unaweza usimuelewa lakini endelea kufuatilia. uzembe wa rubani,hali ya hewa,kutunguliwa ama kuhujumiwa.

National Geographic channel huwa wanaonyesha ndege zinavyoanguka kwa matatizo ya vyombo vyenyewe,sijui hapa muongo ni nani,nachanganyikiwa
 
Tusubiri ripoti itatoka tutajua ukweli. Sijakubali kama huyo meandishi alimuhoji mtaalamu. Angemuhoji jibu lingekuwa tusubiri uchunguzi period wamefunzwa hivyo.

Nafikiri mwandishi yuko kibiashara zaidi. Maana angesema/ angeandika headline ya dizain hii, gazeti lisingeuzika kwa sana.
 
Mara nyingi watanzania tunakwama pale tunaposhindwa kutenganisha siasa na utaalamu.
 
Huyo mtaalamu ametoa majibu ya kisiasa. Kwanza kwa uelewa WA kawaida huwezi kuconclude sababu za ajali ya ndege kabla uchunguzi wa kina haujafanyika. Ngoja wataalamu waende eneo la ajali wachunguze na wataleta detailed report ya ajali ambayo itaonyesha chanzo cha ajali.

Huyo John ndio kiongozi wa mambo ya uchunguzi wa ajali za anga. ...
Ameshaconclude ni pilot error. .....
 
Ripoti Inanukia U-KGB fulani hivi. It's too soon to fast kujua. Chopa zina flight data recorder hata haijapatikana jamaa kashatia conclusion. Not FAIR for the families.

Kabisa Mkuu. ....

Ngoja tuone kama ni kweli kasema hivyo, na sio manjonjo ya mwandishi. ...
 
Huyo anayejiita mtaalamu wa vyombo vya anga ni muongo,mzandiki na mnafiki wa hali ya juu,haiwezekani hata siku moja eti chopa haiwezi kuanguka kwa matatizo ya engine,kuna engine ambayo huwa haipati hitilafu? Huyu ni mshenzi na pumbavu wa hali ya juu,manina zake *¥§>¥&# anatumika na ccm huyu mtaalamu feki,nasema tena ni muongo na mzandiki mkubwa sana tena hafai,kama ni kosa la rubani huyo rubani anakosa gani la kuendesha ndege hadi ianguke? Wamekodi midege mibovu halafu inaua watu anakuja mshenzi mmoja eti ni kosa la rubani na siyo chopa,shenz zake mjinga huyu,kwa kuwa rubani amekufa na hawezi kujitetea ndo analeta huu ujinga hapa? Au anamaanisha ni kosa la rubani kwa kuwa alikubali kurusha chopa chakavu? Nyambafu ccm!

tatizo lenu wabongo mtu akijibu kitu na kufafanua kitaalam mnaanza kumuona Kama hajui anachokieleza huyu ni Mtaalam wa anga wamemuuliza na amewajibu kitaalam....tatizo lenu watu Kama wewe ulitaka ujibiwee kwa msisimko was hisia za moyo wako ndio uliziki ata Kama umedanganywa wee utaona nikwl kwasababu moyo wako ulitaka hujibiwe vile unavyotaka we we....au ulitaka akudanganyeee io chopa ilitupiwa kombora kea akiri yako ili ulidhishe nafsi ya moyo wako eeeh.....na kwa taarifa yako Kama ulikua hujui vyombo vya anga kadri vinavyozidi Ku exist kwa root zake angani ndivyo vinavyozid kua imara maradufuu
 
STUPIDITY REASONS,
helicopter zote 5 kila moja imeonyesha tatizo LA aina yake!
INAMAANA ZOTE NI HUMAN MISTAKE?????
 
Mkuu mara nyingi vyombo vya anga huwa havina hitilafu kama za magari. Sio hii tu nishawahi kusoma makala moja ili prove hilo jambo. unaweza usimuele
wa lakini endelea kufuatilia. uzembe wa rubani,hali ya hewa,kutunguliwa ama kuhujumiwa.

Usitudanganye bhana na wewe, anything made by human hand can never lack mapungufu.. sisi wenyewe tumeumbwa na mungu bt mapungufu kibao itakua mabati haya?? acheni hizo bhana!! wewe sema ndege zimetengenezwa kwa technolojia ya hali ya juu in such a way kwamba hazpat hitilafu za ovyo ovyo bt hitilafu ziko pale pale dats y hata ya malaysia ilipotea!! u guys, achen bhana
 
Back
Top Bottom