Chanzo cha ajali ya chopa iliyombeba Filikunjombe

tatizo lenu wabongo mtu akijibu kitu na kufafanua kitaalam mnaanza kumuona Kama hajui anachokieleza huyu ni Mtaalam wa anga wamemuuliza na amewajibu kitaalam....tatizo lenu watu Kama wewe ulitaka ujibiwee kwa msisimko was hisia za moyo wako ndio uliziki ata Kama umedanganywa wee utaona nikwl kwasababu moyo wako ulitaka hujibiwe vile unavyotaka we we....au ulitaka akudanganyeee io chopa ilitupiwa kombora kea akiri yako ili ulidhishe nafsi ya moyo wako eeeh.....na kwa taarifa yako Kama ulikua hujui vyombo vya anga kadri vinavyozidi Ku exist kwa root zake angani ndivyo vinavyozid kua imara maradufuu

akiri-akili
ulidhishe-uridhishe.
hata ulichochangia pia ni zero kama kiswahl chako!! huyo c mtaalam ni fisi tu..hata ww una mapungufu itakua chopa??? jiongezeni nyie
 
ona sasa vileee ubongo wako unavyofikiria pafupi umekosa hoja unaishia kucopy herufi ambazo ataa hazina manaaa toaaa hojaaaaa weweeeeee......acha mambo ya kidada
 
Mkuu mara nyingi vyombo vya anga huwa havina hitilafu kama za magari. Sio hii tu nishawahi kusoma makala moja ili prove hilo jambo. unaweza usimuelewa lakini endelea kufuatilia. uzembe wa rubani,hali ya hewa,kutunguliwa ama kuhujumiwa.
Huko sahihi mkuu,hali ya hewa ndio uchangia kwa kiasi kikubwa hajali za chopa,kingine ni uzembe wa rubani kutokana na poor judgment, mwisho hujuma zifuatazo:mixing fuel na kitu kingine,kutoa safety pin inayo zuhia nut inayo funga rotor ya nyuma hivyo kufanya nut ifunguguke taratibu kutokana na mzunguko wa rotor mwishowe nut ufunguka kabisa na kufanya rotor kudondoka,hilo likitokea rubani atashindwa ku-control chopa,lingine ni explosives,la mwisho kuingiza carbon monoxide kwenye cabin kutoka kwenye exhaust manifold kwa kutumia paipu ndogo kwa bahati mbaya gesi hiyo hatari haina harufu hivyo si rahisi kugundulika kabla haija sababisha vifo -nayasema haya kwa nia nzuri ili wahusika wa usalama wacheck machopa haya kabla ya kuruhusu watu mashuhuri kuyapanda.

Nimalizie kwa kusema chopa nyingi za siku hizi zinatumia gasturbine engines ambazo zina less moving parts, kwa hiyo si rahisi engine hizo kukorofisha kirahisi.
 
Kwa kifupi ni kwamba, kutokana na tafiti za ajali mbalimbali za chopa inaonyesha kuwa 26% ya ajali za chopa zinatokana na makosa ya rubani (mishandling conntrol na loss of control). Ajali zinazosababishwa na matatizo ya engine ni 5% tu ya ajali za chopa. Kwahyo kitaalamu ni kuwa ajali nyingi zinasababishwa na matatizo ya kirubani na ajali chache tu zinasababishwa na matatizo ya engine. Mtaalamu aliyeongea na gazeti la Mwananchi aliongea generally sio specific kwa ajali ya Deo Filikunjombe kwa sababu kuweza kusemea ajali hii ni hadi hapo uchunguzi kamili ukamilike.
Hebu tupeane elimu zaidi ya hivi vyombo.

Hivi hizo chopa hazina aina ya kifaa kinachofanana na black box za kwenye ndege ambazo huwa zinarecord mwenendo mzima wa chombo hicho kabla ya tukio la ajali na hivyo kuweza kujua kama chombo hicho kilianguka kutokana na matatizo ya kiufundi ya chombo chenyewe au matatizo ya kibinadamu ya rubani mwenyewe?
 
Sidhani malaamu anaweza ksea maneno haya. Hapa ni tatizo la mwandishi na mhariri wake. Ninavyowafahamu waandishi wa Tanzania huenda amenukuu vibaya. Halafu kwa stori sensitive kama hii gazeti au mwandishi ilibidi wapate sources wengi

Ndio tatizo la waandishi wetu bro,, ndio maana dr slaa aliwaasa wawe wanafanya research.
 
Huko sahihi mkuu,hali ya hewa ndio uchangia kwa kiasi kikubwa hajali za chopa,kingine ni uzembe wa rubani kutokana na poor judgment, mwisho hujuma zifuatazo:mixing fuel na kitu kingine,kutoa safety pin inayo zuhia nut inayo funga rotor ya nyuma hivyo kufanya nut ifunguguke taratibu kutokana na mzunguko wa rotor mwishowe nut ufunguka kabisa na kufanya rotor kudondoka,hilo likitokea rubani atashindwa ku-control chopa,lingine ni explosives,la mwisho kuingiza carbon monoxide kwenye cabin kutoka kwenye exhaust manifold kwa kutumia paipu ndogo kwa bahati mbaya gesi hiyo hatari haina harufu hivyo si rahisi kugundulika kabla haija sababisha vifo -nayasema haya kwa nia nzuri ili wahusika wa usalama wacheck machopa haya kabla ya kuruhusu watu mashuhuri kuyapanda.

Nimalizie kwa kusema chopa nyingi za siku hizi zinatumia gasturbine engines ambazo zina less moving parts, kwa hiyo si rahisi engine hizo kukorofisha kirahisi.

Nafikiri ulivyovizungumzia viko ndani ya uwezo wa rubani kabla ya ndege kuruka,,, bila shaka huwa kuna log book za kujaza kabla ya kuruka ambazo humguide kabla ya kuruka afanye nini??
 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwa walipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifariki dunia.

Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam jana jioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi.

Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze.

Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal na kamanda wa Kanda Maalumu ya ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Chopa nyingine ilianguka Februari mwaka jana mkoani Mwanza ikiwa imebeba wanajeshi ambao wote walifariki na nyingine ilianguka Kipunguni Novemba, 2014 ikiwa imebeba marubani watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao pia walifariki.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliiona chopa hiyo ikiwa umbali wa kilomita nne na baadaye wakaona imeshika moto kabla ya kusikia kishindo kikubwa.

-
Sababu za ajali za chopa

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuelezea chanzo cha ajali iliyochukua maisha ya Filikunjombe na wenzake, lakini Mwananchi iliongea na mtaalamu wa mambo ya ajali za anga kutaka kujua sababu za ajali za chopa.

“Hakuna chopa inayoanguka kwa sababu ya ubovu wake,” anasema mtaalamu wa ajali za ndege, John Nyamwiura alipoulizwa na Mwananchi kuhusu chanzo cha ajali za chopa.

“Mara nyingi ajali hizo husababishwa na makosa ya rubani. Ubora wa chopa haujawahi kuwa chanzo cha ajali, chanzo kikubwa ni makosa ya rubani yanayochagizwa na hali ya hewa.”

Silaa, baba wa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa, ndiye aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo iliyoondoka jijini hapa jana jioni kuelekea Ludewa mkoani Iringa.

Hiyo ni ajali ya pili kwa rubani huyo wa kampuni ya General Aviation Services baada ya kunusurika katika ajali nyingine ya chopa iliyotokea mkoani Arusha, akiwa amemchukua mbunge wa Arumeru Mashariki, Nasari na watu wengine.

Katika ajali ya Arusha, rubani huyo alifanikiwa kuipeleka chopa hiyo hadi juu ya mti ambako ilinasa na hivyo kuokoa maisha ya wote waliokuwa kwenye chombo hicho.

Filikunjombe, ambaye alijipatia umaarufu wakati wa sakata la Akaunti ya Escrow mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa makamu mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alipata umaarufu kutokana na msimamo wake wa kutaka wahusika wote kwenye kashfa hiyo iliyohusisha uchotwaji wa zaidi ya Sh306 bilioni, wachukuliwe hatua, akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo, alisema mapema jana kuwa chopa hiyo iliangukia sehemu ambayo si rahisi kuifikia na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya watu waliotumwa eneo hilo kufika.

Chanzo: Mwananchi

Huyo mtaalam pumbaf kabisa
 
EL akisema vipaumbele vyake ni ELIMU, ELIMU, na ELIMU; watu wengine wanaponda. Sasa sikia huyo mtaalamu wa kitanzania anavyo-analyze juu ya ajali hiyo...utashangaa na kuingiwa hasira. Hasira hizi ni bora kuzihamishia kwenye sanduku la kura Oktoba 25.
 
tatizo la watanzania ni kua kila mtu kashakua mwanasiasa . na siasa zimengizwa katika kila kitu hata katika mambo ya kitaalam kama haya, mtu ana gugo huko anakuja bishana na conclusion ya mtaalam mwandamizi kwenye hiyo fani, ukifuatilia historia ya huyo anayempiga mtaalam unakuta hakuwahi hata kupata c ya physics au math katika maisha yake. mtaalam kashasema kosa ni la rubani na nakumbuka kusoma mahali kua hii ni ajali ya pili kwa rubani ukianza na ile ya kuanguka kwa chopa la nasari. sasa wewe unabisha kama nani na kwa vigezo vipi vya kitaalam.
 
Msibishe marubani wanajuana!
Sio ajali ya kwanza kwa huyo rubani
 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwa walipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifariki dunia.

Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam jana jioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi.

Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze.

Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal na kamanda wa Kanda Maalumu ya ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Chopa nyingine ilianguka Februari mwaka jana mkoani Mwanza ikiwa imebeba wanajeshi ambao wote walifariki na nyingine ilianguka Kipunguni Novemba, 2014 ikiwa imebeba marubani watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao pia walifariki.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliiona chopa hiyo ikiwa umbali wa kilomita nne na baadaye wakaona imeshika moto kabla ya kusikia kishindo kikubwa.

-
Sababu za ajali za chopa

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuelezea chanzo cha ajali iliyochukua maisha ya Filikunjombe na wenzake, lakini Mwananchi iliongea na mtaalamu wa mambo ya ajali za anga kutaka kujua sababu za ajali za chopa.

“Hakuna chopa inayoanguka kwa sababu ya ubovu wake,” anasema mtaalamu wa ajali za ndege, John Nyamwiura alipoulizwa na Mwananchi kuhusu chanzo cha ajali za chopa.

“Mara nyingi ajali hizo husababishwa na makosa ya rubani. Ubora wa chopa haujawahi kuwa chanzo cha ajali, chanzo kikubwa ni makosa ya rubani yanayochagizwa na hali ya hewa.”

Silaa, baba wa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa, ndiye aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo iliyoondoka jijini hapa jana jioni kuelekea Ludewa mkoani Iringa.

Hiyo ni ajali ya pili kwa rubani huyo wa kampuni ya General Aviation Services baada ya kunusurika katika ajali nyingine ya chopa iliyotokea mkoani Arusha, akiwa amemchukua mbunge wa Arumeru Mashariki, Nasari na watu wengine.

Katika ajali ya Arusha, rubani huyo alifanikiwa kuipeleka chopa hiyo hadi juu ya mti ambako ilinasa na hivyo kuokoa maisha ya wote waliokuwa kwenye chombo hicho.

Filikunjombe, ambaye alijipatia umaarufu wakati wa sakata la Akaunti ya Escrow mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa makamu mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alipata umaarufu kutokana na msimamo wake wa kutaka wahusika wote kwenye kashfa hiyo iliyohusisha uchotwaji wa zaidi ya Sh306 bilioni, wachukuliwe hatua, akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo, alisema mapema jana kuwa chopa hiyo iliangukia sehemu ambayo si rahisi kuifikia na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya watu waliotumwa eneo hilo kufika.

Chanzo: Mwananchi

Naona jimbo la ludewa linachukuliwa na upinzani
 
Huyo mtaalamu hana jina.? Ndo maana waandishi wa Mwananchi mwachukua vichapo. Na mpigwe tu.
 
Wakuu kifo cha
Deo kimeniuma. Lakini nimekerwa zaidi na Nyamwiura kama mtaalamu kusema uongo juu ya chanzo cha ajali. Anaweza kushitakiwa kwwa jambo hilo. Ripoti ya wataalam ndo itatoa ukweli.
Rubani ni operator wako wataalam wengi wanaohusika na matengenezo ya chopa, watu ea hali ya hewa, hujuma nk.
Tusubiri
 
Wakuu.
Bila uchunguzi siyo sawa kuongelea chanzo cha ajali. Mtaalam feki huyo.
New Engine
 
STUPIDITY REASONS,
helicopter zote 5 kila moja imeonyesha tatizo LA aina yake!
INAMAANA ZOTE NI HUMAN MISTAKE?????
You can as well posit otherwise provided you are knowledgeable enough. . . . . Go through what John Kachembeho has provided the forum with. . . .
 
Last edited by a moderator:
marehemu hana haki. hili bandiko kama kuna mtu anataka kumbebesha marehemu rubani zigo.

marehemu mh na umaarufu wake kisiasa ulipaa sana kama wa marehemu kanumba kwa bongo movi.

nini lilikuwa lengo la marehemu mh la muda mrefu kisiasa?
 
Kama inadaiwa chopa ilikua mbovu na ikaruhusiwa kuruka aliyeruhusu kuruka ahojiwe, lkn ni nani aliyekagua au kuna ushahidi gani manake tusiwe tunajisemea mambo yasiyokua na ushahidi kwakua kwanza taarifa yenyewe ya uchunguzi bado haijatoka naamini hayo ni maoni ya jumla tu ya mtaalam. Tuwe na subira kwenye hili.
 
Back
Top Bottom