#COVID19 Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Kuna "misconceptions" nyingi kuhusu chanjo ya Covid19. Baadhi za kitabibu na nyingine za elimu ya tabia. Zile za kitabibu nawaachia madaktari na wataalamu wa afya wazijibie. Mimi najibu hizi ambazo ni Socio-Cultural infuenced.

1. Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?
JIBU:
Wazungu wangetaka kutuua wana njia nyingi za kutumia. 90% ya madawa na vifaa tiba tunavyotumia vimetoka nje. Kuanzia MRI na CT scan ya Muhimbili, hadi dawa ya panadol pale zahanati ya Nanjilinji vimetoka kwa mabeberu. Kwanini wasitumie njia hizo ambazo ni rahisi zaidi kutumaliza badala ya chanjo ya Corona?

Hata hivyo kuna chanjo nyingi sana tunazitumia kutoka kwa hao tunaowaita mabeberu. Mtoto akizaliwa hadi anapofikisha umri wa miaka mitano anachomwa jumla ya chanjo 13 za aina tofauti. Na hakuna hata moja tunayotengeneza sisi. Zote tunapewa msaada na mabeberu. Je wangekua na nia ya kutumaliza si wangesubiri chanjo ya Corona?

2. Kwanini chanjo ya Corona inatolewa bure?
JIBU:
Ni chanjo ipi inatolewa hapa nchini kwa kulipiwa? Mbona hujahoji kwanini chanjo ya pepopunda, polio, tetekuwanga, homa ya ini zinatolewa bure, badala yake unahoji chanjo ya Corona tu? Halafu pia kwanini hauulizi mbona ARVs zinatolewa bure?

Je ungetakiwa kulipia ungeweza? Au serikali yako ingeweza kukununulia? Kwa mfano dozi ya mwezi ya ARVs ni kati ya $170 hadi $220 yani kati ya shilingi laki 4 hadi laki 5. Kwahiyo kama umeathirika na VVU kila unapoenda CTC kuchukua dawa kuna "mabeberu" wamekulipia laki 4 kila mwezi. Je serikali ya Tanzania ingeambiwa ikulipie ingeweza? Same applies to Corona vaccine.

3. Kwanini tusitengeneze chanjo yetu?
JIBU:
Hata mimi natamani hivyo, lakini hatuwezi kwa sababu zilezile za History ya Form 2B. Poor technology, lack of capital, poor government support etc. Kama toothpick na toilet papers tunaagiza China, je tunaweza kutengeneza chanjo ya Corona?

Serikali haijawa na nia ya dhati ya kufanya uwekezaji wa wataalamu, teknolojia, na fedha. Tukiamua tunaweza. Lakini kabla ya kufikiria kutengeneza chanjo ya Corona tujiulize nini kimetushinda kutengeneza chanjo zingine kama ya polio, tetekuwanga, homa ya ini etc? Jibu utakalolipata lihamishie kwenye Corona.

4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki
JIBU:
Muda wa chanjo kupatikana sio kigezo pekee cha ubora wa chanjo. Zipo chanjo nyingi zilizopatikana kwa muda mfupi na zikaonesha ufanisi mkubwa. Chanjo ya Corona imetumia miaka miwili, lakini chanjo ya matumbwitumbwi (mumps) ilitumia miezi 11 na mpaka leo inatumika.

5. Chanjo zinazotumika Ulaya sio hizi tunazoletewa Afrika
JIBU: Sio chanjo ya Corona tu, hata ARVs tunazotumia Afrika sio zinazotumika Ulaya. Hata Toyota unayoendesha Afrika sio Toyota inayouzwa Ulaya. Kwahiyo kama unadoubt chanjo basi doubt na ARVs unazomeza. Hata malaria kuna wanaotibiwa kwa Mseto na wengine Decotexin. Muhimu ni kuzingatia ubora na usalama wa hizo chanjo na si kulinganisha za Ulaya na hapa.

6. Kwanini tunalazimishwa tuchanje?
JIBU:
Hakuna aliyelazimishwa. Chanjo ni hiyari. Wewe kama hutaki basi usimuandame aliyeamua kuchanjwa, kama ambavyo yeye hakuandami wewe uliyegoma. Muhimu tafuta taarifa za kutosha kabla hujafanya maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.

7. Chanjo zina madhara
JIBU:
Hakina dawa isiyo na madhara. Hata tangawizi na malimao ya mwendazake vina madhara. Lakini mara nyingi madhara ya dawa ni madogo kulinganisha na faida itokanayo na dawa yenyewe (unless for the very rare cases kunaweza kutokea madhara makubwa).

8. Kwanini serikali haiheshimu hisia zetu sisi tuliokataa chanjo?
JIBU:
Imeheshimu ndio maana hamjalazimishwa kuchanjwa. Lakini na nyie heshimuni hisia za wale waliokubali kuchanjwa. Uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzako.

9. Kwanini chanjo ya Corona imekua ya kwanza kupingwa, nyingine hazikupingwa?
JIBU:
Si kweli kwamba chanjo ya Corona ndio ya kwanza kupingwa. Hakuna chanjo yoyote imewahi kubuniwa ikaacha kupata upinzani. Anti Vaxxers wamekuwepo tangu enzi na enzi na hawataisha hadi Yesu arudi.

Ugonjwa wa ndui (smallpox) ulipokua tishio Edward Jenner alitengeneza chanjo mwaka 1721 wakati ambapo maelfu ya watu walikufa kwa ndui. Lakini jamii ilimpinga sana. Mchungaji Cotton Mather aliikubali chanjo hiyo na kuwashauri waumini wake waitumie. Akapata upinzani mkali na kupoteza robo tatu ya waumini wake, wakimhusisha na dhana ya Mpinga Kristo.

Lakini miaka mingi baadae dunia nzima ilikubali chanjo hiyo, na kila mtu alichomwa chanjo ya ndui. Kwahiyo hakuna jipya kwa hawa Anti Vaxxers wa Corona.

10. Je Chanjo ya Corona ndio ile chapa ya 666 ya mpinga Kristo?

JIBU:
Kamuulize Gwajima!

Credit: Malisa GJ
 
4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki.

hoja zako zina amapungufu kadhaa hebu rekebisha 0 1. Ndio wamefanikiwa kwa sana .je ni mbolea kiasi gani zenye viambata vya sumu?je kuku wa kisasa je?vp kuhusu hivi vyakula tunavyozalisha tukiwapelekea wanatoa maoni gani?zaid ya kusema havifai kwa matumizi yao? Na kuongezea vyakula vingi vyenye viambata vya sumu vinatoka kwao 2.poor africans poor mindset like thear colour,wewe unadhani kuna cha bure, je kuna rasilimali tulionayo inafaidisha nchi yetu moja kwa moja .siyo tu tanzania hata africa kwa ujumla majibu yake ni wote ni tunategemeana hata hayo material wanayotengenezea madawa mengi yanatoka huku. Na wanajitahid kila siku kubuni mbinu za kuchukua rasilimaji zetu. Moja wapo ni hiyo misaada, 03 hoja namba tatu hapa ndo nilipo anza kuona umeandika utopolo, vp tulipoamua kupambana na corona sisi kama watanzania hatukufanikiwa.je njia zetu hazikuonexha matokeo ya A plus. akili
ya kutegemea cha mtu ni ya kimaskini .nilifiki kuwa hata ungejisifia tumefanikiwa kwa mbinu zetu za asili,
4. Je vipi matokeo ya chanjo ya corona hata kama hoja ni muda mchache 5. Hoja namba tano ni batili,kama kweli wanatupenda wangetupa wanachotumia wao,siyo kile kinachoneka ni uchafu ama kisichowafaa. nafananisha uwezi kumpenda mtu,halafu ukampa kisichofaa.baadhi ya chanjo wanazozileta africa ni zile ambazo kwao zimepigwa marufuku.
6. Hoja namba sita very good
7.hapa bhana brother umeyumba pakubwa , je ukipata chanjo hupati maambuki? No .ukipata chanjo hufi na maambuki ? No. Je hakuna madhala yanaoonekana baada ya chanjo? No kubwa na hakuna ajuaye. kuna tafiti za kutosha na tumejiridhisha? Hapana hamna . Je ujasiri wa hoja yako unautoa wapi! 8.hoja ya nane very good 9. Hakuna tafiti za kutosha na hata serikali haijajiridhisha usalama wake na imeikurupukia ikiachana na mpango wake wa kwanza, 10.kasome maandiko kuhusu siku za mwisho
 
Kuna "misconceptions" nyingi kuhusu chanjo ya Covid19. Baadhi za kitabibu na nyingine za elimu ya tabia. Zile za kitabibu nawaachia madaktari na wataalamu wa afya wazijibie. Mimi najibu hizi ambazo ni Socio-Cultural infuenced.

1. Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?

JIBU:
Wazungu wangetaka kutuua wana njia nyingi za kutumia. 90% ya madawa na vifaa tiba tunavyotumia vimetoka nje. Kuanzia MRI na CT scan ya Muhimbili, hadi dawa ya panadol pale zahanati ya Nanjilinji vimetoka kwa mabeberu. Kwanini wasitumie njia hizo ambazo ni rahisi zaidi kutumaliza badala ya chanjo ya Corona?

Hata hivyo kuna chanjo nyingi sana tunazitumia kutoka kwa hao tunaowaita mabeberu. Mtoto akizaliwa hadi anapofikisha umri wa miaka mitano anachomwa jumla ya chanjo 13 za aina tofauti. Na hakuna hata moja tunayotengeneza sisi. Zote tunapewa msaada na mabeberu. Je wangekua na nia ya kutumaliza si wangesubiri chanjo ya Corona?

2. Kwanini chanjo ya Corona inatolewa bure?

JIBU:
Ni chanjo ipi inatolewa hapa nchini kwa kulipiwa? Mbona hujahoji kwanini chanjo ya pepopunda, polio, tetekuwanga, homa ya ini zinatolewa bure, badala yake unahoji chanjo ya Corona tu? Halafu pia kwanini hauulizi mbona ARVs zinatolewa bure?

Je ungetakiwa kulipia ungeweza? Au serikali yako ingeweza kukununulia? Kwa mfano dozi ya mwezi ya ARVs ni kati ya $170 hadi $220 yani kati ya shilingi laki 4 hadi laki 5. Kwahiyo kama umeathirika na VVU kila unapoenda CTC kuchukua dawa kuna "mabeberu" wamekulipia laki 4 kila mwezi. Je serikali ya Tanzania ingeambiwa ikulipie ingeweza? Same applies to Corona vaccine.

3. Kwanini tusitengeneze chanjo yetu?

JIBU:
Hata mimi natamani hivyo, lakini hatuwezi kwa sababu zilezile za History ya Form 2B. Poor technology, lack of capital, poor government support etc. Kama toothpick na toilet papers tunaagiza China, je tunaweza kutengeneza chanjo ya Corona?

Serikali haijawa na nia ya dhati ya kufanya uwekezaji wa wataalamu, teknolojia, na fedha. Tukiamua tunaweza. Lakini kabla ya kufikiria kutengeneza chanjo ya Corona tujiulize nini kimetushinda kutengeneza chanjo zingine kama ya polio, tetekuwanga, homa ya ini etc? Jibu utakalolipata lihamishie kwenye Corona.

4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki.

JIBU:
Muda wa chanjo kupatikana sio kigezo pekee cha ubora wa chanjo. Zipo chanjo nyingi zilizopatikana kwa muda mfupi na zikaonesha ufanisi mkubwa. Chanjo ya Corona imetumia miaka miwili, lakini chanjo ya matumbwitumbwi (mumps) ilitumia miezi 11 na mpaka leo inatumika.

5. Chanjo zinazotumika Ulaya sio hizi tunazoletewa Afrika

JIBU: Sio chanjo ya Corona tu, hata ARVs tunazotumia Afrika sio zinazotumika Ulaya. Hata Toyota unayoendesha Afrika sio Toyota inayouzwa Ulaya. Kwahiyo kama unadoubt chanjo basi doubt na ARVs unazomeza. Hata malaria kuna wanaotibiwa kwa Mseto na wengine Decotexin. Muhimu ni kuzingatia ubora na usalama wa hizo chanjo na si kulinganisha za Ulaya na hapa.

6. Kwanini tunalazimishwa tuchanje?

JIBU:
Hakuna aliyelazimishwa. Chanjo ni hiyari. Wewe kama hutaki basi usimuandame aliyeamua kuchanjwa, kama ambavyo yeye hakuandami wewe uliyegoma. Muhimu tafuta taarifa za kutosha kabla hujafanya maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.

7. Chanjo zina madhara

JIBU:
Hakina dawa isiyo na madhara. Hata tangawizi na malimao ya mwendazake vina madhara. Lakini mara nyingi madhara ya dawa ni madogo kulinganisha na faida itokanayo na dawa yenyewe (unless for the very rare cases kunaweza kutokea madhara makubwa).

8. Kwanini serikali haiheshimu hisia zetu sisi tuliokataa chanjo?

JIBU:
Imeheshimu ndio maana hamjalazimishwa kuchanjwa. Lakini na nyie heshimuni hisia za wale waliokubali kuchanjwa. Uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzako.

9. Kwanini chanjo ya Corona imekua ya kwanza kupingwa, nyingine hazikupingwa?

JIBU:
Si kweli kwamba chanjo ya Corona ndio ya kwanza kupingwa. Hakuna chanjo yoyote imewahi kubuniwa ikaacha kupata upinzani. Anti Vaxxers wamekuwepo tangu enzi na enzi na hawataisha hadi Yesu arudi.

Ugonjwa wa ndui (smallpox) ulipokua tishio Edward Jenner alitengeneza chanjo mwaka 1721 wakati ambapo maelfu ya watu walikufa kwa ndui. Lakini jamii ilimpinga sana. Mchungaji Cotton Mather aliikubali chanjo hiyo na kuwashauri waumini wake waitumie. Akapata upinzani mkali na kupoteza robo tatu ya waumini wake, wakimhusisha na dhana ya Mpinga Kristo.

Lakini miaka mingi baadae dunia nzima ilikubali chanjo hiyo, na kila mtu alichomwa chanjo ya ndui. Kwahiyo hakuna jipya kwa hawa Anti Vaxxers wa Corona.

10. Je Chanjo ya Corona ndio ile chapa ya 666 ya mpinga Kristo?

JIBU:
Kamuulize Gwajima!

Credit: Malisa GJ

Kuna "misconceptions" nyingi kuhusu chanjo ya Covid19. Baadhi za kitabibu na nyingine za elimu ya tabia. Zile za kitabibu nawaachia madaktari na wataalamu wa afya wazijibie. Mimi najibu hizi ambazo ni Socio-Cultural infuenced.

1. Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?

JIBU:
Wazungu wangetaka kutuua wana njia nyingi za kutumia. 90% ya madawa na vifaa tiba tunavyotumia vimetoka nje. Kuanzia MRI na CT scan ya Muhimbili, hadi dawa ya panadol pale zahanati ya Nanjilinji vimetoka kwa mabeberu. Kwanini wasitumie njia hizo ambazo ni rahisi zaidi kutumaliza badala ya chanjo ya Corona?

Hata hivyo kuna chanjo nyingi sana tunazitumia kutoka kwa hao tunaowaita mabeberu. Mtoto akizaliwa hadi anapofikisha umri wa miaka mitano anachomwa jumla ya chanjo 13 za aina tofauti. Na hakuna hata moja tunayotengeneza sisi. Zote tunapewa msaada na mabeberu. Je wangekua na nia ya kutumaliza si wangesubiri chanjo ya Corona?

2. Kwanini chanjo ya Corona inatolewa bure?

JIBU:
Ni chanjo ipi inatolewa hapa nchini kwa kulipiwa? Mbona hujahoji kwanini chanjo ya pepopunda, polio, tetekuwanga, homa ya ini zinatolewa bure, badala yake unahoji chanjo ya Corona tu? Halafu pia kwanini hauulizi mbona ARVs zinatolewa bure?

Je ungetakiwa kulipia ungeweza? Au serikali yako ingeweza kukununulia? Kwa mfano dozi ya mwezi ya ARVs ni kati ya $170 hadi $220 yani kati ya shilingi laki 4 hadi laki 5. Kwahiyo kama umeathirika na VVU kila unapoenda CTC kuchukua dawa kuna "mabeberu" wamekulipia laki 4 kila mwezi. Je serikali ya Tanzania ingeambiwa ikulipie ingeweza? Same applies to Corona vaccine.

3. Kwanini tusitengeneze chanjo yetu?

JIBU:
Hata mimi natamani hivyo, lakini hatuwezi kwa sababu zilezile za History ya Form 2B. Poor technology, lack of capital, poor government support etc. Kama toothpick na toilet papers tunaagiza China, je tunaweza kutengeneza chanjo ya Corona?

Serikali haijawa na nia ya dhati ya kufanya uwekezaji wa wataalamu, teknolojia, na fedha. Tukiamua tunaweza. Lakini kabla ya kufikiria kutengeneza chanjo ya Corona tujiulize nini kimetushinda kutengeneza chanjo zingine kama ya polio, tetekuwanga, homa ya ini etc? Jibu utakalolipata lihamishie kwenye Corona.

4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki.

JIBU:
Muda wa chanjo kupatikana sio kigezo pekee cha ubora wa chanjo. Zipo chanjo nyingi zilizopatikana kwa muda mfupi na zikaonesha ufanisi mkubwa. Chanjo ya Corona imetumia miaka miwili, lakini chanjo ya matumbwitumbwi (mumps) ilitumia miezi 11 na mpaka leo inatumika.

5. Chanjo zinazotumika Ulaya sio hizi tunazoletewa Afrika

JIBU: Sio chanjo ya Corona tu, hata ARVs tunazotumia Afrika sio zinazotumika Ulaya. Hata Toyota unayoendesha Afrika sio Toyota inayouzwa Ulaya. Kwahiyo kama unadoubt chanjo basi doubt na ARVs unazomeza. Hata malaria kuna wanaotibiwa kwa Mseto na wengine Decotexin. Muhimu ni kuzingatia ubora na usalama wa hizo chanjo na si kulinganisha za Ulaya na hapa.

6. Kwanini tunalazimishwa tuchanje?

JIBU:
Hakuna aliyelazimishwa. Chanjo ni hiyari. Wewe kama hutaki basi usimuandame aliyeamua kuchanjwa, kama ambavyo yeye hakuandami wewe uliyegoma. Muhimu tafuta taarifa za kutosha kabla hujafanya maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.

7. Chanjo zina madhara

JIBU:
Hakina dawa isiyo na madhara. Hata tangawizi na malimao ya mwendazake vina madhara. Lakini mara nyingi madhara ya dawa ni madogo kulinganisha na faida itokanayo na dawa yenyewe (unless for the very rare cases kunaweza kutokea madhara makubwa).

8. Kwanini serikali haiheshimu hisia zetu sisi tuliokataa chanjo?

JIBU:
Imeheshimu ndio maana hamjalazimishwa kuchanjwa. Lakini na nyie heshimuni hisia za wale waliokubali kuchanjwa. Uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzako.

9. Kwanini chanjo ya Corona imekua ya kwanza kupingwa, nyingine hazikupingwa?

JIBU:
Si kweli kwamba chanjo ya Corona ndio ya kwanza kupingwa. Hakuna chanjo yoyote imewahi kubuniwa ikaacha kupata upinzani. Anti Vaxxers wamekuwepo tangu enzi na enzi na hawataisha hadi Yesu arudi.

Ugonjwa wa ndui (smallpox) ulipokua tishio Edward Jenner alitengeneza chanjo mwaka 1721 wakati ambapo maelfu ya watu walikufa kwa ndui. Lakini jamii ilimpinga sana. Mchungaji Cotton Mather aliikubali chanjo hiyo na kuwashauri waumini wake waitumie. Akapata upinzani mkali na kupoteza robo tatu ya waumini wake, wakimhusisha na dhana ya Mpinga Kristo.

Lakini miaka mingi baadae dunia nzima ilikubali chanjo hiyo, na kila mtu alichomwa chanjo ya ndui. Kwahiyo hakuna jipya kwa hawa Anti Vaxxers wa Corona.

10. Je Chanjo ya Corona ndio ile chapa ya 666 ya mpinga Kristo?

JIBU:
Kamuulize Gwajima!

Credit: Malisa GJ

Umetumia nguvu nyingi na vitisho kuonyesha wanaopinga kuna ujinga flani hv ambao wako nao vichwani mwao.
Kwamba wangetaka kutuua hata ARVs paracetamol,Duocotexin zingetumika kutumaliza na chanjo zilizopita.
Wewe una uhakika gani kama tuko salama na hzo,kitu kinachopandikizwa kwenye mwili majibu yake lazima yatokee tu.nikuulize tu ushawahi kumuona mtu anaekula doze ya ARVs imemkubali?
Hormone kutoku balance vp?
Mwanamke anataka kuwa mwanaume,mwanaume anatka awe mwanamke
Vp unachokiwaza au kutenda Je ndivyo ulipaswa kawaza na kutenda?
Hamasisha watu wakachome Chanjo,Kama kutuwahi walishatuwahi mapema tu
 
Kuna "misconceptions" nyingi kuhusu chanjo ya Covid19. Baadhi za kitabibu na nyingine za elimu ya tabia. Zile za kitabibu nawaachia madaktari na wataalamu wa afya wazijibie. Mimi najibu hizi ambazo ni Socio-Cultural infuenced.

1. Chanjo ya Corona ni mpango wa wazungu kutuua?
JIBU:
Wazungu wangetaka kutuua wana njia nyingi za kutumia. 90% ya madawa na vifaa tiba tunavyotumia vimetoka nje. Kuanzia MRI na CT scan ya Muhimbili, hadi dawa ya panadol pale zahanati ya Nanjilinji vimetoka kwa mabeberu. Kwanini wasitumie njia hizo ambazo ni rahisi zaidi kutumaliza badala ya chanjo ya Corona?

Hata hivyo kuna chanjo nyingi sana tunazitumia kutoka kwa hao tunaowaita mabeberu. Mtoto akizaliwa hadi anapofikisha umri wa miaka mitano anachomwa jumla ya chanjo 13 za aina tofauti. Na hakuna hata moja tunayotengeneza sisi. Zote tunapewa msaada na mabeberu. Je wangekua na nia ya kutumaliza si wangesubiri chanjo ya Corona?

2. Kwanini chanjo ya Corona inatolewa bure?
JIBU:
Ni chanjo ipi inatolewa hapa nchini kwa kulipiwa? Mbona hujahoji kwanini chanjo ya pepopunda, polio, tetekuwanga, homa ya ini zinatolewa bure, badala yake unahoji chanjo ya Corona tu? Halafu pia kwanini hauulizi mbona ARVs zinatolewa bure?

Je ungetakiwa kulipia ungeweza? Au serikali yako ingeweza kukununulia? Kwa mfano dozi ya mwezi ya ARVs ni kati ya $170 hadi $220 yani kati ya shilingi laki 4 hadi laki 5. Kwahiyo kama umeathirika na VVU kila unapoenda CTC kuchukua dawa kuna "mabeberu" wamekulipia laki 4 kila mwezi. Je serikali ya Tanzania ingeambiwa ikulipie ingeweza? Same applies to Corona vaccine.

3. Kwanini tusitengeneze chanjo yetu?
JIBU:
Hata mimi natamani hivyo, lakini hatuwezi kwa sababu zilezile za History ya Form 2B. Poor technology, lack of capital, poor government support etc. Kama toothpick na toilet papers tunaagiza China, je tunaweza kutengeneza chanjo ya Corona?

Serikali haijawa na nia ya dhati ya kufanya uwekezaji wa wataalamu, teknolojia, na fedha. Tukiamua tunaweza. Lakini kabla ya kufikiria kutengeneza chanjo ya Corona tujiulize nini kimetushinda kutengeneza chanjo zingine kama ya polio, tetekuwanga, homa ya ini etc? Jibu utakalolipata lihamishie kwenye Corona.

4. Chanjo ya Corona imetumia muda mfupi kupatikana kwa hiyo ni feki
JIBU:
Muda wa chanjo kupatikana sio kigezo pekee cha ubora wa chanjo. Zipo chanjo nyingi zilizopatikana kwa muda mfupi na zikaonesha ufanisi mkubwa. Chanjo ya Corona imetumia miaka miwili, lakini chanjo ya matumbwitumbwi (mumps) ilitumia miezi 11 na mpaka leo inatumika.

5. Chanjo zinazotumika Ulaya sio hizi tunazoletewa Afrika
JIBU: Sio chanjo ya Corona tu, hata ARVs tunazotumia Afrika sio zinazotumika Ulaya. Hata Toyota unayoendesha Afrika sio Toyota inayouzwa Ulaya. Kwahiyo kama unadoubt chanjo basi doubt na ARVs unazomeza. Hata malaria kuna wanaotibiwa kwa Mseto na wengine Decotexin. Muhimu ni kuzingatia ubora na usalama wa hizo chanjo na si kulinganisha za Ulaya na hapa.

6. Kwanini tunalazimishwa tuchanje?
JIBU:
Hakuna aliyelazimishwa. Chanjo ni hiyari. Wewe kama hutaki basi usimuandame aliyeamua kuchanjwa, kama ambavyo yeye hakuandami wewe uliyegoma. Muhimu tafuta taarifa za kutosha kabla hujafanya maamuzi ya kuchanjwa au kutochanjwa.

7. Chanjo zina madhara
JIBU:
Hakina dawa isiyo na madhara. Hata tangawizi na malimao ya mwendazake vina madhara. Lakini mara nyingi madhara ya dawa ni madogo kulinganisha na faida itokanayo na dawa yenyewe (unless for the very rare cases kunaweza kutokea madhara makubwa).

8. Kwanini serikali haiheshimu hisia zetu sisi tuliokataa chanjo?
JIBU:
Imeheshimu ndio maana hamjalazimishwa kuchanjwa. Lakini na nyie heshimuni hisia za wale waliokubali kuchanjwa. Uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzako.

9. Kwanini chanjo ya Corona imekua ya kwanza kupingwa, nyingine hazikupingwa?
JIBU:
Si kweli kwamba chanjo ya Corona ndio ya kwanza kupingwa. Hakuna chanjo yoyote imewahi kubuniwa ikaacha kupata upinzani. Anti Vaxxers wamekuwepo tangu enzi na enzi na hawataisha hadi Yesu arudi.

Ugonjwa wa ndui (smallpox) ulipokua tishio Edward Jenner alitengeneza chanjo mwaka 1721 wakati ambapo maelfu ya watu walikufa kwa ndui. Lakini jamii ilimpinga sana. Mchungaji Cotton Mather aliikubali chanjo hiyo na kuwashauri waumini wake waitumie. Akapata upinzani mkali na kupoteza robo tatu ya waumini wake, wakimhusisha na dhana ya Mpinga Kristo.

Lakini miaka mingi baadae dunia nzima ilikubali chanjo hiyo, na kila mtu alichomwa chanjo ya ndui. Kwahiyo hakuna jipya kwa hawa Anti Vaxxers wa Corona.

10. Je Chanjo ya Corona ndio ile chapa ya 666 ya mpinga Kristo?

JIBU:
Kamuulize Gwajima!

Credit: Malisa GJ

Mkuu mimi nina Maswali 2
1.Inasemekana Binadamu Tuna Kinga ya asili,Sisi Watanzania asilimia Kubwa Tumeugua Korona,Hivyo Kujijengea Kinga mwilini!
Sasa Wanasema,Hii chanjo ukishachanjwa inauwa Kinga asili Inakuwepo yenyewe,
Hivyo Corona inampata Vema tuu aliechanjwa?
2.Wakiochanjwa Homa ya Ini,Manjano hawawezi Pata Tena Homa ya Ini na Hii ndio tofauti ya chanjo hii na Chanjo zingine,
3.Korona ya Kwanza na Pili Tuliivuka wakati Italy,India walikufa sana,
Na hatukufunga mipaka sio kwamba hatukuipata Tuliipata Lakini vifo havikuwa vingi ni Kama vita Ya Kagera Tulishinda lakini Wanajeshi wetu baadhi walikufa, wengi walipona.
Naomba Ufafanuzi wa Hizi HOJA!
 
wagonjwa wa,
1.KISUKARI
2.PRESHA
3.MOYO
4.SARATANI
5.UKIMWI
wagonjwa wa maradhi hayo wanapaswa wachue tahadhari sana maana Corona itatumaliza sana.
 
Back
Top Bottom