Mandatory vaccination ni nini?
Mbowe kasema Watanzania wote walazimishwe chanjo.
Ndiyo hiyo mandatory vaccination unayoongelea?
Nchi gani inalazimisha watu wote wachanjwe?
Unaelewa kwamba hizi chanjo mpaka sasa hazijapata final approval (mfqno chanjo za Marekani hazijqpqtq final approval kutoka CDC) na zinatolewa kwa ememergency approval tu?
Hao Wamarekani wenyewe ambao wametengeneza chanjo zao hawalazimishi watu wao chanjo. Sisi tunaopewa tu chanjo ndiyo tumewazidi ujanja kutaka watu wote wachanjwe?
Wewe unaelewa kwamba si kila mtu ana hali inayofaa kupewa chanjo? Kuna wengine wenye low immunityna ukiwapa chanjo ndiyo unaongeza risk yao kufa? Tanzania wako wangapi hawa? Ukilazimisha wachanjwe halafu wakafa kutokana na chanjo utakuwa umewasaidia?
Utoaji wa lazima wa chanjo ndio huo unaoitwa mandatory vaccination au pia compulsory vaccination. Ni utaratibu ambao umekuwepo miaka mingi.
Ukisema kuwa ni uongo, utaonekana kuwa wewe ndio muongo sababu hiyo sera inafahamika duniani kote. Ndio maana nikakuuliza kwamba hujui ama unaleta utani tu?
Kama ni suala la utani tu halina shida!
Hata huyo Mbowe kwenye hiyo video uliyoileta hapa amezungumza kuhusu hiyo sera. Kuna sehemu ameitaja kabisa "mandatory". Umefanya jambo zuri sana kuileta hiyo video.
Ukimsikiliza, anasema kuwa nchi za wenzetu chanjo ni lazima, ila wameanzia kutoa kwanza kwa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele wa mapambano, wakifuatiwa na makundi maalumu, taasisi na kuendelea.
Hicho ndicho kinachoendelea kwa nchi kama Ufaransa, Uingereza, Italia, Ugiriki, Urusi na hata Marekani hivi sasa.
Marekani hivi sasa kuna vaccine mandates katika ngazi za taasisi na kampuni. Nafikiri, jana tumejadili hili na nikasema kuhusu hilo suala la "final approval" ya chanjo. Nikakuambia kwamba, tusubiri chanjo zipate full approval kutoka FDA. Isitoshe, siku si nyingi hilo litakamilika jambo litakalochochea kuongezeka kwa chanjo za lazima (vaccine mandates).
Suala la chanjo kuwa lazima nchi nzima kwa utaratibu unaofaa linaanzia kwa makundi ambayo yametajwa na Mbowe katika hiyo video. Isitoshe chanjo kuwa lazima haimaanishi kwamba serikali itatumia nguvu ya dola kulazimisha watu watoke kwenye nyumba zao kwenda kuchanjwa. La hasha!
Serikali inatunga sera ya kuhakikisha kwamba:
1) Chanjo zinapatikana kwa urahisi mahali pote nchini.
2) Kunakuwepo na vikwazo laini kwa wale wasiochanjwa kama vile kutoruhusiwa kuingia katika maeneo fulani yenye mikusanyiko ama kufanya kazi katika taasisi mbalimbali n.k.
3) Anayegoma kuchanjwa halazimishwi kwa nguvu ila tu atahitaji kufanya hivyo kama atataka kupata ajira mahali fulani ama kupata huduma fulani ya kiserikali.
Hiyo ndiyo maana ya mandatory vaccination na hii inafanyika katika hali ya dharura ambayo ni moral justifiable kama nilivyosema. Isitoshe, kabla zoezi la chanjo kufikia nchi nzima (population-wide), lazima lianzie kwa makundi fulani yaliyo hatarini zaidi kama alivyosema Mbowe.
Naweza nisikubaliane naye katika masuala kadhaa ila kuhusu hilo suala la chanjo za lazima ni suala halisi na linafanyika kwa utaratibu maalumu unaokubalika kimataifa.
Nimalizie kwa kusema kuwa, ninakushukuru tena kwa hiyo video uliyoileta. Nafikiri imesaidia pakubwa sana kutujibia maswali kadhaa kuhusiana na mjadala huu ambao tumeujadili hapa kwa muda sasa.