Changia CHADEMA

Anza kusaidia nyanya na ndugu zako walioko kijijini choka mbaya kabla ya kufanya uharibifu wa mali zako ..

Choice is yours..wengine mtoto wa dada akimuomba pesa za nauli ya shule hatoi eti anachangia chademu

Mkuu Topical,
Kuichangia chama cha upinzani ambacho kimeonyesha dira na mwelekeo wa kweli katika harakati za ukombozi wa kifikra ni kuichangia familia au jamii ya watu waliochoka na kukata tamaa.
Mkuu Topical wewe ni msomi, najua unaelewa jinsi Serikali yetu chini ya utawala wa ccm ilivyowasahau wananchi wake na kuwakumbatia matajiri.
Kuichangia CHADEMA chama ambacho kimeonyesha kwa vitendo kuwa kipo kwa ajili ya watanzania wanyonge ni kuikomboa Tanzania ya Wanyonge!
Ukweli unaujua, pamoja na kuwa unafaidika na huu utawala mbovu wa Kikwete uliopo madarakani!
 
Hela ya ruzuku haiwatoshi hadi mnaanza kuwakamua maskini? Jipangeni wazee msije mkajikuta mnachangiwa misaada ya fedha na Al-Shabaab.

Huwa unafuatilia siasa za Marekani? Umesahau Democrats wanapata michango ya fedha kutoka kwa raia wa kawaida? Hadi sasa Obama anachangisha fedha za kampeni kutoka kwa raia wa kawaida, si matajiri kama ilivyo kwa magamba.
 
CHADEMA inapenda kukushirisha,wewe mwananchi,mpenda maendeleo,mwanaharakati,na yeyote mwenye mapenzi mema na Taifa la Tanzania.Mchango wako ni wa maana kubwa sana,katika ukombozi wa Taifa.Tafadhali changia CHADEMA
changia Haki
Changia mabadiliko.

MPESA
... ... 0757 755 333
0763 744 334
0763 766 333
0758 003 509

AIRTEL PESA
0684 424 229
0684 424 144
0684 425 222

TIGO PESA
0655 788 333
0718 611 168
0718 611 126

Namba zote zimesajiliwa kwa jina la "CHADEMA ARUSHA.

Mungu akubariki sana

Mkuu umesomeka
 
Mimi ni mfugaji nataka nichangie ng'ombe mmoja.Je naweza kumtuma kwa njia ya m-pesa?

usilete utani kwenye uwanja wa mapambano.mkuu jaribu kuwa makini kuna majukwaa mengi humu. unaweza kutafuta jukwaa na ukafiti kabisa kwa mchango wako.!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom