Changamoto za Shule ya msingi Kigarama iliyopo Kata ya Igurwa, Karagwe Mkoani Kagera

MAGADO

New Member
Aug 4, 2023
1
0
photo_2023-08-05_17-09-48.jpg

Shule ya msingi Kigarama iliyopo katika Kata ya Igurwa wilayani Karagwe mkoani Kagera ni miongoni mwa shule kongwe wilayani Karagwe. Shule hii kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo upungufu wa madarasa pamoja na shida vya matundu ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi.

Mwaka jana 2022 mwezi Septemba nilitembelea shule hiyo ambayo kimsingi ipo katika kijiji chetu cha Kigarama nilimuuliza mwalimu mkuu juu ya adha hiyo ya vyoo ambayo wanafunzi wnakutana nayo ya wanafunzi zaidi ya 500 kutumia matundu manne alinijibu "Mkurugenzi anafahamu tulikwisha mpa taarifa"
photo_2023-08-05_17-09-49.jpg

photo_2023-08-05_17-09-48 (3).jpg

Nilimweleza kuwa hali iliyokuwepo ni mbaya nilifika kwenye vyoo hivyo ambavyo haviridhishi hata kwa usafi.
wiki iliyofuata nilimpigia mkurugenzi na kumueleza aliniambia analijua hilo,badae nilimpigia mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya karagwe siku chache badae katika kikao kimoja cha baraza la madiwani alieleza hilo kwa msisitizo alisema"shule zetu zinashida ya vyoo lakini nafikiri watu wa mamlaka katika eneo hili mnatakiwa kuangalia mfumo wa kusaidia shule zilizopo katika hali mbaya kama ilivyo kigarama"

Sasa ya pata mwaka hakuna mabadiliko ya namna yoyote shuleni hapo,bado adha ni kubwa, shule hii ndio huwa ni shule ya kupokea mwenge wa uhuru kutoka kyerwa kuingia karagwe na mwaka huu 2023 mwezi August zoezi hilo litafanyika hapo. lakini hakuna vyoo vya kuhudumia wananchi na viongozi wakati wa shughuli hiyo.

Licha yaviongozi wa wilaya ya Karagwe kuwa na taarifa kuhusu shule hii na bila kufanya kitu, wasiwasi wangu ni ikiwa siku ikitokea ugonjwa wa mlipuko kama kipindupindu kutokana na mazingira hayo vya kutokuwa na vyoo, wanafunzi katika shule hiyo wananchi wa kijiji hicho kata na wilaya hawatokuwa salama hata kidogo.
photo_2023-08-05_17-09-50 (2).jpg

photo_2023-08-05_17-09-48 (2).jpg

Basi kama serikali kupitia viongozi wake na miradi ya kuboresha elimu wameshindwa kusaidia afya za wanafunzi hawa basi hata waeleze wazazi na wananchi wa eneo husika kijiji Kigarama angalau wachangie ujenzi wa vyoo kwa ajili ya wananfunzi na watoto wao.

Shule hii pia ina zaidi ya wanafunzi 1000 kuna vyumba vichache vya madarasa na vya zamani ukilinganisha na maendeleo yaliyopo katika shule nyingine.
 
Back
Top Bottom