Changamoto za mahusiano mapya ukiwa 40+

Hahaha hata wa kiume wengine wana tabu, jamaa mmoja yeye nusura apigwe na vijana wa liume wa mpenzi wake, tena walimpiga mkwara wakamwambia wasimuone popote na mama yao
Watoto wa kiume kuwa na wivu na mama yao ni kawaida
 
hakuna maisha magumu na mabaya kwa binadamu kama kua single katika age ya 40+, tena ni bora ukawa single huko ujanani na sio katika 40+ age.
Ndio maana watoto wa kike huwa wanakubalianaga na yoyote maana kuwa single sio mchezo 😅😅😅 wana mashauzi wakiwa age 30 and below ila wakigonga 30+ wanakuwaga on their best behaviours ili tu wapate mtu
 
Sasa wee unadhani kidume na hela yake ataenda kutafuta bibi kizee aoe? Matumizi mabaya ya pesa hayo wakati mtaani kuna pisi kali zinakuffa njaaa 🤣🤣🤣🤣🤣

Na ndio maana watoto wa kike wana mind kwa sababu wanajua fika hulka ya wanaume ni kuchukua dogo dogo ambaye she is just there for the money.
 
Mara nyingi watu wazima hutafta watu wazima wenzao kwa ajili ya kusogeza siku nakuleleana ukikua Sana ngono sio kipaumbele kivile ka wewe kijana umri ukienda Kuna vitu unaona ni ubatili mtupu.
 
Ngoja wenyewe waje ila kuna yule Miss TZ aliolewaga na mzee Mengi kisha akamuua wote hawa ni wachumia mali tu kwahiyo nadhani haya mambo yana cut across sio jinsia moja tu. Wote ni gold diggers
 
Yaani me hii kitu inanisumbua Sana, me 40+ ya nguvu. Lkn wanawake wa size yangu nikiwapata hawaamini umri wangu. Na me wasichana wananipasua Sana kichwa! Maisha ya dar nayo yanasababisha uonekane kijana kila siku..! Yaani mwanamke wa miaka 40 nikimtongoza eti ananishangaa!! Hebu nisaidie Sky Eclat nitumie mbinu gani, me nataka hao wakubwa wenzangu.
 
Kuna wanaume Wana hela Ila ndo kusimamisha shida so atachezea binti kwa vidole na kuhonga vijihela Ila unapohitaji mtu wa kuishi naye ambaye hata ukiugua atakuguuza you don't consider sex ndo kipimo atiiiii.
Hao wa vidole wapo lakini sii unaona bado wanachukua dogodogo.
Hiyo ya mke kukuuguza nayo ni gamble tuu. Unaweza kuoa mke ukadhani atakuwa nawe benet wakati wa majanga lakini ndio akakuacha.

Ukweli usiopingika ni kwamba mwanamke either wamakamu au digidigi wanaangalia uwe wa hudumu nzuri kutoka kwa mwanaume inayopatikana kutokana na uwepo wa hela. Ndio tunarudi kwenye mada yetu ya kwamba watoto wakike wanakuwa na biti kali kwa sababu wanajua fika kuwa mwanamke hapendi bali anaangalia wapi pana maisha.
 
Watoto wataondoka wakaanze miji yao, maisha ya upweke ni mabaya sana. Umri unavyokwenda wengine wanaishi kwa msaada wa dawa za moyo na kisukari. Ukiwa na mtu wa kukuletea glass ya maji inaleta faraja.
Yaani hii dhana huwa inanitetemesha sana utu uzima unapopiga hodi.Mwenyezi Mungu nisaidie!
 
Kuwa mkarimu kwao, usijionyeshe kwao kuwa una pesa, mara nyingi wa umri huu hawana shida ndogo ndogo. Jitoe kwao kufanya vitu ambavyo wana vihitaji.
 
Mapenzi ni kama nguo, unapokufa nguo zinagaiwa kwa wanao zihitaji. Wengine wana clear kabati la nguo baada ya miaka mitatu na nguo zote kupeleka charity.
Usiyachukulie mapenzi serious sana utapata ugonjwa wa moyo.
 
Niliwahi kumtembelea Ex -wangu baada ya kufiwa na mumewe, kumpa pole na kujua anaendeleaje. Huyu alikuwa mwanamke wa ndoto yangu wakati wa uvulana,Wajanja waliniwahi, Aliwahi sana kuolewa.Nilipofika nyumbani kwake nilimkuta na kijana wake wa kiume yuko chuo mwaka wa 2.

Nakumbuka alimwita yule kijana na kunitambulisha, na hakuficha alimwambia nilikuwa nani kwake, lakini alienda mbali akaongea kitu ambacho sikutarajia kama angeongea, ilikuwa way way back akiwa na kitoto kidogo alinifuata Job, tukakaa mahali akapiga maji mbaya, akiwa na mtoto huyo huyo kijana wa chuo, Shughuli ilikuwa namna ya kuondoka hapo!!Nilimtafutia gari alifika kwa muwewe salama, akakumbusha ilivyokuwa siku ile bila kumuogopa yule kijana, ilinipa wakati mgumu kidogo lakini ilikuwa salama.
 
Kuchukua dogodogo ni case ndogo Sana you can have multiple partners wa ku sex tu na Wala no attachments at all hyo hata Mimi naweza fanya na yoyote niki tune mindsets yangu, but when it comes to someone you love, anayeku understand flows zake when your down or high someone anayegusa moyo ni case tofauti kabisa.

So hyo ya kusema gamble ni mtu unakuwa umefeli ku changa karata zako vyema, huwezi wasema wataka mwenzi mzuri unaenda kumtaftia viwanja vya ajabu ajabu, someone from bad background, isiyo na upendo malezi, even dignity na aliyekulia mazingira yasiyo na self control ujue umepata mtu lazima uumie tu.
 
Kuwa mkarimu kwao, usijionyeshe kwao kuwa una pesa, mara nyingi wa umri huu hawana shida ndogo ndogo. Jitoe kwao kufanya vitu ambavyo wana vihitaji.
Mara zote nimekua na kitu na wanawake wanaonizidi umri and I have never regretted.napenda sababu pia kichwa yangu inapata moto upesi kidogo watoto wanasumbua sana
 
Kuwa mkarimu kwao, usijionyeshe kwao kuwa una pesa, mara nyingi wa umri huu hawana shida ndogo ndogo. Jitoe kwao kufanya vitu ambavyo wana vihitaji.
Kufikia hayo ya ukarimu si kwanza akupe hiyo nafasi ya kuwa naye karibu!?? Wanawake hata usipomwambia, lkn huwa wanajua tangu siku ya kwanza kuwa mwanaume atakuja kunitongoza! Ndiyo maana km hakutaki hawezi kukupa muda hata wa kumsalimia au kumsaidia chenji....
 
Shost mmoja kazini yeye mwanaume alimtelekeza akiwa na watoto wawili wa kiume. Alipambana sana, hela ya nauli yao ya shule ilibidi awe anapika maandazi usiku na kuacha kapu hotelini akiwa anakwenda kazini.

Wale watoto walipofika chuo na yeye alipata mtu wa umri wake. Mwanaume ametoka kuachana na mke wake ndiyo anatafuta chumba aanze maisha.

Shost alimvuta jamaa ndani. Watoto walimshangaa mama! Aliwaambia tena mnyamaze, wote nyinyi mna ma girl friend, tangu baba yenu ameondoka mimi kila siku ninawaza sabuni, kodi ya nyumba, mboga ada, sasa mniache nipate ile raha mnayowapa ma girl friend zenu.!
 
Ah labda nyie mnaotaka kujua moyo wa mtu umelalia wapi ndio najua hayo mambo ya love.
Sie wengine toka tukiwa watoto tulishapewa onyo na mama zetu....mwanamke hapendi anaangalia huduma tuu hivyo jikite katika kutafuta pesa wanawake wapo tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…