Chinga One
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 11,494
- 12,465
uholanzi 2 argentina 1.....#teamholland tujuane mapema hapa.....
Stella Maganga utakuwa umevurugwa tu na waliokutuma.
Ila waambie tu kwamba Rais wetu ni Lowasa 2015
Maoni ya Wasomaji-Raia Mwema 2010
Lowassa ni jina moja wapo
Submitted by Msomaji wetu (not verified) on Sat, 2013-03-02 23:57.
Lowassa ni jina moja wapo linavuma. Kithibitisho kipo cha Wizi. Yupo huru, bado analipwa na kodi za watanzania. kithibitisho gani tena kinahitajika. Ni mtu msomi na ni mjanja kwisha kazi . Anaongea kwa utaratibu aonekane kaonewa. Anachangia kwenye makanisa kutafuta kura.Ni rafiki wa Kikwete na mambo mengi wameshirikiana.Hakuna atakayemsaliti mwenzie, ni maneno matupu na michezo ya kuwafumba watu macho. Ni mtu mmojawapo ana msururu wa viongozi nje, wanaokwenda ubia kuibia Tanzania. Ni nyoka mkubwa hatari kwa nchi ya Tanzania. Anakalia dhahabu, almasi , umeme, bila kutolea jasho.
Hana aibu.Nawashangaa wanaomuunga mkono, hawana upeo wa akili, au.
Kamuulize rais wa simba atakupa power ya Lowassa.
Kamuulize Jamal malinzi wa Tff atakupa power ya Lowassa
Kawaulize masheikh habari ya mujini ni nani watakwambia Lowassa
Kawaulize wachungaji makanisani watakwambia Lowassa ni nani
Kawaulize bodaboda watakwambia habari ya mujini ni nani
Kawaulize kina mama na wazee watakwambia habari ya mujini ni Edward Lowassa
Kamuulize mwenyekiti wa CCM taifa habari ya mujini kwenye vikao vyake ni nani atakwambia ni Edward Lowassa
Kawaulize wakulima watakwambia habari yao ni Edward Lowassa.......
Lowassa for presidency
Lowassa jembe
Lowassa jembe
huyu huyu.. sikuzote uzee dawani huyu anayejitetemekea au kuna mwingine
paul Makonda naona unajitahidi lakini MWENYEZI MUNGU HAYUKO NA WEWE.Kufuatia minongono ya Hapa na Pale kwamba ndugu EDWARD LOWASSA kuwa amedhamiria kwenda IKULU hata kwa KUKIPASUA CHAMA chake,
Kwa Mtazamo wangu na wa watu walio wengi, Hizi Hapa CHANGAMOTO KUU zinazomkabili LOWASSA kutimiza ndoto yake hiyo.
1. UFISADI
Popote linapotajwa jina la EDWARD LOWASSA, Idea ya kwanza inayokuja kichwani kwa msikilizaji ni UFISADI ULIOTUKUKA, kwamba kila Watanzania wanapoikumbuka RICHMOND, wanamkumbuka LOWASSA, kwamba kila leo LOWASSA analipwa na Serikali MABILIONI YA PESA kupitia UFISADI WA RICHMOND.
Ni vigumu sana kumtenganisha LOWASSA na RICHMOND, LOWASSA ni RICHMOND na RICHMOND ndo LOWASSA, hili halikwepeki, na Watanzania sio wepesi wa Kusahau kiasi hicho,
Upo UFISADI mwingi uliofanywa na LOWASSA, katika wizara zote alizowahi kuzitumikia na nafasi zote alizowahi kuongoza, kwa sasa itoshe tu kusema LOWASSA ni KIELELEZO KIKUU CHA UFISADI WA TAIFA HILI.
2. UTAJIRI MKUBWA
Yawezekana ni Kutokana na UFISADI wake anaoufanya, lakini ukweli ni Kwamba LOWASSA ni tajiri ambaye hata hawezi kusema mali zak amezipataje pataje, pamoja na kumiliki mali nyingi hapa Tanzania, nyingi kati ya hizo akitumia majina ya watoto zake na Maswahiba zake, lakini LOWASSA ni Miongoni mwa Watanzania wanaomiliki Mali nje ya Nchi,
Unaweza Ukajiuliza Mtumishi huyu wa Serikali wa miaka mingi aliwezaje Kumiliki NYUMBA TATU za kifahari NCHINI UINGEREZA?, NYUMBA ZA MABILLIONI YA SHILINGI, alitoa wapi utajiri huo?.
Gazti la RAIA MWEMA NOV.2010 lilitoa MOJA KATI YA PICHA YA MAJUMBA YA LOWASSA NCHINI UINGERZA.
Leo anazunguka kugawa pesa hizi chafu makanisani na misikitini, UTAJIRI HUU UNA MASHAKA MAKUBWA.
3. AFYA MGOGORO.
Kama kuna jambo linawatesa wapambe wa LOWASSA ni kudorora kwa AFYA yake kila kukicha,
Sio siri tena kwamba LOWASSA ni mgonjwa,
Pamoja na jitihada zinazofanywa na wapamb wake, kumpeleka UJERUMANI kila MWEZI kupata matibabu, Kumpatia WAGANGA wa KIENYEJI, kumpeleka mpaka kwa NABII JOSHUA ili aombewe, lakini Hali ya AFYA ya LOWASSA inazidi kuwa MBOVU kila kukicha.
Sasa hivi hawezi hata kushika kikombe kwa dakika 5 mfululizo, amedhoofika mno
Juzi alikwenda KARAGWE kumtembelea BALOZI RUHINDA ambaye amepata STROKE upande mmoja wa mwili wake,
Cha kushangaza BALOZI RUHINDA ameonekana yupo STRONG MARA DUFU kulinganisha na aliyekuja kumuona, Lowassa ameshindwa hata kutembea na mgonjwa, matokeo yak akaanguka zaidi ya mara tatu kwenye ngazi.
Jioni yake akashindwa hata kwenda kwenye Warsha aliyoandasliwa. Hii ni Hatari
Hata wapambe wake alioongozana nao ambao ni NAZIR KARAMAGI na MUSHI ambaye ni katibu wa CCM MKOA KAGERA walionyesha kufedheheka kwa namna hali ilivyokuwa.
Sasa hivi LOWASSA ameonekana kupoteza matumaini ya kugombea tena URAIS, wapambe wake hawana matumaini na Afya yake nay eye mwenyewe hana tena matumaini.
Kwa Afya ya LOWASSA hakuna muujiza utakaomuwezesha kumudu na kuhimili heka heka za kampeni za kufanya mikutano zaidi ya 10 kwa siku.
4. KUKATALIWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE
Kila mmoja anaijua nafasi ya mwalimu nyerere kwenye maisha ya siasa za Tanzania.
Mwalimu Tangu zamani alionyesha kutokumkubali kabisa LOWASSA, na kwamba UTAJIRI WAKE, UBINAFSI WAKE, UFISADI wake na dhuruma zake nyingi alizozifanya zilimpelekea mwalimu kuwa hataki hata kumsikia akishika nafasi kubwa za uongozi kwenye Taifa letu.
LOWASSA, ndio mgombea pekee anayepigiwa UPATU na viongozi na wanachama wa CHADEMA na vyama vingine vya UPINZANI, sababu kuu ya kumpigia UPATU huo ni kwamba, wanaamini kuwa LOWASSA ndio mgombea pekee ambaye ni Dhaifu na mwenye Kashfa na UBADHILIFU mkubwa kwa Taifa hili hivyo kuwarahishia njia ya kumuangusha na wao kushinda dola. Ndio maana huwezi kusikia popote Dkt.Slaa ama MBOWE akimsema vibaya LOWASSA.
NAWASILISHA.
paul Makonda naona unajitahidi lakini MWENYEZI MUNGU HAYUKO NA WEWE.
huyu huyu.. sikuzote uzee dawa
Wapi FRIENDS OF LOWASA?
Kamuulize rais wa simba atakupa power ya Lowassa.
Kamuulize Jamal malinzi wa Tff atakupa power ya Lowassa
Kawaulize masheikh habari ya mujini ni nani watakwambia Lowassa
Kawaulize wachungaji makanisani watakwambia Lowassa ni nani
Kawaulize bodaboda watakwambia habari ya mujini ni nani
Kawaulize kina mama na wazee watakwambia habari ya mujini ni Edward Lowassa
Kamuulize mwenyekiti wa CCM taifa habari ya mujini kwenye vikao vyake ni nani atakwambia ni Edward Lowassa
Kawaulize wakulima watakwambia habari yao ni Edward Lowassa.......
Lowassa for presidency
Tuwe na huruma na nchi yetu jamani. Mpaka lowassa mnataka awe Rais kweli?.
Ili akafanye nini ikulu alichoshindwa kukifanya kabla
wanyonge ni wale wanao nunuliwa kwa tisheti na wanzuki?Hakika ukipenda chongo utaliita kengeza.
Huyu mtu kapiga hela za wizi unasema alikoanzia unapajua. Wewe unajua Lowasa kuliko Nyerere?
Kiongozi aliyekubali tz iaaini mkataba wa richmond na nchi iwe inalipa dola 150,000 kwa siku bila sababu bado unasema majungu?Hakusema kwamba alikataza akalazimishwa na wakubwa?
Yeye kama PM alipoona taifa linaangamizwa, kwanini hakuside na watanzania wanyonge badala ya wanyang'anyi?
Kwanini aliogopa kukosana na wakubwa lakini hakuogopa kukosana na usaliti kwa wanyonge?
Bado majungu hayo?
wanyonge ni wale wanao nunuliwa kwa tisheti na wanzuki?
siku zote ukitaka mabadiliko chanya unatakiwa kuchukua wale wenye nia ya ku-take initiative sio wale wanaojiona ni wanyonge. Wanyonge hawana haja ya mabadiliko.
Watizedi wengi huwa hawasomi vitabu wala kufuatilia taarifa nyeti zinazohusu mustakabali wa taifa.
Mara utasikia wanapiga kelele kuwa wameona na kusikia kupitia tv na radio;kwamba bungeni kuna mheshimiwa ametukanwa,na wanafurahia utadhani wanajua chanzo na wanashabikia aliyetukanwa bila kuona undani wake. Ndio maana mkuu ameamua kutumia wasanii wa bongo fleva manake anajua huko ndiko wananchi wataelewa zaidi kuliko kutumia watu makini.
Siku zote mwenye uwezo wa kuiba ni rais wa nchi.. Sasa kama jk hajamshitaki lowassa na kwenye mdahalo round ya pili jk alijiumauma ni kitu gani kiliwafanya watizedi wampigie kura? watizedi ni wezi ndio maana ni waelewa sana kwa wezi wenzao. It obvious.
birds of the same flock fly together..je ikiwa mnaleta ngano na zilipendwa za baba wa taifa ni kitu gani walichokiamini kwa kikwete kuwa alikifanya mpaka akachaguliwa na wanamtandao akiwemo lowassa wakati wa awamu ya kwanza. Je hao watizedi waliokuwa wakifahamu historia ya lowassa kwanini hawakumkataa kikwete rafiki yake wakati wanajua wale ni chanda na pete. Na zaidi tena jk ambaye hakuchukua hatua kwa wanyonge kwa kumfunga lowasa na akiwa majukwaani anamsifia.. Mara hii wamemchagua round ya pili wakati wanajua fika alipewa maswali kwenye mdahalo akachemka na wale walio ongea point kama dk slaa wakakosa urais?
Kama nyerere alimkataa lowassa ni wapi nyerere alimkubali kikwete ?pambaffffff
rais mwinyi wanamwimba sana kama mzee wa ruksa wakati wanajua nchi ilikuwa inaoza hii, yule mswahili aliiba digrii chuo kikuu na kutembea na denti na mkewe alikamatwa mara nyingi akisafirisha nyara za taifa hatukumbuki jitihada za wanaharakati wachache waliotaka kubadili hali ya nchi .
Tumeona wezi wengi wengine wakazikwa marekani , wengine walikuwa tanesko waarudishiwa nafasi zao bila hata ya aibu kwa makofi na waheshimiwa wengi bungeni waliochaguliwa na kura za wadanganyika wapenda kupiga kura hata kama hawanufaiki.na wakastahafu nyazifa zao bila shtaka lolote. Mtabaki rais hendisamu huku mnaibiwa na kushindwa kuchukua hatua.
mwacheni lowassa anajua matatizo ya wananchi*
ajira .. Tunadanganywa uchumi unakuwa wakati ajira hakuna, shule za kata zinaendeleza kugawa ziro kwenye karne ya 21, bia na soda zinapanda bei.... Uda imeuzwa kinyemela…udini na migawanyo kitaifa imeshamiri..watizedi kwa unafiki. Ndio maana nimeapa sitapiga kura tena maishani.
Lowassa ni mtu wa vitendo hata alipokuwa pm alitenda hakuwa hofu sio mswahili. Alimkataza jk kuhusu richmond lakini jk akaruhusu mwenyewe. Ndio maana jk hana hoja ya kumshtaki lowassa. Lowassa yupo uraiani anakula maisha akiwa hana tuhuma yoyote. Lowassa alijiudhuru kulinda heshima ya bosi wake aliyemteua. Ndio maana jk huyo huyo amekuwa akitoa sifa kwa lowasa kwenye mikutano yake. Kama mnamwamini jk iweje mkatae sifa anazompa na kumshukuru lowasa pale walipoishia?