Chanel Ten Uzembe Huu Usirudiwe

dala dala

Senior Member
Nov 16, 2011
107
170
Msoma Magazeti wa leo amekosa umakini kabisa. Inakuaje asome magazeti ya wiki mbili zilizopita bila hata kusituka. Lack of concentration kwa hakika. Inabidi muombe radhi.
 

dala dala

Senior Member
Nov 16, 2011
107
170
Naona muda huu wanasoma magazeti ya leo. Umakini ni tatizo kwa vyombo vya habari. Msomaji alikuwa anatiririka tu bila kujua anachokisoma. Aibu kabisa. Then, hawaombi radhi wanakomaa tuuu
 

saimon111

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,726
2,000
Tbccm, na clouds fm and tv, ni wapuuzi kabisa, saiv kidogo na channel ten anawafata
 

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
6,601
2,000
Msoma Magazeti wa leo amekosa umakini kabisa. Inakuaje asome magazeti ya wiki mbili zilizopita bila hata kusituka. Lack of concentration kwa hakika. Inabidi muombe radhi.
Wameyapata wapi hayo magazeti ya zama za kale za mawe?
 

fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
8,625
2,000
Duh atakuwa ana juwa atakuwa mwanachama wa chama cha wezi kunahabari ambazo haziwapendezi za serekali za mitaa
 

kazimba

Member
May 19, 2013
36
95
nilikuwa sielewi,hakuna habari za serikali za mitaa....naona mambo ya miaka 53 ya uhuru nikawa bado gizani kufika za michezo naona mambo ya big brother sijakaa sawa khaa mechi ya mtani jembe haijachezwa nikadhani nipo usingizini nikapata furaha maana timu yangu ilifungwa......
 

UkomboziMpya

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
465
0
Hii ina maana kuwa yeye km mwanahabari hajui kinachoendelea hapa nchini........km gazeti lolote la leo halijaandika habari ya ukawa sio la leo. Hawa ndio wanahabari wetu kizazi cha dotcom.......kazi ipo!
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,361
2,000
Kosa sio lake yeye ameletewa tu akaona labda ndio producer alivyoandaa!
Mkuu usome gazeti la wiki mbili usishtuke. Yaani hata kuona kwamba habari ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo ndiyo habari ya mujini haimo, wewe unatiririka tu basi huna tofauti na robot!!
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,658
2,000
Hapo radhi mpaka mama wa twende kilioni akisema au kina tcra ndio wataomba radhi..
 

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,255
2,000
Kilindi


CCM imepita bila kupingwa katika vitongoji 615 na vijiji 102. Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Kilindi, Daudi Maige alisema jana kuwa kutokana na CCM kupita bila kupingwa katika vijiji 102 na vitongoji 615 uchaguzi ulilazimika kufanyika katika vijiji viwili tu, Kileguru na Makasini.

Mbeya


Mtaa wa Sabasaba nafasi ya Mwenyekiti CCM, Aidan Ng'oma, kura 74 wakati Anna Mwenda wa Chadema akipata kura 23. Mtaa wa Kisoki mgombea wa uenyekiti Edward Mwakasiti wa CCM alitangazwa mshindi baada ya kupita bila kupingwa.


Katika Mtaa wa Mwasyoke, uchaguzi wa mwenyekiti uliahirishwa, lakini kwa upande wa wajumbe, CCM ilipata viti vitatu wakati Chadema ilipata viwili. Mtaa wa Itezi, mgombea wa CCM, Anania Sanga alipita bila kupingwa, kama ilivyokuwa kwa Daud Kipenya wa chama hicho kwa Mtaa wa RRM.


Kutoka Vwawa mgombea wa uenyekiti Kitongoji cha Masaki (Chadema) alipata kura 96 wakati CCM ilipata kura 48.

Arusha


Chadema kimeendelea kukitesa CCM wilayani Karatu, baada ya kushinda viti 24 kati ya 27 katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Karatu. Katika Mtaa wa Mazingira Bora, Chadema ilishinda kwa kura 260, CCM kura 137. Kitongoji cha Bomani, Chadema ilishinda kwa kura 251 na CCM ilipata kura 177. Karatu Kati, Chadema kura 281, CCM, 109.
uchaguz.jpg
Kigoma


Katika Kata ya Mwandiga, Kigoma katika matokeo ya awali hadi tunakwenda mitamboni CCM ilikuwa imeshinda mitaa minane, ACT minane na ADC mtaa mmoja.

Dar es Salaam


Katika Mkoa wa Dar es Salaam, matokeo yalichelewa kutangazwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha malalamiko kutoka kwa baadhi ya wapigakura waliokuwa wakihisi kuwapo kwa uchakachuaji.


Katika Mtaa wa Kwa Mzungu, Kilungule, Temeke, CCM ilishinda kwa kura 378, CUF 303 na zilizoharibika ni 185.


Katika Mtaa wa Kivukoni, CCM kimeshinda kwa kura 183, Chadema (65). Mtaa wa See View, CCM imepita bila kupingwa. Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi msaidizi Renatus Luhungu.


Mtaa wa Segerea Migombani, Chadema imeshinda kwa kura (547), CCM (273), NCCR-Mageuzi (205). Mtaa wa Hananasif Kinondoni, CCM imeshinda kwa kura 472, Chadema (231).

Dodoma


Katika Manispaa ya Dodoma CCM, imeshinda katika Mtaa wa Msangalaleli Magharibi kwa kura 110 huku Chadema ikipata kura 38. Katika Mtaa wa Msangalaleli Mashariki, CCM ilishinda kwa kura 180 na Chadema 26. Mtaa wa Nzuguni A, CCM imeshinda kwa kura 408 na Chadema kupata kura 67. Mtaa wa Chang'ombe Juu, CCM imeshinda kwa kura 325, Chadema (120). Mtaa wa Bwawani, CCM 110, Chadema (40).

Iringa


Katika Mtaa wa Migombani, CCM imeshinda kwa kura 70, Chadema 58. Mtaa wa Frelimo A, CCM imeshinda kwa kura 123, Chadema 83. Mtaa wa Kondoa, Chadema imeshinda kwa kura 113 na CCM 109. Mtaa wa Darajani Chadema imeshinda kwa kura 109 na CCM (86). Katika Mtaa wa Kihesa Sokoni, Chadema imeshinda. Mtaa wa Ngeleli, CCM imeshinda kwa kura 115, Chadema (94). Mtaa wa Kidunda Chadema imeshinda kwa kura 73, CCM (69).


Katika Kijiji cha Nyabula, Wilaya ya Iringa, Chadema imeshinda kwa kura 110, CCM (72).

Morogoro


Hadi tunakwenda mitamboni CCM ilikuwa imeshinda katika mitaa 18. Katika mitaa mitano miongoni mwa hiyo sita, wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa na katika mtaa mmoja, mgombea wa chama hicho, amemshinda mgombea wa CUF.


Katika Kata ya Mbuyuni, CCM imeshinda kura 149, CUF (63). Kata ya Mwembesongo CCM imepata ushindi katika mitaa minane kati ya 16.
Mamlaka ya Mji Mdogo Nansio, Ukerewe, CCM imeshinda viti vitano huku Chadema na CUF wakiambulia kiti kimojakimoja.


Katika Mamlaka ya Mji wa Sengerema wenye mitaa 11 yote imechukuliwa na Chadema.

Mirerani


Katika Kata ya Mirerani Chadema imeshinda Vitongoji 7 kati ya 8.

Bunda


Hadi tunakwenda mtamboni katika, vitongoji 15 vya mjini Bunda na Nyamuswa CCM ilikuwa imeshinda Vitongoji saba, Chadema saba na CUF kimoja.

Njombe


Mtaa wa Posta, Chadema imeshinda kwa kura 218, CCM (216). Mtaa wa Joshoni, CCM imeshinda kwa kura 210, Chadema (155). Mtaa wa Kambarage, Chadema imeshinda kwa kura 479, CCM (288).
 

Zimamoto

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
464
195
Mkuu usome gazeti la wiki mbili usishtuke. Yaani hata kuona kwamba habari ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo ndiyo habari ya mujini haimo, wewe unatiririka tu basi huna tofauti na robot!!
Hii naifananisha na naibu waziri aliyesoma visiwa vya Pemba na Zimbabwe viliungana na Tanganyika kuunda Tanzania.
 

Mokoyo

JF-Expert Member
Mar 2, 2010
15,174
2,000
nilikuwa sielewi,hakuna habari za serikali za mitaa....naona mambo ya miaka 53 ya uhuru nikawa bado gizani kufika za michezo naona mambo ya big brother sijakaa sawa khaa mechi ya mtani jembe haijachezwa nikadhani nipo usingizini nikapata furaha maana timu yangu ilifungwa......
nimecheka sana kwa hii post
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom