Chami, Mkulo, Mponda, Ngeleja na Maige walionewa!

Mwanamalundi

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,125
1,432
Yes. Hawa mawaziri walionewa. Mbona hatujasikia wafanyakazi wa ngazi za chini waliofanya yale madudu wameshughulikiwa. Dr.Kigoda yeye ali "deal" na ekelege tu, halafu santuri ya muziki ikazimika. Balozi Kagasheki tumeona kidogo, japo haitoshi.

Warning. Mawaziri mliokabidhiwa Wizara zilizokuwa na madudu katika Bunge lililopita msipokuwa makini mtaangukia kwenye kundi la kondoo wa KAFARA katika bunge linalokuja. Shughulikieni hao vijana walio chini yenu ambao ndio chanzo cha matatizo.

Anzeni kumpa pressure JK afukuze kazi makatibu wakuu wote waliosababisha "fiasco" ile, kisha rungu lishuke kwa watendaji wa Chini. Msipofanya hivyo, CDM watashuhudia mazishi ya CCM, mwaka 2015.

Nawasilisha.
 
Mkuu,
Uwaziri siyo right ni privelage. Kama jinsi kupewa uwaziri kusivyo kupendelewa, kukosa uwaziri haiwezi kuwa kuonewa.
 
Mkuu naomba unisome vizuri. Wameonewa kwa sababu waliosababisha hayo madudu bado wamo wizarani wanaendelea kupeta na kupika madudu mengine. Mbona hatujasikia kwamba waliosababisha yale madudu wameshughulikiwa? Ndio maana tunasema huu ni uonezi. Na hao mawaziri waliopewa hizo wizara wanatakiwa kuwa makini sana. Vingenevyo, itakula kwao next time. Just wait, time will tell.
 
Ndio siasa ilivyo..........hakuna uonevu kwa kazi ya kupewa......utaonewa kama uliihangaikia kazi
 
Tatizo ni kwamba wengi walikuwa fixed baada ya kuonekana mitandao yao ya 2015 haisomi ramani mmoja na mkulu. Kama huamini kwa nini G. Mkuchika pamoja na kashfa kubwa kugusa wizara yake hajaondolewa? Je, Jumanne Maghembe ameondoka? Selina Kombani alipinga uwepo wa katiba mpya lakini anapeta. Tatizo ni mitandao mkuu kuelekea 2015. Sijasema hawajala rushwa kwa hiyo wameonewa - hapana. Nimesoma hoja ya kubaki au kuondolewa siyo Rushwa ni mtandao. Unaweza ukala rushwa wazi wazi na ukapeta vile vile. Je, tutafika 2015 salama? Kwa neema ya Mungu, YES, and thati is my prayer.
 
Mimi Msimamo wangu bado uko palepale. Haiwezekani waziri peke yake tu ndio awajibike wakati waliosababisha hayo madudu bado wanapeta. Basi serikali itamke wazi kuwa Mabadiliko ya baraza la mawaziri yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida ambayo hayana uhusiano na "fiasco" iliyotokea bungeni mwezi April. Hapo nitaelewa. Vinginevyo, mimi bado nasema akina Maige na Ngeleja walionewa.
 
Mkuu, nimekupata. Inawezekana kuna ukweli ndani ya hoja yako. Maana mie nilikuwa najiuliza, hivi matatizo maliasili ni maige peke yake tu? vipi kuhusu Nundu? Wameonewa. Mpaka wengine washughulikiwe ndio nitaamini kwamba hawa jamaa waliondolewa kwa kashfa. Otherwise, akina chami na wachapa kazi wazuri. Fitna na majungu, na mtandao ndio vyanzo vya uonevu huu.
 
Mimi Msimamo wangu bado uko palepale. Haiwezekani waziri peke yake tu ndio awajibike wakati waliosababisha hayo madudu bado wanapeta. Basi serikali itamke wazi kuwa Mabadiliko ya baraza la mawaziri yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida ambayo hayana uhusiano na "fiasco" iliyotokea bungeni mwezi April. Hapo nitaelewa. Vinginevyo, mimi bado nasema akina Maige na Ngeleja walionewa.

Kawaida hatuendi hivyo.........ni rahisi kumuwajibisha mwanasiasa(waziri- hana mkataba wa ajira) kuliko mtendaji (ana mkataba huyu)......kwa utuuzima wangu hii ni mara yangu ya kwanza kusikia Mawaziri wakilalamika kuondolewa.......miaka yote haya hufanyika na kuisha kimyakimya tu.....hata Lowassa aliwekwa benchi na Mkapa kwa muda tu (1995-1997)
 
Kaka, Inawezekana upo sahihi. Lakini kwanini hawa makatibu wakuu na maafisa walioshiriki kuleta ile "fiasco" wasisimamishwe kazi ili kupisha uchunguzi? Mbona Davidi Jairo amesimamishwa kazi hadi leo hii? Mbona Blandina Nyoni amesimamishwa kazi hadi leo hii? Kuna ugumu gani kuwasimamisha kazi hao viongozi wengine? Ndio maana nasema hawa Ndugu zangu akina Ngeleja, Maige, Nundu, Mkulo nk wameonewa.

NB hao mawaziri wapya wamekali kuti kavu. Trust me. Time will tell.
 
Mkuu naomba unisome vizuri. Wameonewa kwa sababu waliosababisha hayo madudu bado wamo wizarani wanaendelea kupeta na kupika madudu mengine. Mbona hatujasikia kwamba waliosababisha yale madudu wameshughulikiwa? Ndio maana tunasema huu ni uonezi. Na hao mawaziri waliopewa hizo wizara wanatakiwa kuwa makini sana. Vingenevyo, itakula kwao next time. Just wait, time will tell.

Kwani kunyimwa uwaziri ni adhabu? Wale wabunge wengine ambao hawajapewa uwaziri wako kwenye adhabu? Wewe umeshawahi kuteuliwa na Rais kushika nafasi yoyote? if not, je uko kwenye adhabu?
Ndio maana nakwambia walipopewa uwaziri walipewa privelage, sasa uwaziri amepewa mwingine, huyo ni zamu yake kupata privelage. Hakuna aliyeonewa, wangekuwa wameonewa iwapo wangevuliwa Ubunge walioupata kwa jasho lao baada ya kunadi sera kwa wananchi sio uwaziri...
 
Kaka, adhabu na kuonewa ni vitu viwili tofauti. Nisome vizuri. Sijasema kwamba hawa jamaa wamepewa adhabu. Nimesema wameonewa. Ndio maana serikali haijachukua hatua yoyote kwa watuhumiwa waliosababisha ile "fiasco" ya April,2012.
 
Kuonewa ni kunyimwa kitu ambacho mtu ana haki nacho. Hakuna mwenye haki ya kuwa waziri, uwaziri ni privelage ndio maana nasema hakuna kuonewa kwenye kunyimwa uwaziri. Rais ana haki ya kikatiba kumpa mtu yeyote wakati wowote uwaziri vilevile ana haki ya kumtoa waziri yeyote wakati wowote kwenye nafasi hiyo. Ukisema hawa wameonewa unaingilia haki ya Rais kufanya maamuzi yake ya kikatiba na unawapa hawa waliofutwa haki wasiyokuwa nayo...
 
Haya Kaka. Swali. Mbona watumishi wengine waliosababisha yale madudu hawajashughulikiwa?
 
kama mlimsoma vizuri jk alipowa-
drop mawaziri yao alionesha wazi kuwa wao ha
hawakuwa watndaji wabaya ila wale wsliochini yao. hataivyo aliahaidi kuchukua hatua dhidi yao mpaka leo hajafanya hivyo.
 
Nadhani ingekuwa vizuri kama ungechambua tuhuma za kila waziri halafu ueleze ni kwann walisingiziwa. Hii si hoja bado.

Samahani Lakini
 
kama mlimsoma vizuri jk alipowa-
drop mawaziri yao alionesha wazi kuwa wao ha
hawakuwa watndaji wabaya ila wale wsliochini yao. hataivyo aliahaidi kuchukua hatua dhidi yao mpaka leo hajafanya hivyo.

Kaka, tupo ukurusa mmoja. Alisema hivyo. Hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi sasa. Ndio maana nasema hawa jamaa wameonewa. Panga lingeshuka mpaka kwa watendaji hapo haki ingelikuwa imetendeka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom