Tukiachilia mbali mambo ya vyama/itikadi, mimi ni mmoja ya wana JF walio wahi kupigia kelele suala zima za watendaji wakuu wa Wizara zilizo husika moja kwa moja na kashfa. Mpaka sasa sioni kama kuna dalili yeyote ya kulishughulikia suala hili aidha kwa kuhamishiwa wizara nyingine au kustaafishwa kwa manufaa ya umma kama MAWAZIRI walivyo wajibishwa. Wakibaki bila ya kufanywa lolote, basi RAIA wanaweza ku-conclude kwamba labda mawaziri walionewa.
Mwanzo nilifikili labda waliachwa kwa muda ili washugulike na utayarishaji Budget za Wizara, lakini naona siku zinakwenda tu na wenyewe wanaendeleza ubabe wao wa kutowajibika wala kuogopa chochote, yaani wanajiona wenyewe na mawaziri hawana tofauti yoyote - niliwahi kusema hivi: insurbornation kati ya baadhi ya makatibu wakuu na mawazari ni wa kutia aibu kubwa Serikali yetu, si hilo tu yaani mtu unaona wazi wazi kwamba Waziri na Katibu mkuu wake hawaelewani hata kidogo - hawafichi uhasama kati yao, hii nini lakini?? Namuomba JK alishugulikie suala hili mapema iwezekanavyo akifanikisha hilo nidhamu itarudi katika utendaji kazi wizara husika, lakini JK akijisahau kulishughulikia basi ajuwe kwamba Mawazari alio wa-appoint hivi majuzi watapata wakati mgumu katika Wizara zao mpya - oh yes jamaa watakuwa wamejitayarisha kuwawekea SPANA ili wakwame katika kazi zao - chunga sana MKUU.
Tukumbuke kwamba Makatibu Wakuu na wakurugenzi ndio watendaji wakuu wa wizara, Mawaziri ni wa kupita tu lakini watendaji wakuu kama makatibu wakuu na wakurugenzi wanabaki kazini mpaka siku ya kustaafu kwao, kwa mawazo yangu si jambo la busara kuwabakiza sehemu moja kwa muda mrefu, wanajusahau sana, yaani inasikitisha sana tukikumbuka kwamba JK aliwahi kuwapa semina na muongozo wa utendaji kazi huko ARUSHA, lakini inaonekana effort zake zote zilikuwa ni "sawa sawa na hakuna" (msemo wa zamani wa mahafande wa Jeshi la kujenga TAIFA).
Mwisho labda niseme kwamba, lingekuwa ni jambo la BUSARA kama makatibu wakuu wangekuwa wanateuliwa na Waziri Mkuu, ili wa wajibike kwake moja kwa moja hii itarudisha nidhamu kazini.