Balaa kubwa: Baada ya kutimliwa na JK; Mkulo, Maige kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balaa kubwa: Baada ya kutimliwa na JK; Mkulo, Maige kortini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, May 8, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MARA baada ya Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki iliyopita kulisuka upya baraza lake la mawaziri kwa kuwatosa mawaziri sita kati ya wanane waliokuwa wametajwa kwa kashfa mbalimbali katika ripoti ya Mdhibiti Mkuu na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), mawaziri wawili wamo mbioni kushitakiwa kortini. Habari kutoka ndani ya serikali zinasema tayari maofisa wa serikali wanaandaa makabrasha ya kuwafikisha mahakamani maofisa kadhaa akiwemo aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

  MUSTAFA MKULO
  Mkulo ndiye aliyekuwa waziri wa kwanza kutakiwa na wabunge ajiuzulu kwa kutuhumiwa kuvunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili kuficha tuhuma zake ikiwamo uuzaji wa kiwanja Na.10 kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL). Ukaguzi wa CAG ulibaini kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina na Wizara ya Fedha zilihusika moja kwa moja katika uuzwaji wa kiwanja hicho Na.10 kilichopo kando ya Barabara ya Nyerere bila kuishirikisha bodi ya CHC. Aidha, CAG alibaini kuwapo kwa matatizo katika hati ya madai ya Shilingi bilioni 2.4 kutoka katika Kampuni ya DRTC kama gharama za ulinzi na tozo la matumizi ya barabara ya kuingilia kwenye Kiwanja Na.192 kando ya Barabara ya Nyerere. Upungufu pia ulionekana kwenye uuzwaji wa jengo la Kampuni ya Tanzania Motors (TMC) lililopo kiwanja Na.24 kilichopo katika eneo la viwanda la Chang'ombe kwa Kampuni ya Maungu Seed.

  EZEKIEL MAIGE
  Maige akiwa Waziri wa Maliasili na Utalii ripoti ya CAG ilieleza kuwa ofisi yake ilipoteza Shilingi 874,853,564 baada ya kufanya uamuzi wa upendeleo wa kutoa kiwango cha chini cha mrahaba kwa mauzo ya misitu. Katika kipindi cha ukaguzi wa hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (Tanapa) ilibainika kuwa shirika liliingia katika mkataba na Kampuni ya CATS Tanzania LTD unaohusiana na matengenezo ya kawaida, ufungaji wa vifaa vya mawasiliano na vifaa vingine katika mkataba wa jumla ya dola milioni moja za Marekani.

  Alishutumiwa kwa kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ugawaji ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha ni vitalu vipi walivyopewa. Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili. Mbali na tuhuma hizo, Maige hivi karibuni alidaiwa kununua nyumba kwa Dola za Marekani 700,000 iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua kwa Dola 410,000, (sawa na zaidi ya shilingi milioni 600 za Kitanzania).

  Habari za ndani kutoka serikalini zilizotufikia zinasema mara baada ya Rais Kikwete kutoa tamko la wahusika wa ubadhirifu huo ‘washughulikiwe', tayari nyaraka mbalimbali zimeanza kushughulikiwa na vyombo vya dola ili kuona nani aliiba na nani hahusiki. Waliokuwa mawaziri na kutemwa nao wanamulikwa na vyombo vya sheria.
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sheria ni msumeno inakata kotekote

  wangeachwa pia tungelalamika mahakama itatupa jibu juu ya tuhuma dhidi yao
   
 3. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Danganya toto kula..... Hakuna kesi za ufisadi katika nchi hii, chini ya utawala wa ccm unaoongozwa na mkwe.re... Sababu moja ya msingi ni kwamba, mkulu mwenyewe ndio fisadi namba 1... Anashilikiana nao kuitafuna hii nchi.... Kuhusu hizi kesi tuhesabu maumivu mpaka 2015 CDM itakapochukua nchi.
   
 4. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  uh kaazi kweli kweli
   
 5. M

  Mtokambali Senior Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kumbe muandaa mashtaka mwenyewe ni Mtikila! Nothing really serious!
   
 6. K

  Kalimanzira Senior Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa balaa hapo ni nini! Kama kulikuwa na nia ya dhati ya kuwaondolea ulaji wao tena kwa tuhuma, ni vema wafikishwe mahakamani ili sanaa iendelee!
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  Maigizo hayaishi nchi hii!
   
 8. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona jk anatafuta namna ya kutuliza upepo tu. kesi itaendeshwa, watashinda na mwisho serikali itawalipa fidia, mgao utakuwa wa jk na mtuhumiwa. nchi ilishauzwa tusitarajie kitu hapa, ni mchosho tu.
   
 9. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkapa, Mramba, Mgonja, Chenge, Ikerege wanakula kuku,kwanini Maige na Mkullo washitakiwe wao tu!!! not fair kama ni panga wafyekwe wote.
   
 10. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  No standards
   
 11. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It matter most how it ends.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu hapo, just another drama series. Afu ona ulivyoiweka title kidaku. Balaa!, balaa kitu gani wao walipokuwa wanazikomba walidhani nini?

  Na ccm walivyo na ufedhuli na wazimu wanajitokeza na kutaka credits kwa kuwapeleka washtakiwa/watuhumiwa wa kuhujumu nchi hii. Shame upon their very souls.
   
 13. UBISHI

  UBISHI Member

  #13
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu weka paragraph.Hivi ulivyoandika inaumiza macho,
  back to the topic: Takukuru mpaka waambiwe shughulika ndio wakurupuke,kuna namna nyingi za kufuatilia rushwa ama wizi.Ni kiasi cha kuwa karibu na CAG,wakati wanafanya ukaguzi wa hesabu mathalani wilaya ya Kinondoni na wao wanafuata nyayo.

  Lakini zaidi ya hapo ni magumashi tu
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kabla ya Kikwete uliwahi zisikia hizi kesi?

  Kikwete anashirikiana na nani kuitafuna hii nchi, tunaomba uje kutowa ushahidi tunataka kuwapeleka mahakamani wote wanaohusika na msiba huu, jee upo tayari kujitokeza kutoa ushahidi? maana inaonesha unajuwa mengi sana.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkulo ana hela nyie hawezi kufungwa...mahakimu wa kwetu hapa walivyo na njaa huyo yaani ni NOT GUILTY kabisa hamna kitu...huyu jamaa anaweza kutengeneza ile jela pale ukonga chumba chake kikawa kama anacholalia nyumbani kwake so hata mkimfunga ni sawa na ka vile yuko kwake
   
 16. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,589
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Huo ni usanii tu, kwani kina Mramba na wenzake miaka mingapi kesi inasikilizwa? Ni kusubiri tu upepo upite watu waendelee kula kuku. Na wezi wa mali ya umma Tz. Wako wengi na wanafahamika lakini hawaguswi.
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hapo ndio pameniacha hoi kabisa.

  Ninavyofahamu mimi manunuzi kama hayo pia huwa yanaendana na malipo kwa TRA sasa ameipa TRA stahiki yake au ana excemption kama waziri?
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unataka kusema kwamba wakina Mramba wao au serikali inapenda kesi zisiishe?

  Mbona kuna wananchi wa kawaida kesi zao zipo miaka 10 haziishi? kwanini wakina Mramba kesi iishe fasta wao kama wakina nani?
   
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  acha ninunue popcorn kucheki hii movie
   
 20. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Maige pia kamnunulia Wema Sepetu gari la kifahari, ndio anamtia siku hizi..... go & ask kama hamjui ...
   
Loading...