Takukuru yawachunguza Mawaziri wanaotuhumiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru yawachunguza Mawaziri wanaotuhumiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, May 2, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Katika kuonyesha JK amedhamiria tusome habari hii!

  Boniface Meena
  Takukuru yawachunguza Mawaziri wanaotuhumiwa

  SAKATA la ufisadi ulioanikwa kwenye ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), limeingia sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuanza kuwachunguza watendaji wote waliohusika, wakiwamo mawaziri.

  Hatua hiyo ya Takukuru imekuja wakati tayari Kamati Kuu (CC) ya CCM imebariki uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kulisuka upya Baraza la Mawaziri kama hatua mojawapo katika kutekeleza maazimio ya Bunge kutaka mawaziri wanane na watendaji waliotajwa katika ripoti ya CAG wawajibishwe.

  Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hoseah alisema jana kuwa pamoja na hatua ya Rais ya kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri, taasisi hiyo imeanza uchunguzi wake dhidi ya wahusika.

  Dk Hoseah alisema ofisi yake imeshaanza kushughulikia tuhuma zote za rushwa zilizotolewa na CAG na baadaye kupigiwa kelele na wabunge ili watakaobainika wafikishwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

  “Sheria inatutaka tufanye uchunguzi wa tuhuma zozote na katika hili, CAG alitakiwa atupe taarifa. Lakini sisi baada ya kusikia bungeni tulimwandikia barua (CAG) kumwomba atupatie ripoti ya mambo yanayotuhusu tuanze kuyashughulikia haraka,” alisema Dk Hoseah.

  Hata hivyo, Dk Hoseah alisema asingeweza kuwataja watu wanaowachunguza kwa majina, kwa kuwa sheria (Kifungu cha 37 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007, kinazuia kuzungumzia mchakato wa uchunguzi).

  Lakini, mawaziri waliotajwa katika ripoti hiyo ya CAG na hivyo kushinikizwa kujiuzulu ni William Ngeleja wa Nishati na Madini na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu.

  Wengine ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami.

  “Siwezi kusema tunamchunguza nani kwani sheria hairuhusu ila elewa tu kwamba tuko serious (makini) na tunafanyia kazi tuhuma zote na wote tutahakikisha tunawafikia,” alisema Dk Hoseah.

  CAG akiri

  Kwa upande wake CAG, Ludovick Utouh alikiri kuwasiliana na Takukuru kuhusu kuwachunguza wote waliotajwa katika ripoti yake.

  “Kimsingi ofisi yangu inafanya kazi kwa karibu na Takukuru na barua waliyotuandikia tunaendelea kuifanyia kazi. Sheria inatueleza kwamba katika ukaguzi wetu, tunapokutana na suala lolote la rushwa tuliwasilishe Takukuru na tumekuwa tukifanya hivyo,” alisema Utouh.

  Awali, wakati sakata hilo likiwa bungeni, kuliibuka malumbano ya hapa na pale miongoni mwa mawaziri na wasaidizi wao huku watendaji hao wa wizara, wakitupiana mpira kuhusu kashfa mbalimbali zinazoelekezwa kwenye ofisi zao.

  Kashfa za mawaziri
  Waziri Nundu na Naibu wake, Athuman Mfutakamba kwa upande mmoja na Waziri Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu walianza kutupiana mpira huku kila mmoja akijisafisha kiaina.

  Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu katika utetezi wake alisema Naibu wake huyo amekuwa akishinikiza Kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga gati namba 13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ilimgharamia safari kadhaa kwenda nje.

  Waziri Nundu pia alishangazwa na shinikizo la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya Mwenyekiti wake, Peter Serukamba kuingia na kushinikiza CCCC ipewe kazi hiyo huku akihoji kuna nini?

  Hata hivyo, Mfutakamba alipoulizwa kuhusu safari zake hizo za nje kugharamiwa na CCCC na baadaye kuandika ripoti akishinikiza ipewe kazi ya kujenga gati hizo, alikiri kusafirishwa na kampuni hiyo, lakini akasema alifuata taratibu zote za kiserikali.

  Nyalandu kwa upande wake, alionekana kutua mzigo wa kashfa ulioigubika wizara hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege kudaiwa kuiingizia Serikali hasara ya karibu Sh30 milioni kwa ukaguzi hewa wa magari nje ya nchi akisema alimshauri Waziri wake, Dk Chami kumsimamisha kazi mkurugenzi huyo mapema.

  Lakini Dk Chami alisema hadi Bunge linamalizika mjini Dodoma, alikuwa hajaiona ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge iliyomchunguza Ekelege ambayo alisema ingemsaidia kupata tuhuma zinazomkabili mkurugenzi huyo ili kuchukua hatua.

  Mkulo ambaye alikuwa waziri wa kwanza kutakiwa ajiuzulu, anatuhumiwa kuvunja Bodi ya Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) ili kuficha tuhuma zake ikiwemo uuzaji wa kiwanja Na.10 kwa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL).

  Mkuchika alitakiwa aachie ngazi baada ya ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kubaini mtandao mkubwa wa wezi wa mali za umma. Ripoti hiyo ilibainisha kuwa kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2010, Sh583.2 milioni zililipwa kama mishahara hewa, kiasi ambacho kingetosha kujenga madarasa 194.

  Ripoti ya CAG ilibaini kuwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa mwaka mmoja wa fedha linafanya ununuzi wenye thamani ya Sh300 bilioni hadi Sh600bilioni, hivyo kumtaka Waziri Ngeleja awajibike.

  Katika mwaka wa fedha 2009/2010, Tanesco ililitumia Sh1.8bilioni ukilinganisha na Sh65 milioni zilizokuwa zimepangwa katika bajeti ya ukarabati wa gati mojawapo katika Kituo cha Bwawa la Mtera na kuingia mikataba isiyo na tija kwa taifa.

  Waziri Maige anakabiliwa na tuhuma za kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji, ambao inadaiwa ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwa ni pamoja na kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha maeneo waliyopewa.

  Pia, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Maliasili ilieleza kuwa kampuni 16 zilizopewa vitalu hivyo hazikuomba na kwamba vitalu hivyo vilikuwa vya daraja la kwanza na la pili.

  Mbali na tuhuma hizo, Maige pia anakabiliwa na kashfa ya kununua nyumba kwa Dola za Marekani 700,000 iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam, tuhuma ambazo alizipinga na kusema kuwa nyumba hiyo ameinunua kwa Dola 410,000, (wastani wa Sh600 milioni).

  Waziri Mponda ametakiwa kuwajika baada ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), ambako ukaguzi maalumu wa MSD uliofanyika kubaini kuwapo tofauti ya Sh658.9 milioni ikiwa ni pungufu ya kiasi ambacho kilipokewa na kuripotiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwenda MSD na ushahidi wa kupokewa haukutolewa.

  Pia kulikuwa na kiasi cha Sh100 milioni kilichopelekwa na MSD kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kikatumiwa na MSD bila kuwapo na mchanganuo wa matumizi.

  Ukaguzi maalumu ulibaini pia kuwapo kiasi cha Sh4.5 bilioni zilizotoka Hazina kwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa vya hospitali, lakini ni kiasi cha Sh4.344 bilioni tu kilichopokewa na MSD ikiacha Sh196 milioni bila kuwepo na ushahidi wa kupokewa na MSD kutoka wizarani.
   
 2. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  anachunguza nini wakati rushwa imeshathibitishwa na ipo kwenye maandishi cha ajabu boss wao rais ameshaiyona na kuiruhusu wabunge wachukue hatua hawana lolote cha muhimu wao na usalama wa taifa wafutwe tu hawana taarifa nyeti na hawasaidii serekali katika kutatua matatizo wanasubiria nimuhonge mtendaji wakata ndo wanikamate wajidai wapo kazini.Uozo mtupu
   
 3. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  hapo hamna jipya mkuu. huyo Hoseah anahusika sana na rushwa ya richmond na dowans. huyo hoseah ndo aliyewasafisha richmond na dowans kwamba hakuna rushwa iliyotumika katika kupewa mikataba baada ya bunge kumwambia awachunguze. tume ya mwakyembe ndo ilikuja kugundua madudu baadae sana.
  Hoseah bado anahusika katika ununuzi wa rada. katika mgao wa rushwa naye alipata akishilikiana na mwenzake chenge.
  CAG kasema kila mwaka anawapa report lakini haifanyiwi kazi. je nyani atamuwinda ngedere?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is funny

  System inakua reactive badala ya proactive na wana bajeti ya uchunguzi ili kuprevent haya madudu,

  I am very disappointed kusema ukweli...

  And sadly the newspapers are playing a good messenger while we know takokuu has been doing this all along and nothing has come out of anything except burning the funds
   
 5. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uchunguzi wa nini wakati CAG amekwishamaliza kila kitu? Wahusika wapelekwe mahakamani tu....
   
 6. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa na uwezo hii taasisi ya takataka ningeifukuzia mbali...ni ulaji mwingine wa wala rusha wazuri kuliko inavyodhaniwa..kwani kabla ya hawa mawaziri hakuna wengine? Au ndo zuga kwa watanganyika sisi..!?
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hawa wote lao moja...2008 lowasa alijiuzulu kwa sababu ya skendo ya richmond/epa..nini kilifanyika? hakuna...kuna viongozi wameshajiuzulu kwa sababu ya rushwa toka 2005 leo hii wapo mtaani...takukuru na wengineo wote hamna kitu..huyo director wao saivi anajidai anaongea kwa sababu hii kitu ni hot topic mjini hapa...atuambie ameshakamata wangapi na wangapi wameshafikishwa mahakamani...na sitaki aseme wale wala rushwa wa huko vijijini nataka atuambie top dogs...i.e former mawaziri na makatibu wangapi washafungwa or kufilisiwa mali zao....give me a break...hata hawa takukuru nao ni mafisadi vile vile
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,788
  Likes Received: 83,160
  Trophy Points: 280
  Takukuru ni janga la Taifa...haistahili kabisa kuendelea kuwepo.
   
 9. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uwezo huo hawana, hata wakijitahidi huwa wanachunguza mpokea rushwa tu, hizo kampuni za nje ni untouchable. Ni bora kutokuwa na institution kama hiyo kulikuwa kuwa na bogus institution kama Takukuru
   
 10. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #10
  May 2, 2012
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  hiyo ni danganya toto na ni kufurahisha Jamvi. siamini kama takukuru ilivyoshindwa kuchunguza suala la rada na ndege ya raisi bila kusahau richmond .. leo ichunguze suala la mawaziri... nasema na nasisistiza hilo changa la macho hamna kitu.
  mbona kesi za kila mramba na yona zimepotelea kusikojulikana. hamna kitu, zaidi ya kupoteza resources za watanzania.

  mpaka katiba ibadilishwe rais aache kuteua mkuu wa Takukuru na hadi hapo Takukuru itakapokuwa huru (namaanisha uhuru wa kweli) na pia kuchagua mkuu wa takukuru kwa misingi ya utendaji kazi na si ukada wa chama ndo NITAIAMINI
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  May 2, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Dr. Hossea hafai kuwa mkurugenzi wa TAKUKURU? Hiv PhD holder kweli unasubiri mpaka CAG akupe ripoti ndio ukachunguze? Sio kwamba kazi ya TAKUKURU ni kuokoa pesa za umma? TAKUKURU mlitakiwa kuona mapema na kuzuia madudu hayo. Nafikiri TAKUKURU ivunjwe na kazi zake kwenda kwa CAG!!
   
 12. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #12
  May 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu Hosea hivi ni mtanzania kweli?

  Sijawahi kusikia amempandisha mtu kizimbani zaidi ya kuwasafisha wezi. hapo atatumiwa chake na atanunua sabuni kuwasafisha hawa watuhumiwa wang'ae
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  May 2, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu tumpe muda hosea afanye kazi, msichanganye taaluma na siasa!
   
 14. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #14
  May 2, 2012
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kinga ni bora kuliko tiba? Sikuzote walikuwa wapi? mtu unaenda choni kabla ya kuhara? ukishajinyea chooni unaenda kufanya nini?
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  May 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hakuna sababu ya kuwachunguza kwasababu siyo sera ya CCM kuwajibishana kwa wizi na ubadhirifu wa mali ya umma!
   
 16. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Waanze kujichunguza kwanza manake wanakula rushwa hawa takukuru vibaya sana.
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama kuna taasisi siiependi nchi hii ni pamoja na takukuru, hawa jamaa hutumika kama omo kuwasafisha mafisadi wote ambao kimsingi ni vigogo, wale ambao rank zao ni chini kwakweli huwa wanapata tabu sana wanapokutana na hii taasisi.

  Watanzania tusubiri tujionee maajabu ya jinsi watuhumiwa watakavyosafishwa na takukuru, wengi tutaishia kuambiwa hakuna ushahidi.
   
 18. M

  Mzazi Mtata New Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna tofauti kati ya 'Investigation' na 'Auditing' hebu tusaidiane ili tujadili vizuri mada hii!!!!
   
 19. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  TAKUKURU ndo utumbo gani ktk nchi hii ni kitengo ambacho kazi yake haipishani na toilet paper.wanakula pesa za nchi bure tu mishahara yao bora wapewe madaktari na walimu ambao tunaona kweli wanaisaidia jamii kuliko kulea uvundo wa mafisadi.eti institution lol
   
Loading...