Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,650
- 6,088
Jana nilipozungumza na baadhi ya Vyombo vya habari vilivyotaka kupata kauli ya chama juu ya upotoshaji uliokuwa umeenea jana ukitokana na barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyokuwa imenukuliwa kwenye Vyombo vya habari kadhaa, niliwajibu kwa kifupi kuwa chama kitatoa kauli baada ya kuwa kimefuatilia kwa kina correspondences hizo zilizotajwa au kudaiwa kuwa ni za msajili.
Waandishi waliopata kauli hiyo ya jana wengi ni wale tuliokutana nao wakati Kiongozi wa UKAWA, Freeman Mbowe alipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, kwenye ofisi ya msajili, kuzungumza juu ya mstakabali wa mchakato muhimu na nyeti wa Katiba Mpya.
Ilikuwa ni baada ya wito wa Msajili Jaji Mutungi aliyeomba akutane na Kiongozi wa UKAWA ili kupata msimamo wa umoja huo kwa sababu Bunge Maalum la Katiba linapaswa kuanza vikao vyake mwezi mmoja ujao huku mchakato ukiwa bado uko shakani kutokana na kukosekana kwa ushiriki wa UKAWA.
Kama nilivyowaambia waandishi hao kuwa kauli ya chama itatolewa baada ya kujiridhisha na kufanya crosschecking kwenye mambo kadhaa kuhusu correspondences hizo, leo chama kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, John Mnyika kitatoa ufafanuzi juu ya upotoshaji huo ambao leo pia umeendelezwa kwa namna nyingine na Ofisi ya Msajili, kupitia kwa Naibu Msajili.
Watanzania kwa ujumla na hususan wanachama, wapenzi, mashabiki, wafuasi na makamanda wa CHADEMA ndani na nje ya nchi wasisahau kuwa siku zote CHADEMA imesema kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani, inapigania ukombozi/ uhuru wa pili wa Watanzania.
Hatuwezi kuwa na uhuru utakaoweza kuwa fursa ya kupata au kujitafutia maendeleo, iwapo taasisi kama hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa haziko huru na KUWAJIBIKA kwa uwazi na uadilifu kwa wananchi badala ya kufuata maagizo ya chama tawala.
Ni Msajili huyu huyu aliyenukuliwa leo ambaye alitumwa na kutumiwa na CCM kutetea ujambazi, uhalifu na ugaidi wa Green Guard wakati wa mjadala wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa hasa baada ya CC ya CHADEMA kupitisha maamuzi kuwa chama kitaanza kutoa mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake, kama Katiba inavyosema, ili kulinda mali, viongozi na rasilimali za chama.
Ni Msajili huyu pasi na haya wala mishipa ya soni kumshtuka, alikubali kutumwa na kutumika na CCM kwenda kutetea Green Guard lakini akipinga vyama vingine kama CHADEMA na CUF kujilinda dhidi ya mashambulizi ya vijana wa CCM na wakati mwingine kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi.
Bila shaka tunao wajibu wa kuisaidia Ofisi ya Msajili iendane na hadhi ya kuongozwa na mtu mwanasheria mwenye hadhi ya Jaji.
Ofisi yenye hadhi ya namna hiyo haipaswi kuingizwa kwenye such disgraceful shows zilizoanza kwa kupokea maandamano ya watu asiowajua.
Majuzi DCR Mnyika alipofanya press conference mjini Dodoma kuweka hoja cha chama dhidi ya viroja vilivyoibuliwa na kundi la watu wanaojiita wanaCHADEMA huku wakizungumza lugha na maneno ya Nape na Kinana, alisema move hii inajulikana na itaendelea kujitokeza kwa sura tofauti tofauti kama ilivyopikwa jana na leo
Stay tuned...
Makene.