Chama kitatoa kauli upotoshaji wa Msajili wa Vyama

Chama kitatoa kauli upotoshaji wa Msajili wa Vyama

Kwani chama cha kisiasa mpo nyinyi tu chadema kama wapinzani??

Kwanini kila siku hamuish kulalama mbona wenzenu wapo kimya na mambo yao hatuskii fujo wala migogoro??

Hakuna mwenye haja ya matamko.

Ukweli unaotakiwa ni kwamba kikao gani halali kilikaa na kubariki kunyofoa kipengele cha ukomo wa madaraka??

Wenzenu wote washafanya chaguz zao nyinyi mtaukumbatia huo uungu mtu hadi lini.

Hamuwez kuwa mbadala wa ccm kama nyinyi wenyewe demokrasia imewashinda

Mkuu wewe si upo ACT, CDM inakuhusu nini,kma sio umbeya tu mwanamme mzima duh, gesi imekutoa akili nini?
 
Pia Msajili pia aangalie yafuatayo:-
- Uchaguzi Chadema unafanyika
- Viongozi (Mbowe na Slaa) waliojikopesha ruzuku walizirudisha
- Mahesabu ya Chadema yanakaguliwa
- Wabunge wa viti maalumu wasichaguliwe kwa udugu[/

Na sisi kama chademA tunataka ccm wafanye yafuatayo

1)sehemu ambako wananchimba dhahabu hususan geita,tarime hawana Maji safi na salama
2)waache kuhubiri siasa za udini ,ukabila,ukanda ,
3)kutoa kanga na tisheti feki za wakti Wa uchaguzi tntka origino
4)kujenga vyuo vikuu vya serikli kanda zote siyo Dar pekee
5)kuacha kutumia mashee,mapadri,wachungaji,mapasta na maaskofu kutishia chadema
6)kutoweka mapandikizi kuvuruga vyamA
 
Lini bosi, maana barua ipo mezani kwa Katbu mkuu muda sasa.... Hamkujipanga wakati huo mpaka litokee kwenye vyomo vya habari...
 
Mkuu wewe si upo ACT, CDM inakuhusu nini,kma sio umbeya tu mwanamme mzima duh, gesi imekutoa akili nini?

Mkuu upo sahihi sana, kwa siasa za Tz za kanga pashkuna mtu anatoka ACT alishahama Chadema Mwigamba anakuja kuhoji katiba ya CDM kwa Msajili anasikilizwa ni bora na CDM sasa ianze kujibu mapigo yale yale kwa kuangalia na kufuatilia kila kitu kama kweli CCM wanafuata katiba yao na kumtaarifu Msajili halafu tuona reaction yake kwa CCM.
 
Jana nilipozungumza na baadhi ya Vyombo vya habari vilivyotaka kupata kauli ya chama juu ya upotoshaji uliokuwa umeenea jana ukitokana na barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa iliyokuwa imenukuliwa kwenye Vyombo vya habari kadhaa, niliwajibu kwa kifupi kuwa chama kitatoa kauli baada ya kuwa kimefuatilia kwa kina correspondences hizo zilizotajwa au kudaiwa kuwa ni za msajili.

Waandishi waliopata kauli hiyo ya jana wengi ni wale tuliokutana nao wakati Kiongozi wa UKAWA, Freeman Mbowe alipokutana na Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, kwenye ofisi ya msajili, kuzungumza juu ya mstakabali wa mchakato muhimu na nyeti wa Katiba Mpya.

Ilikuwa ni baada ya wito wa Msajili Jaji Mutungi aliyeomba akutane na Kiongozi wa UKAWA ili kupata msimamo wa umoja huo kwa sababu Bunge Maalum la Katiba linapaswa kuanza vikao vyake mwezi mmoja ujao huku mchakato ukiwa bado uko shakani kutokana na kukosekana kwa ushiriki wa UKAWA.

Kama nilivyowaambia waandishi hao kuwa kauli ya chama itatolewa baada ya kujiridhisha na kufanya crosschecking kwenye mambo kadhaa kuhusu correspondences hizo, leo chama kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano, John Mnyika kitatoa ufafanuzi juu ya upotoshaji huo ambao leo pia umeendelezwa kwa namna nyingine na Ofisi ya Msajili, kupitia kwa Naibu Msajili.

Watanzania kwa ujumla na hususan wanachama, wapenzi, mashabiki, wafuasi na makamanda wa CHADEMA ndani na nje ya nchi wasisahau kuwa siku zote CHADEMA imesema kwa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani, inapigania ukombozi/ uhuru wa pili wa Watanzania.

Hatuwezi kuwa na uhuru utakaoweza kuwa fursa ya kupata au kujitafutia maendeleo, iwapo taasisi kama hii ya Msajili wa Vyama vya Siasa haziko huru na KUWAJIBIKA kwa uwazi na uadilifu kwa wananchi badala ya kufuata maagizo ya chama tawala.

Ni Msajili huyu huyu aliyenukuliwa leo ambaye alitumwa na kutumiwa na CCM kutetea ujambazi, uhalifu na ugaidi wa Green Guard wakati wa mjadala wa vikundi vya ulinzi ndani ya vyama vya siasa hasa baada ya CC ya CHADEMA kupitisha maamuzi kuwa chama kitaanza kutoa mafunzo ya ukakamavu kwa vijana wake, kama Katiba inavyosema, ili kulinda mali, viongozi na rasilimali za chama.

Ni Msajili huyu pasi na haya wala mishipa ya soni kumshtuka, alikubali kutumwa na kutumika na CCM kwenda kutetea Green Guard lakini akipinga vyama vingine kama CHADEMA na CUF kujilinda dhidi ya mashambulizi ya vijana wa CCM na wakati mwingine kwa kushirikiana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi.

Bila shaka tunao wajibu wa kuisaidia Ofisi ya Msajili iendane na hadhi ya kuongozwa na mtu mwanasheria mwenye hadhi ya Jaji.

Ofisi yenye hadhi ya namna hiyo haipaswi kuingizwa kwenye such disgraceful shows zilizoanza kwa kupokea maandamano ya watu asiowajua.

Majuzi DCR Mnyika alipofanya press conference mjini Dodoma kuweka hoja cha chama dhidi ya viroja vilivyoibuliwa na kundi la watu wanaojiita wanaCHADEMA huku wakizungumza lugha na maneno ya Nape na Kinana, alisema move hii inajulikana na itaendelea kujitokeza kwa sura tofauti tofauti kama ilivyopikwa jana na leo

Stay tuned...

Makene.

Hivi wewe Makene na wenzio hapo makao makuu mmegundua kuwa toka Kinana aingie pale Lumumba mmekuwa on the defensive? Bado hamjakubali kuwa mmeshindwa mbinu na inabidi mjitazame mara mbili kama kweli mna uwezo wa kuongoza mapambano?si lazima kufukuza watu kama mnavyofanya, mnaweza kuwapumzisha waliokuwepo kwa muda mrefu. hata Makamba CCM walimheshimu, lakini CDM mlivyokaza uzi na kelele za Ufisadi na yeye kung'ang'ania wimbo ule ule magwiji wa CCM wakamtosa. Kufanya Uchaguzi CDM sasa hivi sio tena OPTION ni necesiyt ya nyie kusurvive. cha kufanya muufanye uchaguzi uwe katika hali ya kuzima mashanmbulizi yote. Naamini Mbowe na Slaa wakisimama kama wagombea watapata kura za kutosha, kwani Slaa huyu juzi juzi amepigiwa kura na watanzania milioni kadhaa, hawezi kosa kura mamia kuwa katobu mkuu asiye na qn mark hapo CDM. Mbowe ni vizuri akaachia ngazi kuondoa fikra hasi juu ya chama chenu. Hii hadithi ya ukanda kwa CDM imekuwa kama wakati ule mnatamba na UFISADI, kila kitu ilikuwa ukisema ufisadi unashinda hoja, sasa soundbite hiyo haina tija tena, kwani jamii ya watanzania sasa hadi fundi viatu naye ana aina flani ya ufisadi, na jamii imekubali kila mtu kuwa mwizi wa sehemu aliyokuwepo( sad, but true fact).

Kwa tunaotizama mambo kwa jicho la pembeni, Ukanda wa CDM unakuzwa kadri iwezekanavyo na maadui zenu, na nyie kwa kukosa mbinu mbadala mnawasupport(bila kujijua). hizi hadithi za kuchokonoa hao wajumbe feki sijui zinaifanya hii hadithi ya jamaa hao izidi kupata free airtime, wakati mngekaa kimya au kuchagua counter move hili lingekwisha.

Mlipewa break nzuri sana ya kufanya re-organisation wihtin CDM kupitia bunge la Katiba, hamjaitumia nafasi hiyo, sasa bunge hili likipita maadui zenu focus yao yote itahamia kwenye kuwadhoofisha zaidi,worse enough mnawaachia wafanye hivyo, ama kwa kutokujua au kwa kutokuwa na njia za kuwazuia.
 
Last edited by a moderator:
Lumumba buku saba tulieni Msajili ni TV na nyie ni remote kwahiyo mnamtumia mnavyotaka lakini kwa tarifa mtashindana sana lakini hamtashinda lazima tutawanyoa tu
 
Kinana, hahahahahahahah. huyu mwizi wa mashine za kufulia.
Hivi wewe Makene na wenzio hapo makao makuu mmegundua kuwa toka Kinana aingie pale Lumumba mmekuwa on the defensive? Bado hamjakubali kuwa mmeshindwa mbinu na inabidi mjitazame mara mbili kama kweli mna uwezo wa kuongoza mapambano?si lazima kufukuza watu kama mnavyofanya, mnaweza kuwapumzisha waliokuwepo kwa muda mrefu. hata Makamba CCM walimheshimu, lakini CDM mlivyokaza uzi na kelele za Ufisadi na yeye kung'ang'ania wimbo ule ule magwiji wa CCM wakamtosa. Kufanya Uchaguzi CDM sasa hivi sio tena OPTION ni necesiyt ya nyie kusurvive. cha kufanya muufanye uchaguzi uwe katika hali ya kuzima mashanmbulizi yote. Naamini Mbowe na Slaa wakisimama kama wagombea watapata kura za kutosha, kwani Slaa huyu juzi juzi amepigiwa kura na watanzania milioni kadhaa, hawezi kosa kura mamia kuwa katobu mkuu asiye na qn mark hapo CDM. Mbowe ni vizuri akaachia ngazi kuondoa fikra hasi juu ya chama chenu. Hii hadithi ya ukanda kwa CDM imekuwa kama wakati ule mnatamba na UFISADI, kila kitu ilikuwa ukisema ufisadi unashinda hoja, sasa soundbite hiyo haina tija tena, kwani jamii ya watanzania sasa hadi fundi viatu naye ana aina flani ya ufisadi, na jamii imekubali kila mtu kuwa mwizi wa sehemu aliyokuwepo( sad, but true fact).

Kwa tunaotizama mambo kwa jicho la pembeni, Ukanda wa CDM unakuzwa kadri iwezekanavyo na maadui zenu, na nyie kwa kukosa mbinu mbadala mnawasupport(bila kujijua). hizi hadithi za kuchokonoa hao wajumbe feki sijui zinaifanya hii hadithi ya jamaa hao izidi kupata free airtime, wakati mngekaa kimya au kuchagua counter move hili lingekwisha.

Mlipewa break nzuri sana ya kufanya re-organisation wihtin CDM kupitia bunge la Katiba, hamjaitumia nafasi hiyo, sasa bunge hili likipita maadui zenu focus yao yote itahamia kwenye kuwadhoofisha zaidi,worse enough mnawaachia wafanye hivyo, ama kwa kutokujua au kwa kutokuwa na njia za kuwazuia.
 
Hilo sijui lutakuwa tamko la ngapi

Waache watachoka kama yule tulie kuwa tuna muona kila mwisho wa mwezi ktk tv zote nchini ila tangu mwaka huu mmmhhhh hasikiki...... mbaya zaidi alivyoaanza akataka apigiwe simu live akiwa tbcaaaa wapi alifanya mara moja tuuu wakamtonya, mzee acha hizo utaumbuka kuna wehu kule chadema

Hebu iteni baraza kuu murekebishe hvyo vipengele mambo yaendelee cdm wakifanya mikutano,wakitoa maandiko haisaidii Cdm wasivunje sheria wafate sheria waitshe baraza kuu warekebishe mambo yaende
 
Matamko hayawasaidii tekelezeni maagizo ya Masajili atakifuta chama!

Mara ya mwisho kauli kama hii niliisikia kwa msajiri wa vyama mstaafu Judge John Tendwa kwamba ataifuta CDM kwenye daftari lake la usajiri wa vyama vya siasa. Masikini kabla ya kutekeleza hilo yakamkuta yale yaliyomkuta Sheikh Yahya Hussein Japa yeye Tendwa bado yuko hai, ila sasa anavuna aibu mitaani.
 
Teh teh teh

Matamko kila siku.

Wachaga bana wanataka wakifanye hiko chama kuwa cha ukoo sasa huku wanafanya demokrasia magilini.

Ha ha ha.
Nafikiri na wewe una matatizo, hivi ni lazima useme uchagga katika mawasilisho yako? Hii inaonesha kana kwamba Tanzania tunaongoza kwa ukabila au unaupalilia? Nafikiri unahitaji kuondokana na dhana hii ya kufikiria kuna makabila hayatakuwa kuwa katika siasa. Zaidi wakati mwingine unaweka na udini!!
 
Back
Top Bottom