Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community

Hizi jumuiya ni za kuandaa party tuu na wengine kuzitumia kama NGO kuweka mambo yao sawa,sioni ubaya wowote kuzianzisha lakini hazina maana sana,wabongo nawashauri nunueni life insurance kuliko kutegemea michango matatizo yakiwakuta...matatizo yakikukuta ni insurance yako na ndugu/marafiki wa karibu ndio watakusaidia lakini sio hivi vyama.
 
- Ahsante mkuu mawazo mazito sana haya tutayafanyia kazi kwenye kikao maalum cha kutafakati mawaidha, karibu sana endelea kutupa nasaha zako nzito sana kama hizi.

Ahsante.

William.
 
KJ ru serious?Unaweza kutuhabarisha ilikuwa vipi?Mkuu Malecela vipi kuhusu huo ukabila,bado upo ama nao umebarikiwa mkuu?
Chama kilishindikana kwa vile watu walianza kujipanga kikabila. Baadhi yao naona ndio hao hao walioombwa ushauri. Nina uhakika Malecela anayafahamu haya vizuri sana.

Sasa wanapoanza kujipanga tena kiubalozi na kuomba ruhusa kwa balozi, si tunarudi tena kule kule ingawa sasa sio ukabila bali ni ni uCCM/TZ-Gov?
 
- Mwenyekiti wa muda Khaji ni anatokea visiwani, mimi ninatokea Dodoma, katibu mkuu anatokea Kigoma, katika viongozi wote wa muda tulionao hakuna mfanyakazi wa ubalozi wowote uwe wa nchi au nyumba kumi kumi na wala hakuna influence ya yoyote kutoka anywhere, unless kama unawafahamu unaweza kuwasema kwa majina yao ili tuweze kujiangalia ndani ya chama chetu kama wapo bila sisi wenyewe kujua. Ya chama cha zamani hayatuhusu sisi tunajali chama cha sasa.

Ahsante Sana.

William.CO

Malecela,
Sijasema kuwa mmejipanga kikabila ila nafikiri mnafahamu jinsi ukabila ulivyoathiri uundwaji wa chama hapo awali.

Nililosisitiza toka awali ni kuwa hivi sasa hiyo interim team yenu ina harufu ya ukaribu sana na balozi/serikali na ndio maana mkaanzia huko kuomba baraka. Kwa nini msiondoe wote wenye ukaribu na walio ubalozini ili chama kuwa huru kweli kweli?
 
- Mkuu maneno mazito sana haya, sasa vipi ukitoa ushahidi kwamba chama kina watu wa ubalozi ukiwataja wka majina utasaidia sana, na kama huna ushahidi ni vyema ukaomba radhi kwa kuwa mzushi!

Respect.

FMEs!
Mkuu FMEs,
Mbona unataka kujifanya huwajui au unataka umpatie Mod kibarua?

Kama nia ni kuunda chama kwa ajili ya kuwa jumuisha waTanzania, basi hakuna haja ya kuumbuana na kuvuana nguo mitandaoni ila ni muhimu kukosoana.
 
Malecela,
Sijasema kuwa mmejipanga kikabila ila nafikiri mnafahamu jinsi ukabila ulivyoathiri uundwaji wa chama hapo awali.

Nililosisitiza toka awali ni kuwa hivi sasa hiyo interim team yenu ina harufu ya ukaribu sana na balozi/serikali na ndio maana mkaanzia huko kuomba baraka. Kwa nini msiondoe wote wenye ukaribu na walio ubalozini ili chama kuwa huru kweli kweli?

- Sasa mkuu naomba uwataje wenye harufu na ubalozi ili tujiajngalie kama ni kweli, ninakuruhusu uwataje hao unaodhani wana harufu ya ubalozi.

William.
 
Mkuu FMEs,
Mbona unataka kujifanya huwajui au unataka umpatie Mod kibarua?

Kama nia ni kuunda chama kwa ajili ya kuwa jumuisha waTanzania, basi hakuna haja ya kuumbuana na kuvuana nguo mitandaoni ila ni muhimu kukosoana.

- Mkuu acha majungu huwasaidii wananchi wengi wanaotaka kwua na hii jumuiya, haya yako ni majungu hao wamekwedna ubalozini kama walivyokuja hapa kama wanavyosema, sasa haina maana hiki chama kitakwua cha JF simply huna hoja kama unayo ungetaja acha uzushi mkuu.

FMEs
 
Ndugu Malecela, objective hasa ni nini? kuwaunganisha tu? then what next? lazima kuna vision unayo, je unaweza kuiweka hapa mkuu?
 
Unapokuwa unaweka mawazo yako kwenye hii forum ili yaweza kujadiliwa you mus be very careful, maana Umesema mnataka kuanzaisha chama, je ni chama cha siasa au cha jamii kuwaunganisha watanzania huko?
Mmmepata baraka za Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa NY,it doesn't make sense at all, ni kwa sababu gani hamjaanzia kwa balozi wa Tanzania Marekani??
Kama siyo chama cha siasa bali ni chama cha kuwaunganisha watanzania walioko Marekani, mmechelewa sana, ingetakiwa kuwa kipo since 1980's.
All the best
 
Wazo zuri la kuunda jumuiya ya watanzania. Muongee pia na jumuia za watanzania wa sehemu nyingine kwa ushauri zaidi, kwa mfano New England kuna jumuia ambayo ilianzishwa kama a social organization kuwakutanisha watanzania kila summer kwa kufanya barbeque na sports (soccer matches/ volley ball). Watu tunaoishi New England hatuna ulazima wakuwa wanachama ili tushiriki katika summer events. Watu wengi hutoa michango kufanikisha hiyo siku. NewEngladUmoja ina zaidi ya miaka 5. here's their website http://www.newenglandumoja.net/ Texas, Atlanta na Ohio pia wanajumuia ambazo zina muda mrefu kidogo itakuwa vizuri kama utawatafuta viongozi wa hizo jumuiya ili kubadilishana mawazo. Nawatakia kila la kheri.
 
hizi jumuiya kazi zao kubwa ni kuchoma nyama na hiki nadhani kinaandaliwa kwa ajili ya kuchoma nyama manake joto linaanza soon.

ukiwapa mawazo ya maana huwa hawapendi na watu wengi hawashiriki kwa vile wanajua historia ya hizi jumuiya.

jumuiya ni kitu kizuri sana nchi za nje kama kitaendeshwa kisheria na kila mwanachama atakuwa na nguvu.jumuiya nyingi zinaendeshwa kimzaa mzaa na matokeo yake hazileti faida yoyote kwa wananchi waliokuwa nje kwani kikubwa kama nilichosema huishia kuchoma nyama wakati kuna mambo mengi sana vyama hivi vingeweza kufanya vyenye faida zaidi kwa wanachama wao.

kila la kheri jumuiya mpya na ingekuwa vizuri mueke tofauti yenu kubwa na jumuiya ya mwanzo hau haikuwepo?
 
Back
Top Bottom