Chama Kipya: New York Metropolitan Tanzanians Community

William, umenipa mtihani mgumu. Lakini nitajaribu niwezavyo kukujibu baada ya kuawasiliana na vyanzo vyangu vya habari hapo New York na kwingineko.
 
hivi W Malecela na FMES sauti ya umeme wana uhusiano gani?
huu mjadala na ule mjadala wa baba mtu na Sofia Simba naona kama wana fanana.

Anyway hawa ndio waliotufikisha hapa tulipo, ni bora kuwapuuuza, hawana cha uzalendo wala nini. wanachumia matumbo yao tu.

- Mjadala ni kuhusu chama sio FMES, kama unatka kunijadili mimi fungua thread inayonihusu, hapa ninaamini kinajadiliwa chama. Sijakufikisha popote ni wewe mwenyewe ndiye umejifkisha ulipo, hii tabia ya kusingizia wengine tuache na mimi kama binadam nina matatizo yangu mengi sana simlaumu mtu!

Es!
 
William, umenipa mtihani mgumu. Lakini nitajaribu niwezavyo kukujibu baada ya kuawasiliana na vyanzo vyangu vya habari hapo New York na kwingineko.

- Ungetumia hivyo vyanzo vyako kutusaidia ushauri wa kuimarisha chama, badala ya kunijadili mimi katika huu mjadala, labda ufugnue mjadala mpya unaonihusu kama ni muhimu sana, ila kuishi huko uliko na kuleta majungu kutoka kwenye vyanzo inasikitisha sana, nilitegemea ungekubali na kuomba radhi kwa kuleta majungu na uzushi, I mean how low can it get na mtumzima kama wewe kujivua nguo mbele ya public?

- Hivyo vyanzo vyako wananifahamu au wananisikia, eti mimi ninajipendekeza kwa mtu mwingine hilo neno kwangu halipo, ninasema hivi katika maisha yangu neno kujipendekeza halipo wala sielewi maana yake, ungeuliza wanaonijua vizuri wakusaidie, na ungekua mstaarabu ungeachana na hivyo vyanzo ambavyo tayari vimekupelekea kujivua nguo hapa na maneno ya majungu na uzushi na uongo wa mchana.

- Jaribu kutupa ushauri wa chama maana uwezo unao, kama unataka kunijadili mimi fungua thread inayonihusu please.

Ahsante.

William.CO.
 
- Mjadala ni kuhusu chama sio FMES, kama unatka kunijadili mimi fungua thread inayonihusu, hapa ninaamini kinajadiliwa chama. Sijakufikisha popote ni wewe mwenyewe ndiye umejifkisha ulipo, hii tabia ya kusingizia wengine tuache na mimi kama binadam nina matatizo yangu mengi sana simlaumu mtu!

Es!

Nyie na mafisadi wenzio CCM ndio mmetufikisha hapa tulipo sasa mnajifanya mnajua kuongoza, mnataka kutuongoza hadi kwenye nchi za watu.

Hata aibu hamuoni.
 
William, mosi, naomba sana usiite, 'Mkuu" wala Esteemed Reader'! Sitaki. Niite, Estmeed Reader. Napenda!

Pili, naomba nianze na mchango wangu kwa machache ya kufanikisha kutunga mimba, kuzaliwa na kulea chama hicho hadi kikue hapo New York and its environs, kama ifuatavyo:

(a) Ni wazo zuri la kuwa na Chama cha Watanzania wa New York na vitongoji vyake, kama ilivyo sehemu nyinginezo za Amerika, kwa mfano, huko Houston, Texas. Lakini baadhi yenu mnaokiandaa inafaa sana kung'atuka kuwaoganize hao wa-Tanzania wa New York. Watanzania wa sasa (na hao wa New York) sio mabwege wa kuburuzwa buruzwa!
(b) Wengine acheni agenda zenu za kufanikisha maslahi yenu ya binafssi kuliko mustakabali wa Watanzania, kwa ujumla, hapo New York. Kusema kweli, New York ilikuwa ni ya pili kwa na idadi kubwa ya Watanzania (ya kwanza ilikuwa ni Washington, DC) huko Amerika. Lakini NY haijafanikiwa kuwa na Umoja wa jumuiya hiyo. Inapitwa na sehemu nyinginezo chipukizi.
(c) Tanzania ina ofisi mbili za u-Balozi: Washington, DC - ambayo inawakilisha raia wa Watanzania; na New York – ambayo inwakilisha serikali/taifa ya/la Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa. Zamani ofisi ya New York ilikuwa pia ikitekelza shughuli za diplomatic protocal, kwa mfano, maelezo/habari, utalii na pasipoti. Lakini serikali ya Amerika ilikataa kuwa hizo si shughuli za Umoja wa Mataifa; zinahuzu consular relationships. Kwahiyo, shughuli za ki-consulate ziliamishiwa kwenye ofisi husika ya Washington, DC. Ukweli ni kwamba ninyi wa NY mko chini ya himaya ya Balozi wetu aliyeko Washington, DC.
(d) Hayo ya kuomba "blessings" eti kutoka kwa ma-Balozi (New York na Washington) yatakinyima "Chama-tegemewa" hadhi yake na mwelekeo wake. Je, endapo Balozi yeyote hatatoa "blessing" si ni kujitakia mgawanyiko na uchonganishi kati ya ofisi zetu hizo mbili huko Amerika?
(e) "Chama-tegemewa" kisiwe an affiliate ya serikali au chama chochote cha siasa! Chama-tegemewa" kiwe huru kukosoa mabaya ya Tanzania.
(f) Hata wakati wa ufunguzi, msimwalike Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa awe mgeni rasmi. Mwalikeni Balozi wa Washington, DC, ambaye kama atapenda, ndiye amwombe Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa kumwakilisha (sisemi kuwa msimkaribishe Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa kwenye ufunguzi).
(g) Jifunzeni kwa vyama vya nchi nyingizo za jirani, hususan Uganda!

Tatu, William, umenikuu mengi. Nimejibu baadhi tu, kama ifuatavyo. Wasomaji, huenda kuna makosa ya ki-uandishi; mnisamehe:

  • (N)ilipofika (mimi William) hakukuwa na Social life nikaanza kupiga Disco kwenye Club yaani mziiki ya ki-Africa, na pole pole nikaanza kupiga Muziki kwenye party za wananchi, sikujibatiza jina kwa hizo sababu unazozisema huo ni uzushi tena wa mchana, nimejipa hilo jina kutokana na shuguli nyingi sana nilizowahi kushiriki NY either kama mjumbe wa kamati au kiongozi wa kamati, au sometimes on my own.

Jibu: Una maana gani ya social life? Una ukweli wowote kuwa social life haikuwepo? Mbona vinazo vyangu (ambavyo sitavitoa nje) vinasema kuwa kabla wewe hujaja NY, New York ilikuwa "vibrant". Watanzania walikaribishana majumbani kwao. Kwahiyo, watu walikuwa na social life wakialikana majumbani mwao!

Na kila wakaribishanapo, hawakuhitaji mtu wa kuwapigia disko. Karibu kila nyumba ilijitosheleza kwa muziki, na kwamba wenye kupenda kuja na albums walikaribishwa kufanya hivyo. Mambo yalibadilika baada ya Balozi Rupia kuondoka.

Likaja wimbi la "vijana", kama nilivyoeleza. Baadhi ya "vijana wa vigogo" wakajifanya ndio wajuzi wa muziki wa Disko na kwanza kupiga kwenye hafla za urely mwenye nyuma. Na hapo baadaye, kwanza kupangisha nafasi kwenye mabaa na mahala penginepo kupiga muziki, ki-biashara, sio ki-social (kama klabu).

Je, kwako social life ni kucheza dansi tu?

  • Kwa mfano katika shughuli ya kumuaga Balozi Mwakawago alipokua anaondoka, nilishiriki kama mjumbe wa kamati nilichangisha hela zote zilizotakwia na kamati kwa ajili ya sherehe sherehe zilifanyika na zilifana sana infact tulialika karibu mabalozi 20 kutoka Africa walikuja pale New Rochelle…

Jibu: Ni nani aliyeanzisha wazo la kumuaga Balozi Mwakawago alipokua anaondoka? Je, unaweza kutuorodheshea majina ya wanakamati? Mlialika mabalozi 20 kutoka Afrika! Je, walifika wangapi? Sidhani kama kweli hao mabalozi walifika wote!

Na huyo Field Marshall ES (ambaye inaonekana kuwa si mgeni hapa) aliyeweka tangazo na kusaini Professor ni mmojawapo wa wanakamati ya kumuaga Balozi Mwakawago?

  • Wakati wote huu nilikuwa na tabia ya every Summer kukodisha ukumbi kwa hela zangu na kupigisha Disco kubwa sana la Waa-Africa na hasa Wa-Tanzania, nimeifanya hii shuguli kwa muda mrefu sana, bila ya ubalozi wala mke wangu kuwepo huko.

Jibu: Hayo ya kupiga madisko huko NY hayana uhusiano na wewe kujidai kuwa Community Organiser…hiyo ilikuwa ni biashara binafsi. Ili kuwapata wateja wa kuja kunengua viuno ilibidi uanzishe makakati wa k-biashara ni mere business strategy!

  • Kabla sijaoa nyumba yangu ilikuwa ni nyumba ya wageni wote wasio na pa kwenda au pa kulala, nimewasaidia vijana wengi sana waliokwua wamekwama NY, sometimes hata wazee, haya niliyafanya bila ubalozi wala mkewangu kuwepo huko...(ikiwa ni pamoja na kumsaidia sana ) Dada Pengo marehemu…

Jibu: Huenda, kulikuwa na sababu ya kufanya hivyo! Bye the way, huyo marehemu Dada Pengo alikuwa anatokea sehemu gani ya Tanzania?

  • Last Summer mimi na vijana wengine tulishirikiana kufanyisha sherehe kubwa kule Park ambayo iliwaleta wananchi karibu 400 ubalozi haukuwemo wala mke wangu. Kabla Summer haijaisha Ubalozi ulinomba kushirkiana nao kufanya sherhe nzito pale nyumbani kwa Balozi kama kawaida wananchi karibu 300 walishikiriki.
Jibu: Ni nani alikuwa progenitor wa wazo hilo la kufanya sherehe kubwa kule Park? Vijana wengine hao ni akina nani?

  • Majuzi nimeshiriki kwenye kamati kama mjumbe kwenye msiba wa Balozi Mwakawago, sasa hayo yote niliyoyasema hapo juu niliamua kujiita Community Organizer kwa sababu ndiyo hasa kazi aliyoifanya Obama kabla ya kuingia kwenye siasa za taifa, nimeanza hizi shuguli za Community toka nikiwa Shule ya Secondari ambako siku zote nikikuwa kinara wa Sherehe na safari za Picnic na nilikua ninapiga disco ziku zote kwa ajili ya wanafunzi, nilipoenda JKT kama kawaida nilikwua Oljoro nako nilikuwa kinara wa hizi shughuli za social, nilipoenda Vyuoni nilikuwa kama sasa yaani na hizi shughuli za social, nilipoenda Belgium kama akwaida wananchi niliosoma nao pale kina Mollel aliyekua Manager wa Ralways TRC, watakueleza kama kawaida nilikuwa ninaongoza hizi shuguli za sheerhe na kuwakutanisha wananchi.

Jibu: Hiyo kamati iliundwaje? Ni akina nani waliokuwa wajumbe wake na walichaguliwaje? Hayo ya kuongoza hizi shuguli za sheerhe na kuwakutanisha wananchi, pengine ni kwa sababu ya uwezo wako wa kuwa na vifaa vya muziki!

Mimi nisema "Sasa Melecela amejibatiza jina la Community Organiser..." Na wewe ukatamka, …" sikujibatiza jina kwa hizo sababu unazozisema huo ni uzushi tena wa mchana, nimejipa hilo jina kutokana na shuguli nyingi sana nilizowahi kushiriki NY either kama mjumbe wa kamati au kiongozi wa kamati, au sometimes on my own."

So what! Ulikuwa wapi kujipa jina hilo...hadi baada ya BO? Acha kufananisha shughuli zako na hizo za alizokuwa akifanya BO! Ama unataka nazo zikusaidie kwenye cv yako, ki-siasa?

  • Bash La Mwaka NYC: Wakulu Tukutane Huko W. J. Malecela 2nd June 2009, 02:05 AM: Ndugu zangu wote JF, salaaam kwa wote ninaomba kuwafahamisha kwamba kwa kushirikiana na wananchi wengine kama kumi hivi, tunatayarisha bash kabambe la mwaka litakalo fanyika huko NYC, kwa maajaliwa ya Mungu itakuwa tarehe 27, June 2009.
Jibu: Tarehe ni tofauti. Mimi nilitaja tangazo lifuatalo: "Tangazo: Bash la Balozi NYC Haya Tukutane Wakuu! W. J. Malecela 11th August 2009, 03:10 AM: Wakulu wote JF, na wananchi wenzangu wote mnaoishi US na hata nje, na hasa New York City na vitongoji vyake..."

Mwisho, nawaachia wengine nao wachangie kwa matumaini makubwa kwamba "chama" kina blessings zangu (as if ninanzo) – cheka!
 
Estmeed reader,

nimecheka, na asante sana kwa mchango wako. Natia shaka hiki chama, na ushiriki, hasa wa huyo FMES.
Chama cha jamii kinaanzishwa na wanajamii.

Unless muhtasari wa kikao cha kwanza kilichozaa wazo hili ukawekwa hapa ili kuondoa wingu la lengo halisi la kuanzishwa kwa chama hiki. Sina haja ya kutoa mawazo ya kusaidia kuimarisha chama kwa manufaa ya mtu binafsi.

Kama mtu anaweza kujiita 'community organiser' bila kutaja kikao gani cha community kilikaa kumchagua, na kwamba kama ana wasaidizi mbona hawajawahi kujitokeza kusupport wazo lake (sijui kuhusu Balatanda - hajadeclare).

Hizo 'shughuli' za community ambazo jamaa 'amefanikisha akishirikiana na vijana wenzie' ambao wanaremain kuwa anaonymous pia ziatia mashaka.

Kuna mtu ni haambiliki fulani hivi na akitaka lake lazima liwe, by hooks and crooks. Waliochangia hii thread concretely ni wewe na KJ. Mchango yenu itachukuliwa kama hila au chuki, na soon mtaanza kutajwaa majina yenu ikifuatiwa na allegations kibao, God fobid.
 
hivi W Malecela na FMES sauti ya umeme wana uhusiano gani?
huu mjadala na ule mjadala wa baba mtu na Sofia Simba naona kama wana fanana.

Anyway hawa ndio waliotufikisha hapa tulipo, ni bora kuwapuuuza, hawana cha uzalendo wala nini. wanachumia matumbo yao tu.

Ni mtu huyo huyo mmoja, the former ambaye anapata shida kidogo kutenganisha hizi personalities kwenye posts zake. It is so transparent it is becomiing sad
 
Serikali ishasikia NY kuna vichwa fulani ambavyo hapo baadaye vinaweza kuleta matatizo, vichwa hivi vimejaribiwa kuwekwa kwenye radar lakini vinakuwa vigumu sana kupatikana kwani vinaenda miendo ya kijasusi.

Sasa watu wamepewa kazi ya ku infiltrate network through hivi vyama.

Lakini bado wamekuta hivi vichwa ni "not reachable"
 
Mnang'ang'ania u Community Organiser kwenye nchi za watu kama hamna aibu vile kwa nini usirudi nyumbani ukauendeleza u CO wako huku nasikia kule jimbo la Mtera kuna shule moja ya sekondari kata ya Fufu ina walimu wanne tu kwa nini usije kusaidia .....hovyo....
 
Ingelikuwa vyema kama tungejadili mada hasa kwa nini William Malecela hafai kuongoza Jumuia ya Watz hapa New York!

Tutoe sababu za msingi bila kusukumwa na hoja za chuki,kimsingi kila Mtz aliye ndani au nje ya Tanzania ana haki ya kugombea nafasi aitakayo,kama William Malecela kasema yeye ni Interim leader tu na kutafanyika uchaguzi hapo baadae,si ndiyo nafasi yetu kumuondoa madarakani kwa njia ya sanduku la kura muda ukifika?

Luten,haya mambo ya kumtaka William arudi akaendeleze jimbo la Mtera ni irrerevant na hoja husika,kwani hata wewe binafsi kikatiba unaruhusiwa kwenda Mtera kuwaletea maendeleo ukitaka!

Pia hata walioleta hoja kusema kuwa likely William ndiyo FMEs nao hawamtendei haki William maana wameshindwa kuthibitisha "beyond any reasonable doubt"kuwa madai yao ni kweli tupu!

Tujadili hoja inayohusu chama hiki cha New York kwa heshima na adabu bila jazba wala matusi!

Asanteni!
 
- Anyways kesho nitaendelea kuleta agenda zingine za chama naona sasa ni wakati wa kusonga mbele na mengine, wengine wote huko ushauri wenu unaofaa tutauchukua na usiofaa hatutauchukua, ingwa ninawashukuru wote so far kwa michango yenu.

Ahsanteni Sana, Lakini by kesho nitaleta agenda zaidi za chama.

William. (Community Organizer).
 
- Mkuu nitajitahidi sana kuchukua yale ya maana tu kwa chama:-

Ni wazo zuri la kuwa na Chama cha Watanzania wa New York na vitongoji vyake, kama ilivyo sehemu nyinginezo za Amerika, kwa mfano, huko Houston, Texas.

- Sawa sawa.

Lakini baadhi yenu mnaokiandaa inafaa sana kung'atuka kuwaoganize hao wa-Tanzania wa New York. Watanzania wa sasa (na hao wa New York) sio mabwege wa kuburuzwa buruzwa!

- Tunaongoza kwa muda tu, baadaye utafanyika uchaguzi rasmi wa wanachama wote.

Ukweli ni kwamba ninyi wa NY mko chini ya himaya ya Balozi wetu aliyeko Washington, DC.

- Ndio maana Mwenyekiti wa muda akirudi tu kesho, ataenda DC kuonana na balozi wetu kule kupata baraka zake.

Hayo ya kuomba "blessings" eti kutoka kwa ma-Balozi (New York na Washington) yatakinyima "Chama-tegemewa" hadhi yake na mwelekeo wake. Je, endapo Balozi yeyote hatatoa "blessing" si ni kujitakia mgawanyiko na uchonganishi kati ya ofisi zetu hizo mbili huko Amerika?

- Sio wote walioombwa baraka wametoa, lakini wote wanajua kuwa tupo na tunaendelea na kukisimamisha chama kama tulivyopanga na kukubaliana kule Harlem.

"Chama-tegemewa" kisiwe an affiliate ya serikali au chama chochote cha siasa! Chama-tegemewa" kiwe huru kukosoa mabaya ya Tanzania.

- Soon nitaweka nia na madhumuni ya chama hapa,utaona kwamba hatuna mpango wa kujiingiza kwenye siasa za taifa lolote iwe US wala Tanzania, sio nia yetu hiyo.

Hata wakati wa ufunguzi, msimwalike Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa awe mgeni rasmi. Mwalikeni Balozi wa Washington, DC, ambaye kama atapenda, ndiye amwombe Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa kumwakilisha (sisemi kuwa msimkaribishe Balozi wetu kwenye Umoja wa Mataifa kwenye ufunguzi).

- Ushauri huu tutauzingatia sana ni mzito sana.

Mwisho, nawaachia wengine nao wachangie kwa matumaini makubwa kwamba "chama" kina blessings zangu

- Ninakushukuru sana kwa baraka zako mkuu.

Ahsante.

William. (Community Organizer).
 
Nitaangalia yaliyo muhimu tu kwa chama:-

Estmeed reader,

nimecheka, na asante sana kwa mchango wako. Natia shaka hiki chama, na ushiriki, hasa wa huyo FMES.
Chama cha jamii kinaanzishwa na wanajamii.

- So far hatuna mwanachama wala kiongozi anayeitwa FMES, kesho nikijaaliwa nitaweka majina ya viongozi wote wa muda na kamati nzima ya chama ya muda.

Unless muhtasari wa kikao cha kwanza kilichozaa wazo hili ukawekwa hapa ili kuondoa wingu la lengo halisi la kuanzishwa kwa chama hiki. Sina haja ya kutoa mawazo ya kusaidia kuimarisha chama kwa manufaa ya mtu binafsi.

- Ni chama cha jumuiya sio changu wala cha mtu yoyote ni cha jumuiya, tunaenda pole pole kwanza ilikuwa ni introduction na baadaye tutaenda kwenye mengine ila on our pace.

Kama mtu anaweza kujiita 'community organiser' bila kutaja kikao gani cha community kilikaa kumchagua, na kwamba kama ana wasaidizi mbona hawajawahi kujitokeza kusupport wazo lake (sijui kuhusu Balatanda - hajadeclare).

- Obama hakupewa hiki cheo na yoyote, so na mimi sikupewa na yoyote, inaruhusiwa kujipa mwenyewe kutokana na kzi zako kwa Community ambazo ni za kujitolea, nafikiri unakumbuka sana kwenye msiba wa mzee Chiume, hakuna aliyeniomba kujituma, maana he was my friend na nilikuwa niki-spend a lot of time karibu naye kuchota siasa na busara za maisha.

- Mkuu nimejaribu kuchukua na kujibu niliyoyaona muhimu tu, mengine hapana, halafu be careful maana huenda kuna wanaokuhusu kwenye uongozi na uanachama wa hiki chama, yaani wananchi wengine.

Ahsante
.

William. (Community Organizer)
 
Ingelikuwa vyema kama tungejadili mada hasa kwa nini William Malecela hafai kuongoza Jumuia ya Watz hapa New York!

Tutoe sababu za msingi bila kusukumwa na hoja za chuki,kimsingi kila Mtz aliye ndani au nje ya Tanzania ana haki ya kugombea nafasi aitakayo,kama William Malecela kasema yeye ni Interim leader tu na kutafanyika uchaguzi hapo baadae,si ndiyo nafasi yetu kumuondoa madarakani kwa njia ya sanduku la kura muda ukifika?

Luten,haya mambo ya kumtaka William arudi akaendeleze jimbo la Mtera ni irrerevant na hoja husika,kwani hata wewe binafsi kikatiba unaruhusiwa kwenda Mtera kuwaletea maendeleo ukitaka!

Pia hata walioleta hoja kusema kuwa likely William ndiyo FMEs nao hawamtendei haki William maana wameshindwa kuthibitisha "beyond any reasonable doubt"kuwa madai yao ni kweli tupu!

Tujadili hoja inayohusu chama hiki cha New York kwa heshima na adabu bila jazba wala matusi!

Asanteni!

- Mkuu tuko pamoja, lakini unajua mimi ni muumini mkubwa sana wa Demokrasia, yaani kutoa nafasi kwa kila mwananchi kusema maoni yake, wamesema nimeyasikia ya muhimu tu nitayapeleka kwenye chama, usiwe na wasi wasi mkuu kila kitu kiko under control, haya maji nimeyavulai nguo nitayaoga thanks for the concern, na chama kimesimama tayari na kitasimama kwa ajili ya the future ya watoto wetu.

Ahsante.

William. (Community Organizer).
 
Nitaangalia yaliyo muhimu tu kwa chama:-

- So far hatuna mwanachama wala kiongozi anayeitwa FMES, kesho nikijaaliwa nitaweka majina ya viongozi wote wa muda na kamati nzima ya chama ya muda.

- Ni chama cha jumuiya sio changu wala cha mtu yoyote ni cha jumuiya, tunaenda pole pole kwanza ilikuwa ni introduction na baadaye tutaenda kwenye mengine ila on our pace.

- Obama hakupewa hiki cheo na yoyote, so na mimi sikupewa na yoyote, inaruhusiwa kujipa mwenyewe kutokana na kzi zako kwa Community ambazo ni za kujitolea, nafikiri unakumbuka sana kwenye msiba wa mzee Chiume, hakuna aliyeniomba kujituma, maana he was my friend na nilikuwa niki-spend a lot of time karibu naye kuchota siasa na busara za maisha.

- Mkuu nimejaribu kuchukua na kujibu niliyoyaona muhimu tu, mengine hapana, halafu be careful maana huenda kuna wanaokuhusu kwenye uongozi na uanachama wa hiki chama, yaani wananchi wengine.

Ahsante
.

William. (Community Organizer)

Vya maana hujajibu, na kuandika maneno mengi hakuna maana kuwa umejibu yale ya maana.

Wapi ametajwa FMES kama ni kiongozi kwenye hiyo post yangu? Read between the lines ndugu.

Unaposema ni chama cha jumuiya, na mnaenda pole pole, ina maana wewe na familia yako ndio mnawakilisha jumuiya?

Unatumia mfano wa Obama, una uhakika Obama alitumia njia kama unayoitumia leo, vinginevyo mfano wako ni irrelevant.

Tabia ya kuanza kujikweza humu unaposaidia kwenye misiba si ya kiungwana. Haiwezekani ufanikishe misiba na party zote peke yako. Je hii ndio inakufanya uwe community organiser? Je ni misiba yoye unashiriki vilivyo au ile misiba ya wanajamii wa aina fulani.

Nasubiri hayo majina ya viongozi na muhtasari wa kikao ulichokuchagua wewe kiongozi.
 
Again nitajaribu kuangalia yaliyo muhimu tu kwa chama:-

Nitaangalia yaliyo muhimu tu kwa chama:-
Unaposema ni chama cha jumuiya, na mnaenda pole pole, ina maana wewe na familia yako ndio mnawakilisha jumuiya?

- Ni mimi na viongozi wote wa muda na mimi kama naibu katibu mkuu wa muda wa chama na msemaji wa chama, kilichonileta hapa ni kuki-introduce chama kwanza, na kutafuta mawazo na ushauri wa namna ya ku-move forward, ndicho ninachokifanya sasa na nitaendelea kufanya hivi.

Unatumia mfano wa Obama, una uhakika Obama alitumia njia kama unayoitumia leo, vinginevyo mfano wako ni irrelevant.

- Obama aliyafanya yale yale kwa jumuiya yake niliyokwisha yafanya na besides katika hiki chama nafasi yangu ni msemaji wa chama, Community Organizer ni nafasi yangu binafsi ambayo haina anything to do na chama, hata wewe unaweza kujiita anything cha muhimu ni kama huvunji sheria kwa kujiita anything.

Tabia ya kuanza kujikweza humu unaposaidia kwenye misiba si ya kiungwana. Haiwezekani ufanikishe misiba na party zote peke yako. Je hii ndio inakufanya uwe community organiser? Je ni misiba yoye unashiriki vilivyo au ile misiba ya wanajamii wa aina fulani.

- Ninashukuru kwamba angalau hapa tunakubaliana kuhusu CV yangu kwa jumuiya, ingawa hayana anything na kukisaidia chama, lakini ni muhimu kwamba umekubali.

Nasubiri hayo majina ya viongozi na muhtasari wa kikao ulichokuchagua wewe kiongozi.

- Kumbuka kwamba hatuna member wala kiongozi anayeitwa ama, kwa hiyo regardless ya what you feel on personalities haiwezi kuwa na effect yoyote kwenye hiki chama, na si kweli kwamba utakua na any impact na what you say, hapana tutasikiliza ushauri tu, ukitaka unaweza kunifungulia thread yangu ninakukaribisha sana, na pia ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba nimeileta hii idea hapa na sasa hii ishu ni the talk of the town, yaani kuanzishwa kwa chama kipya NY,

- Again niwashukuru sana utawala wa JF kwa kutupa hii nafasi, tutaendelea tena soon na mengine zaidi ya chama kipya.

Ahsante.

William. (Community Organizer).
 
William:

  • Zingatia onyo langu: “[N]aomba sana usiite, 'Mkuu" wala Esteemed Reader'! Sitaki. Niite, Estmeed Reader. Napenda!” Lakini bado you are not getting it kwa kuniita, “Mkuu”!
  • Kama self-anointed “Community Organiser”, inaonekana umetumia madola mengi! Hayo mapesa yalikuwa yanatoka wapi, yakhe? Hiyo apartment yako ina vyumba vingapi?
  • Bado sijaridhika na hilo la wewe kudai kuwa ni “progenitor” (mzalishi) wa “social life” hapo New York Metro! kwani ni sawa na Al Gore alivyodai kuwa ndiye aliyegundua Internet! Social life ilikuwepo kwani Watanzania walikuwa huko NY kabla yako! Ila tofauti ya social life ya hao wa zamani ni kwamba iliwajumuisha wazee (wazazi) zaidi ya vijana. After all, vijana wao walikuwa bado ni watoto miaka ya nyuma hadi lilipofika hilo kundi la tsunami la vijana wa Tanzania hapo Mt. Vernon na kwinginepo! Na huu ndio ukweli; sio majungu.
  • Kufika kwa kundi hilo la vijana, kulisukuma nje ya ulingo kundi la wazazi. Vijana wakatamba uwanja wa mbele. Wazazi hawakupenda kujumuika na watoto wao katika kunengua viuno…mgongomgomgo, twanga pepeta type! Na wewe kufika ukafikiria kuwa kulikuwa na ombwe la social life hapo NY!
  • Baadhi ya kundi la vijana (Fundi na Mao) lilianza, kama wewe, kutafuta hafla ziko wapi (birthdays, graduations, batizo, sikukuu) na kubeba vifaa vya miziki kutumbuiza. Mwishowe kutafuta mahali pa kupigia miziki ya disko kwenye mabaa huko Mt. Vernon au kualikwa penginepo. Mwishowe, wewe ukaachwa kwenye mataa ya disko na Mao akang’aa hadi leo.
  • Unaposema, “Soon nitaweka nia na madhumuni ya chama hapa,utaona kwamba hatuna mpango wa kujiingiza kwenye siasa za taifa lolote iwe US wala Tanzania, sio nia yetu hiyo,” una maana kuwa chama tayari kimezaliwa? Hayo si madhumuni, bali ni tentative tu hadi hapo wanachma watakapoyakubali.
  • Kulingana na usemi wako, website na katiba itatolewa. Je, kwa nini muanze kutengeneza website na kutunga katiba na hali chama hakijazaliwa?
  • Unapenda sana credit, Msemaji wa Chama na wakati mwingine Mkuruenzi wa Habari na Mawasiliano?
  • Itafaa sana kuwataja wale waliokutana hapo Harlem, sijui kwa nani na kuanzisha wazo la kuunda chama? Tupe majina yao. Ili chama kianze na unquestionable transparency.
  • Mke wako alitoka Ubelgiji, kama local employee wa huko huko ofisi yetu ya ubalozi; hakuwa Foreign Service Officer. Cheo hicho si transferable.Kwa muda mrefu hiyo Ofisi ya Ubalozi wetu ilikuwa ikikataa kuajiri Watanzania on local terms (local employees). Lakini mke wako alifanikiwa.
  • Kutokana na vyanzo vyangu (ambavyo nitaviheshimu kwa kutovilopoa nje ya kadamnasi) kuna ukweli kwamba akina mama wa Tanzania, kama watatu hivi, waliojaribu sana kuomba kazi ya u-receptionist hapo kwenye Ofisi ya u-Balozi wetu NY na kugonga mwamba kwamba ofisi ilikuwa haiajiri!
  • Lakini mke wako alifanikiwa. Na hii imewaacha hao akina mama kujiuliza, kulikoni? Mosi, mmoja wa akina mama hao anaamini kuwa ni kutokana na shauri ya uhusiano wa ki-kabila - baina ya baba mkwe wako (Mzee Brown Ngwilulupi) na Balozi Mwakawago (watu wa Iringa), licha ya hao kusoma pamoja huko Makerere na kufanyakazi serikalini kwa muda mrefu. Pili, uhusiano wa Mzee Brown Ngwilulupi/Balozi Mwakawago na baba yako (John Malecela) pia ulisaidia mke wako kapata hiyokazi!
  • Kwa nini hujaweka majina ya wanakamati ya kutayarisha kumuaga Balozi Mwakawago (marehemu sasa)? Ndio mlitayarisha hafla ya kumuuga Balozi Mwakawago. Je, mlimuaga Balozi Foum na kumkaribisha Balozi Chagula? Mlimuaga Balozi Chagula na kumkaribisha Balozi Nyaki? Mlimuaga Balozi Nyaki na kumkaribisha Balozi Mwakawago? Je, mlimkaribisha Balozi Mahiga? Je, mlimkaribisha Balozi wa ma-Balozi Asha Migiro?
  • Mwisho, ni lazima iwepo sababu ya kumuaga Balozi Mwakawago na hata kuomboleza kifo chake! Kuna wenye kuamaini kuwa sababu hiyo imejikita sana katika u-dini kwa baadhi ya Watanzania hapo NY na (kwako ilikuwa ni) “payback time” kwa kumwajiri mke wako!
Disclaimer: Kama haya niliyoandika yanazidisha u-majungu jungu, yatupilie mbali!! Ni matumaini yangu kuwa baadhi ya Watanzania wa huko New York watani-vindicate!
 
- Again, nitajibu yale tu yanayohusu chama, hayo mengine nisubiri kwenye kampeni iwapo nitagomeba nafasi yoyote kwenye chama hiki kipya:-

William:

  • Zingatia onyo langu: “[N]aomba sana usiite, 'Mkuu" wala Esteemed Reader'! Sitaki. Niite, Estmeed Reader. Napenda!” Lakini bado you are not getting it kwa kuniita, “Mkuu”!

- Siiti majina ya bandia kwangu ni mwiko, unless ungekwua unatumia jina lako kamili kama mimi.
  • Kama self-anointed “Community Organiser”, inaonekana umetumia madola mengi! Hayo mapesa yalikuwa yanatoka wapi, yakhe? Hiyo apartment yako ina vyumba vingapi?

  • - Panapobidi nimetumia hela zangu za binafsi na pasipobidi nimechangisha, mapesa niliyotumia ni ya kutoka mfukoni mwangu,yaani mapesa yangu.

    [*]Baadhi ya kundi la vijana (Fundi na Mao) lilianza, kama wewe, kutafuta hafla ziko wapi (birthdays, graduations, batizo, sikukuu) na kubeba vifaa vya miziki kutumbuiza. Mwishowe kutafuta mahali pa kupigia miziki ya disko kwenye mabaa huko Mt. Vernon au kualikwa penginepo. Mwishowe, wewe ukaachwa kwenye mataa ya disko na Mao akang’aa hadi leo.

    - Wakuu Fundi na Mao walinikuta NY, nikiwa tayari nimeshaanza hizi shughuli za kupiga muziki, infact mara mbili nilipigisha Disco kabambe sana ambapo hawa wakuu wawili walikuwa ndio ma-DJ, nikapiga tena one more time nikishirikiana na DJ Mao, tulipomaliza nilimkabidhi rasmi mikoba na ku-retire shuguli za kupiga Disco akaanza kwa kushikiriana na Club Serengeti, inaelekea ulikua hujafika NY.

    - Anyways, ninakwenda kukutana na Mkuu aliye-originate ile Movie ya 'Hotel Rwanda", nitarudi later kumalizia majibu.

    Thanks.

    William.
 
Back
Top Bottom