Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 186
...and Tendwa, still insists......CCJ is HOAX!
...and Tendwa, still insists......CCJ is HOAX!
Tendwa naye alikuja na hiyo term jana, akikanusha uwepo wa CCJ! sasa nashindwa kushangaa kama anayajua hayo yaliyowekwa hapo juu......!We hizo terminology za kwa akina Mama Lwakatare na misukule nawe wazileta huku??
Poa mzee......Dar takupa update.....bt hujaachwa Kitonga mzee.....!Tehe teheeee.... mambo vipi? Mbona ile issue unataka kuniacha kitonga?
Binadamu wote ni sawa na wana haki sawa ...... Hao wenye hadhi nao walianzia kwenye usisimizi tu!Jamani naiomba CV ya hawa akina Kiyabo na huyo mwenzie Muhabi. Hawa background zao ni nini? Kwa nini wanapewa hadhi inayofanana na CCM wakati wao ni sisimizi tu?
Kisije kikawa ni Chama cha Mafisadi, No. 2, in disguise!
KIWEWE cha kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) kinachohusishwa na baadhi ya vigogo maarufu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashika kasi huku kamati ya wazee iliyoongozwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, ikishindwa kumaliza makundi kama ilivyokusudiwa, Raia Mwema limefahamishwa.
Habari zinaeleza kwamba CCJ imeitikisa CCM, pamoja na kauli za kujifariji zinazotolewa kupooza makali ya chama hicho ambacho hata usajili hakijapata, kikineemeka kwa gharama za hofu ya ndani ya CCM.
Uchunguzi wa Raia Mwema umethibitisha kwamba vyombo vya dola vimekuwa katika harakati za kuwafuatilia watu wote wanaohusishwa na CCJ hata kwa kutajwa tu, wakiwamo wabunge na hata viongozi wastaafu na wa sasa serikalini.
Kaazi kweli kweli, kuna watu hawalali ati !! Halafu twadai tuna demokrasia !Kwa mujibu wa habari hizo, nyumba za baadhi ya watu wanaohofiwa kuwa nyuma ya CCJ zimewekewa ukachero wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuwekwa vifaa ama watu maalumu ndani na nje ya maeneo wanayoishi na kufanyia kazi na baadhi ya maeneo hata watu kuzunguka ufukweni mwa bahari karibu na makazi hayo.
Tanzania sasa imekuwa kama nchi nyingine za Afrika zinazoendesha siasa za kibabe na huko tunakoelekea hali itakuwa mbaya zaidi. Hebu fikiria sasa CCJ imesababisha watu waanze kuogopa hata kutembeleana. Inatisha sana, wageni wakija unawaambia wasizidi wawili maana mtaambiwa mnafanya kikao, anasema Mbunge mmoja wa CCM anayetajwa kuhusishwa na CCJ.
Imeelezwa kwamba kwa sasa watu ambao vigogo ndani ya CCM wanawahofia wanaotajwa kuwa ndani ya kundi la Sitta na lile la mawaziri wastaafu, kutokana na nguvu zao kisiasa na wanasiasa hao wameelezwa kufuatiliwa kwa karibu huku baadhi ya wafuatiliaji wakidhihirisha waziwazi na wengine wakifanya hivyo kijasusi.
Masikini Tendwa, halafu anadai anatimiza wajibu wake kwa uhuru na bila kuingiliwa !Mbali ya wanasiasa, Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa na watendaji wake nao wamejikuta wakitakiwa na vyombo hivyo kutoa maelezo ya kina kuhusiana na wahusika wakuu wa chama hicho na historia zao hali ambayo inatishia uhai wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini leo zaidi ya miaka 18 tokea kuhalalishwa.
Wakati vyombo vya usalama vikiwa katika harakati hizo, baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM, akiwamo Katibu Mkuu wake, Yussuf Makamba, wameendelea kutoa kauli za kupuuza kuanzishwa kwa chama hicho na kuhusishwa kwake na vigogo mashuhuri wa CCM.
Makamba amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akisema chama chake hakitishiki na kuanzishwa kwa CCJ lakini pia kwamba kama kuna vigogo wanaokusudia kuhama CCM wakifanya hivyo watakuwa wamejimaliza kisiasa.
Mbali na Makamba kiongozi mwingine wa CCM aliyetoa kauli ya namna hiyo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni (mstaafu) John Chiligati, huku baadhi ya vyombo vya habari vikiwamo vinavyotajwa kuegemea kundi mojawapo kati ya mawili makubwa yanayokinzana ndani ya CCM, vikitumika kuwahusisha wenzao wa kundi jingine.
Makamba na wenzake wamekuwa wakikwepa hali ya mambo kwamba makundi mawili makubwa ndani ya CCM yamekuwa yakijitofautisha katika kile kinachotajwa kuwa ni vita dhidi ya ufisadi, kundi moja likipinga ufisadi na kutaka chama hicho kisimamie misingi ya kuanzishwa kwake na misimamo ya waasisi wa chama hicho, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.
Hiki si tayari kipo mkuu?Tunasubiri CCK- Chama Cha Kifisadi???????????kije maana ndio wakati huu.
Wadau wa JF naomba mwenye data za kweli atusaidie watu walioko nyuma ya CCJ maana kila muhusika mshukiwa anayeulizwa aidha anakataa au anapatwa kigugumizi kujibu. Natanguliza shukrani.