Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Mwenyewe (Tendwa) alishasema 'CCJ is a hoax'!
 
Mwenyewe (Tendwa) alishasema 'CCJ is a hoax'!
 
Wakuu CCJ wamenza kuwekewa kiwingu.

Hivi haiwezekani hiyo CCJ kuwaomba wanachama wake toka hiyo mikoa 8 ya Bara na Miwili huko Visiwani kwenda Ofisini kwa Mrajisi ili aweze kuwa hakiki?

Mfano wa Dar labda Jumatatu, Moro - Jumanne, Dodoma - J'tano, Aruisha - Alhamisi, Kilimanjaro - Ijuma, Tanga - Jumatatu inayo fuatia, Iringa - Jumanne nk nk , wamuulize tu waje na vitambulisho gani na barua gani za nyumba kumi kumi?

Au CCJ wamkopeshe mrajisi hela za usafiri za hao makarani wake wakafanye uhakiki.


Mbona haujaeleweka mzee. Hujaweka evidence yeyote ku-justify hiyo mizengwe!!!
 
Wakuu CCJ wamenza kuwekewa kiwingu.

Hivi haiwezekani hiyo CCJ kuwaomba wanachama wake toka hiyo mikoa 8 ya Bara na Miwili huko Visiwani kwenda Ofisini kwa Mrajisi ili aweze kuwa hakiki?

Mfano wa Dar labda Jumatatu, Moro - Jumanne, Dodoma - J'tano, Aruisha - Alhamisi, Kilimanjaro - Ijuma, Tanga - Jumatatu inayo fuatia, Iringa - Jumanne nk nk , wamuulize tu waje na vitambulisho gani na barua gani za nyumba kumi kumi?

Au CCJ wamkopeshe mrajisi hela za usafiri za hao makarani wake wakafanye uhakiki.


Mbona haujaeleweka mzee. Hujaweka evidence yeyote ku-justify hiyo mizengwe!!!
 
ukijibu kama hivyo unakuwa umemsaidia au kumkomoa?
Kawaida ya wabongo, kukatisha tamaa tu. Mkuu mimi hata kama sipo CCJ wala CCM wala CHADEMA usumbufu wowote usio wa lazima ambao unaonekana wa wazi huwa sifurahishwi nao. Yawezekana aliyemjibu pia ni mmoja wa wafanyakazi wa Tendwa, fungua macho
 
ukijibu kama hivyo unakuwa umemsaidia au kumkomoa?
Kawaida ya wabongo, kukatisha tamaa tu. Mkuu mimi hata kama sipo CCJ wala CCM wala CHADEMA usumbufu wowote usio wa lazima ambao unaonekana wa wazi huwa sifurahishwi nao. Yawezekana aliyemjibu pia ni mmoja wa wafanyakazi wa Tendwa, fungua macho
 
Kawaida ya wabongo, kukatisha tamaa tu. Mkuu mimi hata kama sipo CCJ wala CCM wala CHADEMA usumbufu wowote usio wa lazima ambao unaonekana wa wazi huwa sifurahishwi nao. Yawezekana aliyemjibu pia ni mmoja wa wafanyakazi wa Tendwa, fungua macho
hahahahahahhahahaha...safi sana...
 
Kawaida ya wabongo, kukatisha tamaa tu. Mkuu mimi hata kama sipo CCJ wala CCM wala CHADEMA usumbufu wowote usio wa lazima ambao unaonekana wa wazi huwa sifurahishwi nao. Yawezekana aliyemjibu pia ni mmoja wa wafanyakazi wa Tendwa, fungua macho
hahahahahahhahahaha...safi sana...
 
Bandiko hili halieleweki? Ni mizengwe gani unayozungumzia?
 
Bandiko hili halieleweki? Ni mizengwe gani unayozungumzia?
 
Mbona haujaeleweka mzee. Hujaweka evidence yeyote ku-justify hiyo mizengwe!!!
kauli yake ya kutabiri kama sheikh Yahya ndio inaonyesha picha ya mizengwe yake.
Kwamba kukipatia usajili wa kudumu kabla ya uchaguzi haiwezekani, pili unasema chama hicho ni hoax, kwa hiyo waliokuja kukisajili ni maruhani?
 
Date::2/1/2010Mrema: CCJ zao la kongamano la Butiku
bwanamrema.jpg
Mwenyekiti wa chama cha TLP,Augustino Mrema ambaye amedai Chama Cha Jamii CCJ ni zao la lililotokana na kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Joseph ButikuWaandishi Wetu
MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema amesema Chama Cha Jamii (CCJ) kimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Joseph Butiku, ambaye ameyaelezea madai hayo kuwa "upuuzi".

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mrema alisema vigogo wa CCM waliozungumza kwenye kongamano hilo na kutamka wazi kuwa Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kufanya maamuzi magumu, ndiyo waanzilishi wa CCJ.

CCJ ni chama kipya cha kisiasa ambacho kuanzishwa kwake kunahusishwa na mkakati wa vigogo na baadhi ya wabunge wa CCM ambao hata hivyo hadi leo hawajajitokeza hadharani.

Mrema, ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kabla ya kutofautiana na mawaziri wenzake mwaka 1995 na kujiunga na chama pinzani cha NCCR Mageuzi, alidai kuwa ametumia mbinu zake za usalama wa taifa kuwatambua vigogo hao.

Bila kuwataja kwa majina, Mrema alisema vigogo hao wanatumia mwamvuli wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuandaa makongamano kwa nia ya ya kumtukana na kumhujumu Rais Kikwete.

"Wanatumia mwavuli huo kumtukana rais kwamba anazungukwa na wezi na kwamba hana maamuzi magumu wakati wenyewe hawana maamuzi hayo," alisema Mrema.

"Ni aibu kwa vigogo hao wa CCM tena wanaojifanya kuwa wapo chini ya mwamvuli wa Tasisi ya Baba wa Taifa kuandaa makongamano ya kumtukana rais wetu hadharani wakati wenyewe pia hawana mamuzi magumu na kama wanayo basi wajitangaze hadharani kuwa wao ndiyo CCJ," alisema Mrema.

Mrema, ambaye alikuwa nchini India kwa matibabu na ambaye alikanusha kuwa safari yake ilidhaminiwa na Kikwete, alisema: “Kumwambia rais maneno makali kama hayo tena hadharani ni kutaka wananchi wamdharau na kumwona mwizi pia na kimsingi huu ni uhaini.

"Nimetumia uzoefu wa taaluma yangu ya Usalama wa Taifa na kubaini machafu yanayofanywa na vigogo... simtetei Kikwete bali natetea rais yeyote wa taifa hili siyo Kikwete tu kama wanavyosema nipo kwenye mtandao wa Kikwete na wengine kudai kuwa nimenunuliwa.

"Kikwete hawezi kuninunua; mimi ni mtu wa gharama sinunuliki, ila kwenye ukweli panastahili kuzungumzwa; natumia taaluma yangu kutetea taifa, siwezi kuona taifa linayumba halafu nikae kimya; mimi na mkurugenzi mstaafu wa Usalama wa Taifa bwana."
Hata hivyo, hakueleza alikuwa mkurugenzi wa kitengo gani cha Usalama wa Taifa.

Mrema aliongeza kusema: "Siingii jikoni kupika, lakini nina utaalamu wa kupika. Ninataka wale vigogo wanaomhujumu rais kwa maneno ya kijeli, kama wana uwezo na kujiamini wajitokeze hadharani wasema wao ndiyo wenye CCJ."

Hata hivyo mwenyekiti wa taasisi hiyo, Joseph Butiku alipuuza madai hayo ya Mrema akisema hawezi kuzungumzia upuuzi.
"Sitaki kuulizwa maswali yasiyo na maana; nenda kamuulize aliyekwambia upuuzi huo," alisema Butiku.

Katika hatua nyingine wakati Mrema akitoa tuhuma hizo nzito, CCJ imeanza mapambano kupigania usajili wake kwa kumhoji Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa sababu za kushindwa kuwapa usajili wa muda.

Tamko hilo la CCJ kwa Tendwa limekuja katika kipindi ambacho Msajili amekuwa akisisitiza kuwa uwezekano wa chama hicho kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 haupo kwa sababu muda hautoshi kwa chama hicho kukamilisha taratibu zote ili kipate usajili wa kudumu.

Usajili wa muda, ambao unahusisha chama kipya kitafuta angalau wanachama 200 kutoka mikoa 10 au zaidi, huchukua miezi sita ambayo hufuatiwa na uhakiki unaofanywa na Msajili kabla ya kupata usajili wa kudumu.

Tendwa alisema hata kama chama kipya kitakamilisha sharti hilo la kwanza katika muda mfupi, sheria ya miezi sita inabakia kama ilivyo.

Ndani ya kipindi hicho cha usajili wa muda na uhakiki, Tume ya Uchaguzi itakuwa imeshaanza taratibu za uchaguzi kwa kuruhusu wagombea waliopitishwa na vyama vyao kuanza kuchukua fomu.

Lakini uvumilivu uliwashinda CCJ ambao jana walimshukia Tendwa wakidai kuwa anadhofiisha mipango hiyo ya kukipa chama usajili wa muda kwa malengo anayojua mwenyewe.

Renatus Muabhi, ambaye ni katibu mkuu wa CCJ, alitoa tamko linalosema: "Hali iliyopo sasa imesababisha viongozi pamoja na wanachama watarajiwa wa CCJ kuwa katika hali ya utata na kuhofia mustakabali mzima wa upatikanaji wa usajili wa muda wa CCJ.

"Tunapata taarifa za maelezo ya msajili wa vyama vya siasa nchini yanayokinzana na wajibu wake kupitia vyombo vya habari pasipo sisi kuwa na taarifa yoyote inayoonyesha hatua ipi imefikiwa juu ya usajili wa CCJ.

"Kwa mfano, tarehe 26/01/2010 siku ya Jumanne gazeti la Daily News lilichapisha maneno ya msajili ambayo kwetu sisi yanatuingiza katika utata na hofu juu ya usajili wa chama chetu."

Tamko hilo linaendelea kueleza kuwa Tendwa anakwenda kinyume na taratibu pamoja na dhamana aliyopewa na kuhakikisha kwa vitendo ya kwamba nchi ya Tanzania ni ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa vyama vingi, badala ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha watu kuunda na kujiunga katika vyama vya siasa ili kuleta demokrasia ya kweli.

Linamtuhumu Tendwa kuwa anakatisha tamaa na kuwavunja moyo Watanzania kuhusu tafsiri ya kuanzishwa kwa CCJ hasa pale anaposema chama hicho ni sawa na vyama vingine vilivyopo. Habari hii imeandaliwa na Ramadhan Semtawa, Mussa Mkama na Minael Msuya.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=17669
 
Mrema kaamua kumpigia magoti Kikwete, Maalim Seif naye anamlammba miguu Karume, siasa za Tanzania kunani?
 
Nadhani hapo kuna technical mistake inayofanywa na Msajili wa vyama vya siasa. Kama hilo si kweli, basi anataka kukisaidia Chama Cha Jamii (CCJ) kujijenga.

Nasema hivyo kwa kuwa, hatua anayoichukua ya kuchelewesha kwa makusudi kukisajili chama hicho, itazua manung'uniko na watu wengi zaidi (hata ambao hawakuwa wakijali uanzishwaji wa chama hicho) wataanza ku-sympathize na CCJ na kuamsha ari ambayo haikuwepo. Baada ya hapo, atalazimika kukisajili chama ambacho kitakuwa na nguvu kubwa kuliko iliyokuwa nayo, au ambayo ingeweza kuwa nayo kama Msajili angetekeleza wajibu wake bila hiyana.

Mambo kama haya ya kukuza umaarufu wa watu na taasisi pinzani, hufanywa sana na viongozi wa sasa wa chama tawala katika sehemu mbalimbali. Walifanya kosa kama hilo walipomsimamisha Mhe. Zitto Kabwe kuhudhuria vikao vya Bunge. Hatimaye akapata umaarufu wa juu kabisa aliporudi bungeni.

Nadhani inabidi kutenda majukumu kama inavyotegemewa badala ya kuanza kufanya maajabu ya kushangaza. Msajili atekeleze wajibu wake na aache kukuza umaarufu wa CCJ bure tu, kitu ambacho nahisi hakusudii, na anadhani anasaidia anaowajua.
 
Hivi huyu Tendwa ambaye kama sikosei aliwekwa na Chama Cha Majambazi tangu mfumo wa vyama vingi ni muadilifu kiasi kwamba hawezi kupatikana msajili mwingine? Masharti ya ufanyaji kazi katika sehemu nyeti kama hizi lazima iangaliwe, haiwezekani aendelee kukaa pale miaka na miaka kwa sababu za uzoefu atakwamisha mambo na atakuwa corrupt..
 
tanzania_210_29.jpg

Chama kipya cha kisiasa kimejitokeza huko Tanzania wakati nchi inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa Rais na wa Bunge baadae mwaka huu.

Chama hicho kimeanzishwa na baadhi ya wanachama wa sasa katika chama tawala cha CCM, ambao wanakhofu wataondolewa kwa njama katika utaratibu wa kupata wagombea ndani ya chama hicho kutokana na tofauti za mtazamo zinazojitokeza hivi sasa miongoni mwa wanachama wa CCM.

Kuna shutma kwamba ndani ya chama cha CCM, kuna makundi yanayopingana na kupanga mikakati ya kuharibiana katika utaratibu wa kupata wagombea ndani ya chama hicho kwenye uchaguzi utakaofanyika baadae mwaka huu.

Kufuatia hali hiyo hatimaye chama kinachohusishwa kuondoka kwa baadhi ya vigogo wa chama cha CCM, kinachojulikana kama Chama Cha Jamii-CCJ, kimewasilisha maombi ya usajili wake kwa msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania, John Tendwa.

Sauti ya Amerika ilizungumza na katibu mkuu wa muda wa chama cha CCJ, Renatus Muhabi, ambaye hata hivyo alikana kuhusishwa kwa chama hicho na baadhi ya vigogo ndani ya chama cha CCM, wenye khofu ya kuenguliwa. Anasema, “chama hichi tumekiunda kwa makusudi mazima kwamba kiwe chama cha jamii, kwa maana kila mtanzania atakae jisikia kua na imani na chama hichi, atakae pendekezewa na sera zake basi anakaribishwa.”



http://www.voanews.com/swahili/2010-01-22-voa5.cfm
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amesema kuwa, ofisi yake inafuata demokrasia na misingi ya haki hivyo hakina mpango wa kuwanyima haki wanaotaka kuanzisha chama chao.

  1. Akizungumza leo asubuhi katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na kituo cha TBc 1, amesema kuwa lawama anazopewa za kuchelewesha usajili wa chama kipya cha Chama cha Jamii (CCJ), hazina hoja za msingi hivyo ni vyema sheria zikafuatwa ili usajili ukifanyika uwe umezingatia misingi ya sheria.

    Amesema kuwa ofisi yake ina masharti ya usajili ambapo haiwezi kusajili chama chenye ubaguzi wa kidini, kinachotumia mabavu kuendesha siasa, ubaguzi wa kijinsia na mengineyo.

    Amesema kuwa hadi sasa ana jumla ya maombi ya vyama sita kikiwemo CCJ ambao wameomba usajili na wanafanya taratibu kuchunguza kama vimekidhi viwango vya usajili.

    " Si CCJ peke yao vipo vyama vitano tayari vimeomba usajili na CCJ ni cha sita, tunaomba eleeleweka kuwa nchi inaongozwa kwa sheria na tunazingatia zaidi misingi ya demokrasia hakuna atakayenyimwa haki yake katika hili, "amesema Tendwa.

    Aliongeza kuwa, ana imani ofisi yake inafanya kazi kwa taratibu bila kusukumwa na mtu yoyote kwa maslahi yake binafsi au ya chama chake.

    Akielezea kucheleweshwa usajili kwa chama cha CCJ amesema kuwa, wakati CCJ wakileta maombi yao tayari ofisi yake ilikuwa ikijiandaa kwenda bungeni.

    " Ndani ya chama hakuna hata chama kimoja tunachokipigia debe ili kifanye vizuri kuliko vingine hivyo nina imani tutakaporejea wanasheria wetu wakakuwa wamekamilisha taratibu za usajili kwa vyama ambavyo vimekidhi masharti,"amesema Tendwa.

    Amesema kuwa, masharti yanayozingatiwa na waombaji wa usajili ni kutafuta wanachama 200 kutoka Unguja na Pemba na kila mkoa wa Tanzania Bara.

    " Inatakiwa wananchi wajiulize kwanini watu wawe na haraka waje Januari kama walikuwa wapo kwa muda mrefu sisi tupo sasa kwa miaka 18 pale wangekuwa wamekuja ili tuwashughulikie suala lao, "amesema Tendwa.

    Tendwa amesema kuwa maridhiano ni jambo bora ambapo tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa kulikuwa na changamoto mbalimbali ambapo hadi sasa vilivyo imara na vinapata ruzuku ni saba tu.

    " Utaratibu wa usajili mtu anakuja kusajili chama chake ambapo kama haelewi anaelekezwa kwani demokrasia ni mfumo si chachu hivyo taratibu za kisheria lazima zifuatwe,"amesema Tendwa.

    Tendwa amesema kuwa ni jambo la busara kama misingi ya maadili ya nchi itazingatiwa kwani rushwa imekuwa ndo kero kubwa sasa hasa katika kuelekea uchaguzi ambapo wajumbe wengi wamekuwa wakilia kutokana na hali hiyo huku baadhi ya wananchi wakineemeka kwa kukiita kipindi cha uchaguzi ni cha mavuno.

    Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Tendwa anakwamisha usajili wa chama cha CCJ jambo ambalo mwenyewe amelikana.
 
Kauli ya CCM Kuhusu Kuanzishwa kwa Chama Kipya cha Upinzani – CCJ

Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vinaandika sana habari za kuanzishwa kwa Chama kipya cha upinzani kiitwacho Chama cha Jamii (CCJ). Habari kuhusu ujio wa chama hiki zimekuwa zinapambwa na vibwagizo vingi kwamba kimenzishwa na vigogo wa CCM kwa lengo la kukisambaratisha Chama cha Mapinduzi. Baadhi ya vyombo vya habari na hasa makala katika magazeti yamekuwa yanatabiri na kutarajia kumeguka kwa CCM kutokana na kuanzishwa kwa CCJ.

Chama cha Mapinduzi kinapenda kuwaarifu WanaCCM na Watanzania kwa jumla kwamba.

Kwanza, Chama cha Mapinduzi ndicho kiliruhusu uanzishwe mfumo wa vyama vingi 1992; hii ilikuwa baada ya Watanzania 80% kutoa maoni kwamba mfumo wa chama kimoja (yaani CCM) uendelee, na 20% walitaka uanzishwe mfumo wa vyama vingi. CCM ilikuwa na sababu nzuri ya kuwasikiliza waliowengi (80%), yaani wengi wape!

Lakini kwa kutumia busara kubwa CCM ilitoa fursa ya Watanzania 20% waanzishe vyama vyao vya upinzani na wamekuwa wanavianzisha, hadi sasa vipo 17. Hivyo kuanzishwa kwa chama kipya cha upinzani cha 18 si jambo la ajabu; lakini magazeti yanalikuza mno jambo hili kwa lengo la kuuza magazeti yao na pia kuwatisha Watanzania na hasa WanaCCM kwamba CCM inameguka. Hila hizi ovu hazitofanikiwa!

Pili, Chama hicho kinachoandikwa sana magazetini ndio kwanza kimeomba usajili. Hakijasajiliwa; na inawezekana kisipate usajili kabisa. Kwa mujibu wa sheria chama kinachoomba usajili, kwanza hupata usajili wa muda, na kisha huchukua miezi sita kupata usajili wa kudumu iwapo kitatimiza masharti na vigezo vya usajili wa kudumu. CCJ hawajapata hata usajili wa muda! Kwa kuwa mchakato wa uteuzi wa wagombea utaanza mara tu Bunge litakapovunjwa mwezi Julai, hao vigogo wa CCM watakao hama na kujiunga na CCJ wataomba uteuzi kupitia CCJ wakati gani? Hivyo taarifa kwamba kuna vigogo wengi wa CCM watagombea kupitia CCJ ni uvumi usio na mantiki yoyote. Hakuna kiongozi makini wa CCM atagombea Ubunge au Urais kupitia Chama kisicho na usajili; ni sawa na kuingia katika boti iliyotoboka na kutaka kusafiri nayo baharini!

Tatu, Hata kama ikitokea miujiza CCJ ikapata usajili wa kudumu kabla ya miezi sita na kuingia katika uchaguzi, na hata ikitokea baadhi ya viongozi wa CCM wakaamua kuhama CCM na kugombea kupitia CCJ, halitakuwa tukio la kwanza, wala sio jambo la ajabu. Tukio kama hilo limetokea mara nyingi. Wapo viongozi wengi wa vyama vya upinzani ambao walikuwa viongozi wakubwa CCM; waliamua kuhama, lakini CCM iliendelea kuwepo na iliendelea kuwa imara. Utabiri kwamba baadhi ya vigogo wa CCM wakihamia CCJ utakuwa ndio mwisho wa CCM, unapingwa na historia. Ukweli ni kwamba viongozi waliohama CCM na kwenda upinzani hawakupata mafanikio yoyote huko walikokwenda, wakati CCM waliodhani ingetetereka inaendelea kuwa imara, haijameguka wala kutetereka. Vivyo hivyo ikitokea baadhi ya viongozi wa CCM wakihama na kwenda CCJ au chama chochote cha upinzani, ukweli wa historia utabaki pale pale kwamba CCM itabaki imara, haitameguka wala kusambaratika; bali wao watakuwa wamejimaliza kisiasa. Ni muhimu Watanzania waelewe kwamba umaarufu wa viongozi wa CCM unatokana na umaarufu wa CCM, kiongozi anayeondoka CCM umaarufu wake huporomoka. Huu ndio ukweli wa kihistoria.

Nne, CCM inapenda kusisitiza kwamba wale wote wanaosubiri CCM imeguke wanapoteza muda wao. CCM ina historia ndefu na iliyotukuka, ina mtandao mpana sana, pia inajeshi kubwa la wanachama milioni nne na nusu. Sera za CCM za kupigania haki za wanyonge kuhusu elimu, afya, maji, uwezeshaji wananchi kiuchumi; ujenzi wa barabara za Vijijini na barabara kuu, n.k, zinawavutia watu wengi. Na jambo la muhimu ni kwamba zinatekelezwa vizuri pamoja na maneno ya ghiriba yanayoandikwa katika vyombo vya habari kwamba eti Rais Kikwete na CCM hawajafanya lolote! Hii ni ghiriba ambayo nayo haitafanikiwa. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita ambapo CCM ilipata ushindi wa 91% ni majibu tosha kwa wale wote wenye ndoto mbaya dhidi ya CCM. Matokeo haya ni salamu na ujumbe mzito kwamba wananchi Mijini na Vijijini wanaridhika na Sera za CCM na utekelezaji ilani ya CCM chini ya jemedari Rais Kikwete. Na ni hao hao wananchi watakaopiga kura katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, na hapana shaka matokeo yatakuwa hayo hayo kwa CCM kuibuka na ushindi mkubwa. Katika mazingira haya ya Chama cha Mapinduzi kukubalika na kuheshimiwa na Watanzania, suala la kumeguka au kusambaratika ni ndoto ya mchana!

Tano, kwa kifupi CCM inapenda kuwatahadharisha WanaCCM kwamba wasitishike na ripoti za magazeti yanayokipamba chama ambacho hakina usajili, chama ambacho hakitashiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao, wala hakuna kigogo hata mmoja wa CCM ambaye hadi sasa aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa chama hicho. Kelele ni kubwa za kukipamba chama hiki (CCJ) kuliko hali halisi. Vitisho kwamba CCM itameguka ni vingi lakini ni uzushi mtupu. Hizi ni njama na ghiliba; hivyo WanaCCM na wananchi kwa jumla zipuuzeni. CCM ndiyo iliyoanzisha mfumo wa vyama vingi 1992 na hivi sasa vipo 17, haitishiki na hakijapata kutishika na mfumo wa vyama vingi; iweje hicho cha 18 ndicho kiinyime usingizi CCM! Tunatoa wito kwa WanaCCM kwamba tuendelee kujenga chama chetu, tuendelee kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa bidii. Chama cha CCJ ni chui wa karatasi, kisiwahangaishe, ni njama za kutufanya tuchelewe kutekeleza agenda muhimu za chama chetu na tubaki tunafuatilia chama ambacho bado hakina usajili na wala hakitashiriki katika uchaguzi. Tusiingie katika mtego huu uliowekwa na watu wasiokitakia mema chama chetu.

Mwisho kabisa tunapenda kuwahakikishia watanzania kwamba CCM hakikuogopa kuruhusu mfumo wa vyamba vingi, CCM ndiye mwasisi na mkunga wa mfumo wa vyama vingi, hivyo uanzishwaji wa chama chochote cha upinzani haliwezi kuwa tishio kwa CCM. Aidha kwa viongozi wa CCM kuhamia vyama vya upinzani sio jambo jipya na halijaathiri umaarufu na uimara wa CCM. Na mara nyingi viongozi wa CCM wanaohamia upinzani wamekuwa wanarejea CCM baada ya kugundua kwamba kwenye vyama vya upinzani hakuna lolote la maana, na CCM tumekuwa tunawapokea na tutaendelea kuwapokea bila ya kinyongo. Kwa jumla tunawaomba WanaCCM wasitishwe na ghiriba za magazeti kwani chama chetu bado ni imara na tumaini na nguzo ya Watanzania katika kudumisha umoja na amani ya nchi yetu.



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na


CAPT JOHN Z. CHILIGATI (MB)

KATIBU WA NEC: ITIKADI NA UENEZI
 
Back
Top Bottom