Dr. Bana, kwa hilo namuona ana muono wa upeo mkubwa sana.
Hivi uchukulie mfano wa magwanda, si watasusia nchi hawa mambo yakienda kombo kidogo. Mzee wa kiraracha nachama chake wamesha salim amri, NCCR ndio hoi bin Taaban, CUF ndio tayari na kushinda kwao uchaguzi wa visiwani lakini wamejijuwa kuwa chama chao hakiwezi kuongoza na wameridhia kuongozwa na CCM.
Bana kwa hili uko juu. Wengi sana wanafikiria kupiga kelele na kushinikiza maandamano na kususa ndio kuongoza? hapana. Wangeona mfano Egypt, huko sasa tunaona hata washabiki wa mpira wanauana hovyo.
Nadhani viongozi wa magwanda wameliona hilo na sasa wamebadilika, nilipowaona wanakwenda Ikulu na kunywa juisi kwa kashata nikajuwa, sasa hawa ndio wanaanza siasa, wakiendelea hivyo, baada ya miaka 20, wajukuu wa waasisi wa hiyo kampuni wanaweza kuongea mengine.