Hao ndiyo chadema bwana hataki hata ukiwaambia ukweli kupinga ni jadi yao. ila kwa hapa nakupongeza kwa kuwaomba waelewe manaa ya neno Mbadala maana tutaruka Maji na kukanyaga matopeee
Mkuu kwa hapa tulipofokia kama watanzania, umuhimu wa kubadili utawala ni kurejesha nguvu ya utawala kwa wenye nchi ambao ni watanzania na kuondokana na kasumba ya leo ambavyo watanzania wamesukumizwa kwenye kona na watawala na mafisadi wakiwa hawana sauti ya kuhoji wala kugomea ubaya wowote unaofanywa na watawala hawa . Watanzania wamekuwa kama watumwa kwenye nchi yao, wanalima na kuzalisha kwa ajili ya matumbo ya watawala na mafisadi. Hawana ujasiri wa kuhoji wala kikataa uovu wanaotendewa na watawala wa sasa. Ni nchi gani ambayo wananchi waka hawawezi kulalamika hata kama ukipandisha bei ya kila kitu? Hawawezi hata kugomea huduma mbovu za afaya na elimu ili hali watawala wanatesa na maV8 wakizunguka kwa kodi zao?
Nchi hii tuko huru lakini bado ni watumwa ndani ya nchi yetu wenyewe! Mtumwa hupoteza kwanza fikra zake na kujiona yuko kawaida hataanapoonewa huwa hana uwezo wa kubishana na bwana wake! Watawala ndiyo mabwana wa watanzania.
Mkuu katika hali hii njia ni moja tu ni kuuangusha utawala unaodumisha utumwa huu na kuweka utawala mwingine wowotw ili watawala watambue umuhi wa kura za wananchi.
Mkuu mimi sisemi kuwa chadema italeta maziwa na asali, iLa ninachokiangalia hapa ni kubadilisha watawala ili kurejesha nguvu ya utawala kwa umma wa watanzania. Watawala wajue kuwa wananchi ndo wenye nchi wanauwezo wa kumweka yeyote wanayemtaka wao, na wanaweza kumwondoa wakati wowote wakitaka wao.
Tukifikia hapo ndipo heshima itarudi na kila mtawala atafanya yaliyomatakwa ya watanzania si matakwa yake na kIkundi cha watawala wenzake.
Tunataka ccm na mafisadi wake wakae pembeni ili kurejesha nguvu ya utawala kwa umma. Tunahitaji chama kingine kitakachotawala kikijua kuwa kimewekwa na nguvu ya umma hivyo kufanya yale tu umma unataka.
Tukifika hapa watawala hawatatupa shida hata ndani ya miaka miwili tunaweza kumpiga chini na kuweka wengine.
Bila kufanya hivyo tutaendelea kujenga taifa lenye watumwa ndani ya nchi yao na kikundi kidogo cha mabwana.
Mwenye kupinga mtazamo huu atakuwa ni chizi na pengine labda yuko katika hiki kikundi kidogo cha mafisadi na mabwana wanaotaka hali hii iendelee maana kwao ni faida na wataendelea kurisishana mpaka vitukuu.
Wake up Tanzanians achana na propaganda za watawala na mafisadi eti kuipiga chini ccm na kuweka chama kingine tunaweza kuruka mkojo na kukanya mavi! Kama wanamapinduzi tuliangalie swaala la kubadilisha utawala ni kuwanyang'anya ccm na mafisadi wake nguvu ya utawala na kuirejesha
kwa umma.