Chama gani mbadala kwa CCM?

Chama gani mbadala kwa CCM?

akishiriki katika mahojiano kwenye star t.v dr benson bana amesikika akirudia mara kadhaa kwamba kwa sasa hakuna chama mbadala zaidi ya ccm.msimamo wake unajengwa na hoja kwamba ccm ilishinda urais kwa asilimia 60,ccm ina wabunge wengi,serikali za mitaa zinaongozwa na ccm(asilimia 90).[/QUOTE

cRAP, SASA TENDWA AKIKIFUTA NCHI ITAKUWA BILA VIONGOZI? WE BANA WAKATI MWINGINE UNADUMAZAA UPEVU WA FIKRA ZA MABADILIKO. UWE UNAKAA KIMYA KAMA HUNA HOJA, SI LAZIMA KILA KITU UWE NA CHA KUSEMA.
 
Ingawa daktari hakuzungumza kama mwakilishi wa REDET, tungemshauri ,kuwa kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti Mwenza wa REDET, awe anajitahidi kutoa maoni yanayo akisi hadhi na heshima ya taasis hiyo maana kauli yake yoyote anayoitoa inatafsiriwa kuwa ni kauli ya REDET.
Tufahamu kuwa REDET ya kweli ilikuwa ile ya akina Prof .Baregu , marehemu Prof.Samuel Mushi na wengine.
 
Akishiriki katika mahojiano kwenye star T.V Dr benson bana amesikika akirudia mara kadhaa kwamba kwa sasa hakuna chama mbadala zaidi ya ccm. Msimamo wake unajengwa na hoja kwamba CCM ilishinda urais kwa asilimia 60, CCM ina wabunge wengi, serikali za mitaa zinaongozwa na ccm(asilimia 90).

Aise! PhD holder wengine ni janga la Taifa. Lakini kwa Dr Benson Bana tunaweza kusema kwamba 'hawezi kukata mkono unaomlisha'
 
hata mimi nimemsikia.huyu naye ni tatizo
 
Bana hana jipya,ametumia takwimu za 2010 ambazo ni za muda mrefu,kwa nini asingetumia takwimu za Igunga?tusimshangae njaa ndo inamsumbua
 
Akiongea katika tuongee asubuhi kupitia Star Tv,yule msomi wetu wa Redet Dr Bana amesema yeye mpaka sasa ajaona chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi ya CCM,nadhani hizi ni dalili mbaya kwa wasomi wetu.Badala ya kuwasaidia watanzania kujua haki zao za msingi yeye anasema hakuna wa kuiongoza hii nchi..

Hana lolote Bana kazi yake kuwavizia akina Mage chuo, anawaza ngono tu

Benson Bana ana maana gani hasa anaposema 'mbadala'. Mbadala kwa vipi? kwa wizii? kwa kutofanya maamuzi? au kwa kuvuruga uchumi? au kwa kutotatua migogoro ya wafanyakazi? What exactly do you mean Bana? Na kwa nini REDET hawajafanya research tangu uchaguzi mkuu 2010 uishe ili watueleze public opinion iko vipi?
 
Akiongea katika tuongee asubuhi kupitia Star Tv,yule msomi wetu wa Redet Dr Bana amesema yeye mpaka sasa ajaona chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi ya CCM,nadhani hizi ni dalili mbaya kwa wasomi wetu.Badala ya kuwasaidia watanzania kujua haki zao za msingi yeye anasema hakuna wa kuiongoza hii nchi..

dokta poyoyo
 
Wanajamvi, leo nimemsikia DR. Benson Bana katika kipindi cha asubuhi Star tv akisema kuwa hajaona chama mbadala wa CCM katika kuongoza au kushika dola. Hapa ndipo naunga hoja ya kuwa wasomi wetu hapa nchini hawalisaidii taifa hili zaidi ya kutetea yale yanayowapa ulaji.

Katika kutetea hoja yake ametoa kigezo cha matokeo ya uchaguzi uliopita kama kielelezo cha CCM kukosa mbadala, lakini nilitaraji msomi kama huyu atajikita katiaka kutafakari na siyo kukurupuka kutoa sentensi bila kufikiri akidhani watanzania bado ni wa miaka arobaini na saba.

Hivi tujiulize matokeo ya uchaguzi yalikuwa ya haki maana ukiingia kwenye wavuti ya tume ya uchaguzi huyakuti yote sasa kama CCM ilishinda kihalali iweje tume ya uchagu ishindwe kuweka matokeo halisi kama sio udanganyifu.
Wasimamizi wa Uchaguzi majimboni;

Kitu kingine ambacho DR. Bana anajua kuwa wasimamizi wa uchaguzi majimbo yote ni wateule wa Raisi ambaye ni mwenyekiti wa CCM na hata majimbo waliyoshinda upinzani tuliona matokeo yalivyotolewa kwa mbinde mpaka watu waandamane amani itoweke ndo matukio yatoke.

Tume ya uchaguzi;Tume hii tuliyonayo wajumbe wake wote ni wateule wa yuleyule mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais hivi msomi huyu hajui madaraka aliyonayo rais kiasi kwamba atumie kielelezo cha matokeo ya uchaguzi pekee kama kigezo cha CCM kutokakuwa na mbadala.

Hivi raisi akimfukuza kazi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kuna atakaye hoji? Kwa maana hiyo ili mwenyekiti huyo wa tume ili kulinda kibarua chake ni lazima atomize matakwa ya bosi wake.

Uchaguzi mdogo Igunga
;Hebu tuangalie uchaguzi wa Igunga ,CCM kilitumia zaidi ya bil.17 , pamoja na kugawa chakula kwa wale wenye njaa na kukitumia ili kupata kura, hivi kama uanakubalika utatumiaje nguvu kubwa kwenye uchaguzi mdogo na baadaye ushinde kwa tofauti ya kura zisizozidi 3000 na bado useme hauna mbadala?

Namshauri DR. Bana aache kufikiri kama mototo wa darasa la nne na achambue mambo kama msomi. Angeangalia kwanza mazingira ya uchaguzi kabla ya kutumia matokeo yake kama ni kielelezo pekee kuhalalisha kukubalika kwa CCM. DR. Bana. Uwanja wako, refa we mwenyewe, ukiishinda timu pinzani utasema we ni bingwa? DR. Bana acha utani kwenye maisha ya watu!

Hao ndiyo chadema bwana hataki hata ukiwaambia ukweli kupinga ni jadi yao. ila kwa hapa nakupongeza kwa kuwaomba waelewe manaa ya neno Mbadala maana tutaruka Maji na kukanyaga matopeee
 
tatizo wasomi wanakuwa wanazungumza huku wakiwa na maslahi fulani,,, nahis bwana B Bana anaogopa kivuli chake mwenyewe na sidhani kama kweli kauli yake ina uhalisia... mzee kapitiwa katika hilo, tumsamehe
 
hivi nini maana ya 'msomi'?
 
Anachoongea ni kweli kbs,, Mpaka sasa vyama vya upinzani bd havijaonyesha mfano wa kuongoza zaidi ya kupiga kelele2,, wanachojivunia zaidi ni mwamko wa wananchi kutaka wawapigie kura lakini wamejipanga vp ktk kuendeleza taifa hili? Au ni kuwatoa madarakani ccm tuu? Mm naungana na dr. Banna kuwa bd hakuna mbadala ingawa ccm kuonyesha mapungufu katk baadhi ya maeneo lakini bd ni chama imara kwanza kinaruhusu mawazo tofauti kutoka ndani ya chama na nje ya chama chake, leo hii chama gani kinathubutu hvyo?. Kwa mfano cdm mm naona ni kama chombo cha habari na cyo chama cha siasa , kwa nn, wamekua wakihubiri matukio zaidi badala ya kueneza sera zao kwa watanzania sasa uwezo wao wa kutetea hayo wanayo yaamini unapimwa vp?. Wajipange na kama mawazo yao ni kuondoa ccm bs cy chama , kwani na ccm nao wakija na mkakati wa kuua upinzani patakuwa vp hapo kwa cc wananchi wa kawaida?
 
hao wanaotaka kupiga kura ndio wanatakiwa watoe dira, chama watakachokichagua kiwe na uwezo kimkakati kutekeleza sera zinazoreflect dira ya wenye nchi, usikosee kuelewa.
 
akishiriki katika mahojiano kwenye star t.v dr benson bana amesikika akirudia mara kadhaa kwamba kwa sasa hakuna chama mbadala zaidi ya ccm.msimamo wake unajengwa na hoja kwamba ccm ilishinda urais kwa asilimia 60,ccm ina wabunge wengi,serikali za mitaa zinaongozwa na ccm(asilimia 90).

Hili nalo janga hili....hiyo cCmaFsdi inajifilia professor Mzima anasubutu kujidanganya!! Inachekesha kweli, sio mbaya ila ukweli Ni kwamba katanguliza maslahi binafsi zaidi kuliko uzalendo AMA anahofia kibarua chake, ana target zake hvyo anahofia kuziharibu....but deep inside anajua fika ccM Tia maji Tia maji.
 
Back
Top Bottom