Chama gani mbadala kwa CCM?

Nyami2010

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
227
50
Wapendwa wana JF

Bila kujali wewe ni chama gani tafadhari nisaidie kujua:
1. Ni chama gani mbadala kwa CCM hapa Tanzania?
2. Kwa nini tunasema CCM basi (is it irrepairable)?
3. Huyo wa kushika usukani, anao ubavu kwa maana ya nguvu watu?
4. Au tunadanganywa na ushawishi wa mtu mmoja au wawili?
5. Tunapodadavua haya, angalia chama bila fulani na fulani....., itakuwaje?

Ndugu zangu: Chama ni watu makini na si bora watu! Bora niwe na wanachama watano (5) makini kuliko wanachama 5,000 ovyo, wagomvi, wahuni na wavuta bangi!

Ninahisi huko mbele tuendako tunaweza kujikuta tunajuta na kusaga meno huku tukisema; bora.....................kuliko hawa.......................:tonguez:. Watanzania tuchambue mbivu na mbichi mapema, tusifike huko!

Kwa wenzetu msiopenda kusikia msioyapenda, leteni matusi kama kawa..........:dance:
 
chama mbadala n tpp maendeleo nenda kajiunge,kama hicho hukijui pana JK SAR1(Jakaya Kikwete Salima RizOne)chagua lako nyama viwili hivyo na vyema vina katiba bomba
 
inaelekea hujui hata tulipotoka tulipo na tuendako...............think kwanza ndo upost hiyo thread yako
 
Mosi, Ni kile chama ambacho watanzania wanakipenda. chama ambacho;
Pili, Wakitangaza maandamano au mikutano ya hadhara haiwabebi watu kwa malori.
Tatu Haina tuhuma za ufisadi
nne, inakubalika zaidi na wasomi kwa sababu wao ndo wanaojua ukweli daima.
Tano, Viongozi wake wako tayari kutaja mafisadi kwa gharama yo yote bila kuogopa kufa
Sita, ni kile chama ambacho mafisadi wa CCM wameshindwa kukiweka mifukoni mwao.
Saba, Chama ambacho watanzania waliikubali sera yake 2010 kikachakachuliwa na usalama wa Taifa
Nadhani sasa unaweza kupata jibu mwenyewe.
Wish you a nice day.
 
Akiongea katika tuongee asubuhi kupitia Star Tv,yule msomi wetu wa Redet Dr Bana amesema yeye mpaka sasa ajaona chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi ya CCM,nadhani hizi ni dalili mbaya kwa wasomi wetu.Badala ya kuwasaidia watanzania kujua haki zao za msingi yeye anasema hakuna wa kuiongoza hii nchi..
 
Redet imekua ni taasisi ya wasomi wetu kutafutia vyeo..so sishangai kwa comment yake! Ukimskiliza utaskitika jinsi alivyojenga hoja yake.
 
akishiriki katika mahojiano kwenye star t.v dr benson bana amesikika akirudia mara kadhaa kwamba kwa sasa hakuna chama mbadala zaidi ya ccm.msimamo wake unajengwa na hoja kwamba ccm ilishinda urais kwa asilimia 60,ccm ina wabunge wengi,serikali za mitaa zinaongozwa na ccm(asilimia 90).
 
...Dr Bana ...umeaibisha wasomi na usomi....,jibu ulilotoa lime base ..kwenye matokeo ya uchaguzi wa 2010..,,,

Mimi nilidhani umeongea "sasa",ukiwa na Ripoti ya kiutafiri ya sasa......

Je kwa sasa kwa wimbi la uongozii uliopo Sasa hakuna chama mbadala?
Kwa mfumko mkubwa huu asilimia ishirini wa bei hakuna chama mbadala...
Kwa uwezo wa hoja na kiongozi na hata kwa ushauri wanaoutoa kwa serikali ...hakuna chama mbadala...?
Kwa uchumi huu mbovu?? Kwa migomo hii ??
Unaongelea nguvu ndogo ya upinzania.....kwenye katiba ya sasa? Tume ya uchaguzi ?

Nadhani tuna haja ya kuwa na Shaka na maoni ya daktari Bana,,...
 
huenda ameongea kifalsafa zaidi. CDM inaweza kuchukua madaraka lakini ni mbadala wa CCM au na yenyewe itakuwa ni yaleyale ya CCM? CDM imejipangaje kuchukua nchi ama ni kwa sababu tu CCM inaboronga basi watu wakakimbilia CDM? Unaweza kuruka majivu ukakanyaga moto! Tungetambua kwanza muktadha wa neno mbadala.
 
Redet imekua ni taasisi ya wasomi wetu kutafutia vyeo..so sishangai kwa comment yake! Ukimskiliza utaskitika jinsi alivyojenga hoja yake.

Redet haijawahi kufanya kazi kwa maslahi ya nchi. Mara zote wamekuwa wakifanya kazi za propaganda kwa niaba ya ccm. Dr. Bana amewekwa pale na ndugu yake Mukandara, ambaye kwa kweli ameshindwa kuiongoza UDSM kama msomi. Mtakumbuka wakati ule wa uchaguzi wa 2005 na 2010 jinsi taasisi hiyo ilivyotumika. Hata hivyo walipata aibu mara zote kwani maeneo yote ya wasomi ccm ilipata kura kiduchu tu za wale walamba magamba.

Tusimshangae, tumuombee.
 
Akiongea katika tuongee asubuhi kupitia Star Tv,yule msomi wetu wa Redet Dr Bana amesema yeye mpaka sasa ajaona chama mbadala cha kuongoza nchi zaidi ya CCM,nadhani hizi ni dalili mbaya kwa wasomi wetu.Badala ya kuwasaidia watanzania kujua haki zao za msingi yeye anasema hakuna wa kuiongoza hii nchi..

Hiyo ndiyo ubaya wa elimu ya kukariri inayokupa cheti na siyo knowledge, pamoja ma elimu yake yote anashindwa kusoma hata alama za nyakati? Au anaongea kuwafurahisha watu fulani?
 
Huyu ni kibaraka mkuu wa CCM anatafuta madaraka kwa hali na mali,usomi wake upo wapi,anawaaibisha wasomi wa nchi hii.
 
huenda ameongea kifalsafa zaidi. CDM inaweza kuchukua madaraka lakini ni mbadala wa CCM au na yenyewe itakuwa ni yaleyale ya CCM? CDM imejipangaje kuchukua nchi ama ni kwa sababu tu CCM inaboronga basi watu wakakimbilia CDM? Unaweza kuruka majivu ukakanyaga moto! Tungetambua kwanza muktadha wa neno mbadala.

Nadhani neno mbadala ni kwamba kuwepo kwa chama kingine madarakani pengo la ccm litaonekana kwa upande wangu litaonekana megative way mfano mafisadi hatutawasikia tena ndani ya serikali wakitamba mitaani kuwa ni wazalendo kwa kujiuzulu, mikataba fake haitakuwepo na iliyopo itafumuliwa upya, migomo na maandamano hayatakuwepo, katiba na sheria ya nchi itafuatwa, bomu linalosubiriwa kulipuka muda wowote litateguliwa (ukosefu wa ajira kwa vijana), siasa za kudanganyana fitna na siasa uchwara havitakuwepo na vitu vingine vingi
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom