Chama gani mbadala kwa CCM?

Chama gani mbadala kwa CCM?

Tanzania tuna vyama vyama siasa vya upinzani takribani 30.

Lakini hadi sasa bado hatujapata chama mbadala ambacho kitambana na CCM na hivi vingine vimuunge mkono chama kimoja.

Ikumbukwe ya kwamba mwaka 1995 NCCR ilitingisha kupitia Mrema walipambana wakashidwa.

2000 na 2005 CUF kupitia Lipumba walipambana lakini wakashidwa

2010 na 2015 CHADEMA kupitia Lowassa walipambana mara mbili wakashidwa.

2020 inakaribia hadi sasa sijui mawazo ya upinzani wamejipanga vipi kushinda.

Lakini pia kama vyama vyote vimeshidwa ni chama gani mbadala wa CCM ikizingatiwa vyama vyote vimeshindwa.
Labda wamjaribu Dr Shika!
 
Samahani mkuu ,nakushauri pakuwa mavi kwenye kichwa chako then ndiyo uongee. Sema hivi tuweke tume huru na tutenge polisi na ccm ndiyo uje ongee upoyoyo wako.
Acha kulazimisha MTU hadi kumtukana, ili afikirie kama wewe, kamwe.
Na mjiheshimu, mtaheshimiwa.
 
Kwani mleta mada huna habari kuwa ccm haijawahi kushinda kokote? Sema wanatumia dola kukwapua kura za wapinzani, hakuna chama pinzani chenye dola ndiyo maana huwezi linganisha kati ya ccm na upinzani. Lakini jua wananchi wa Tanzania wengi hawana hamu na ccm sema njia ya kuitoa ndiyo hawana mana kwa sanduku la kura wote tunashuhudia yanayotokea. Mungu ibariki Africa na Mungu ibariki Tanzania kwa pamoja ccm itashindwa
 
Kwa kipindi kirefu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi tumeshuhudia uanzishwaji wa vyama lukuki lakini vyama hivi vingi vimekuwa kama Mali ya mtu binafsi,tunaweza tusikubaliane lakini sisi sote ni mashahidi mfano Chama cha UDP cha mzee Cheyo, TLP cha mzee Lyatonga, na vingine vingi.ukiviangalia huoni vikisimama kama taasisi bali vipo kama Mali ya mtu.chama cha CUF kimeendelea kuwepo lakini uhai wake unategemea eneo moja la nchi Pemba, bila pemba hakuna CUF huku bara ipo tu mradi na sote tunajua.Chadema kimejitahidi kuenea kwenye sehemu sehemu za bara lakini kule zanzibar hakipo kabisa.katika Hali kama hiyo na kwa kuangalia katiba yetu Chama pekee kinachobaki kuwa na sifa pande zote mbili za muungano ni ccm.Katika Hali kama hiyo wote ni mashahidi kuwa vyama hivi havijajengwa katika misingi imara ya kushika nchi hasa kwa katiba hii ya sasa.Tunaweza kuilalamikia ccm lakini ni ukweli usiopingika kuwa bado hatujawa na Chama kilichosheheni barabara pande zote na nchi nzima kwa maana ya uwepo wake zaidi ya ccm.kwa sababu hiyo bado hatuna Chama mbadala kwa mfumo,Sera na uwepo wake.vyama vya upinzani vinapaswa kuungana na kuunda Chama imara kinachoweza kushika dola.kwa mtizamo wangu naona bado hakuna Chama mbadala wa kushika dola na kuongoza nchi.
 
Chadema mhimili wake ni wafanyabiashara wa kichaga wakati CUF muhimili wake ni wafanyabiashara wa kipemba,Muungano wa UKAWA ulikuwa muungano wa wafanyabiashara wa kipemba na kichaga kutaka kuchukua dola.Baada ya mafanikio yao kwenye biashara waliona hiyo haitoshi wachukue na dola kabisa wakitaka hata kuuza nchi wauze!!!!.Maskini wanyonge ambao ndio wengi wakawakataa wakawapiga chini .As long as Chadema na CUF vinabaki kuwa vyama vya mabwanyenye na matajiri wafanyabiashara wa kichaga na kipemba wasau kushika dola
 
Chadema kinaweza kuwa chama mbadala iwapo wataacha Viroba.
 
Chadema mhimili wake ni wafanyabiashara wa kichaga wakati CUF muhimili wake ni wafanyabiashara wa kipemba,Muungano wa UKAWA ulikuwa muungano wa wafanyabiashara wa kipemba na kichaga kutaka kuchukua dola.Baada ya mafanikio yao kwenye biashara waliona hiyo haitoshi wachukue na dola kabisa wakitaka hata kuuza nchi wauze!!!!.Maskini wanyonge ambao ndio wengi wakawakataa wakawapiga chini .As long as Chadema na CUF vinabaki kuwa vyama vya mabwanyenye na matajiri wafanyabiashara wa kichaga na kipemba wasau kushika dola
20% ya watanzania ni mbumbumbu hawajuhi kusoma wala kuandika(milioni 12).. ndio mtaji wa CCM...UKAWA watapata tabu sana kueleweka ...
 
Noise,..

Kama mnaamini upinzani haukubaliki kwa wananchi, embu acheni uchaguzi uwe huru tuone kama mtashinda.

Sisiemu wanashinda kwa udanganyifu mwingi, siyo kwa kuchaguliwa na wananchi
 
20% ya watanzania ni mbumbumbu hawajuhi kusoma wala kuandika(milioni 12).. ndio mtaji wa CCM...UKAWA watapata tabu sana kueleweka ...
Afu ndo wapiga kura mana wasomi hawapigi kura kwa wingi
 
Noise,..

Kama mnaamini upinzani haukubaliki kwa wananchi, embu acheni uchaguzi uwe huru tuone kama mtashinda.

Sisiemu wanashinda kwa udanganyifu mwingi, siyo kwa kuchaguliwa na wananchi
Nchi haifanyiwi majaribio hata kidogo.nchi waachiwe Chadema ambayo ukiwaangalia wote huoni viongozi imara na taasisi imara ya kuimili dola
 
Nchi haifanyiwi majaribio hata kidogo.nchi waachiwe Chadema ambayo ukiwaangalia wote huoni viongozi imara na taasisi imara ya kuimili dola
Pole sana sister go back to school
 
Back
Top Bottom