Chama Cha Wananchi (CUF) kuzindua kongamano la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi Desemba 20, 2020

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20201203_131435_640.jpg


CUF CHAMA CHA WANANCHI

Desemba 20,2020 kitazindua rasmi kongamano la kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Kongamano hilo litafanyika katika ofisi kuu ya chama BUGURUNI .

MWANACHI, MWANACHAMA WA CUF WOTE MNAKARIBISHWA.
 
Fursa ya kupata Katiba mpya mliharibu ninyi wanasiasa baada ya kususia ushiriki kwa sababu za kibinafsi ambazo wananchi hawakuwatuma seuze kongamano hilo ambalo bila shaka ni kichaka cha kujifariji.

Tume huru ni ipi? kama tume itaundwa na wajumbe toka vyama washirika wa siasa vilivyosajiliwa hiyo sio tume huru tena ila ni kutengeneza kikundi cha mabishano kwa kuzingatia ushabiki wa itikadi. Kama tume itaundwa kutokana na watu wenye taaluma kwa kuomba nafasi za kazi basi tutegemee mamluki wengi kuingizwa humo ili malengo ya upande wenye nia OVU ufanikishe zoezi hilo.

Duniani kote hakuna tume huru zote ziko compromised ila ulimbukeni wa baadhi ya wanasiasa wanadhani ndio itakuwa nafuu kwao kukwea ngazi kufika juu ya kilinge.
 
Back
Top Bottom