Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.
Hizi kwa sisi wenyewe uelewa mdogo,tunazichukulia kama ni kauli za uoga na kujilinda,watawala chini ya CCM wanaelewa ni kwa kiasi gani CHADEMA wameshaingia na kuteka hisia za mamilioni ya Watanzania!uungwaji mkono wa CHADEMA umekua mkubwa katika kila idara hata zile za ulinzi na usalama!ni ukweli usiofichika kua,consequencies za kuifuta CHADEMA itakua ni kubwa mno kuliko kuindoa CCM kwenye sanduku la kura!ilo lipo wazi hata lipingwe vipi!hata huyo Tendwa analielewa ilo,labda amekupa hayo maneno Pasco ili kuifuraisha nafsi yake tu!bad enough ni Judge gani ambae anakaa pembeni/kijiweni na mtu binafsi na akaanza kujengea hoja kitu kilichopo mahakamani,kukitolea uamuzi na maamuzi atakayochukua yeye kama msajili?hiki ni kichekesho sana!
 
Ama kweli nimeamini sikio la kufa halisikii dawa. Pia nimeelewa ni kwa nini bwana tendwa anaendelea kuwa ofisini hata kama mda wake wa kuwa ofisini umeisha. Nawaambieni tendwa yupo ofisini kusubiri hukumu ambayo wameshaandika iliakifute chama cha CHADEMA hukumu amboyo naamini haitakuwa ya haki kwa kuwa wameandika kabla ya ushahidi wa kila upande kutolewa. Lakini nawaambieni enyi mnaomwabudu MUNGU kuwa alilopanga MUNGU mwanadamu hawezi kupangua. Nasema hivi kama CHADEMA kimekuwepo kwa mpango wa MUNGU basi hamna awaye yote chini ya mbingu anayeweza kukifuta.

Na kama CHADEMA siyo mpango wa MUNGU basi hata mwaka huu hawamalizi watakuwa wameshafutwa. Aliyeleta uzi huu amekuja kupima upepo kwenye jukwaa na wakigundua kuna upepo wa kimbunga hiyo hukumu ambayo wameshaandika wataifutilia mbali na ndiyo kitakachotokea. MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
mwalimu wangu wa uraia amewahi kuniambia maneno haya: "bangi ukivuta leo itakusumbua na kukuendesha miaka 20 ijayo".. Amini usiamini,.. Hapa tz kuna ofisi zinaendeshwa kwa nguvu ya bangi za miaka 20 iliyopita.
tendwa mbona bange alivuta siku nyingi tu na bado anaendelea kupiga msuba.
 
You can take africans out of africa, but you can't take africa out of africa. So kukifuta chadema ni ndoto za mchana tena za mtu anayeota huku anatembea
 
mkuu ze marco, kuwa bonafide genuine ni one thing!, addmissibility as evedence before the court of law is something else and establishing 'actus reus' na 'mens rea' is something else and finally proving beyond reasonable doubt is quite another! And its not that simple kama establishing the bonafide genuine kwa macho tuu!.
Pasco

pasco! Kuna siku huwa unakuja vizuri humu katika reasoning. Lakini kuna siku unakuja ki mwigulu kabisa. Huwa nakushangaa sana. Sasa wewe umeenda kwa tendwa kufanya maongezi yasiyo rasmi kisha ukatumia maneno maguumuu ya kisheria kwa mzee ambaye ni "old dog who cant be taught new tricks of hunting" sasa alielewa kwanza unaongelea nini? Kama analinda katiba, ulisahau nini kumuuliza yeye "ameibaka katiba" mara ngapi na kui "castrate" mara ngapi? Kuhakikisha kwamba vyama mbadala vya sisiemu havifurukuti kwake? Ni mara ngapi amepuuzia madai ya kweli ya wana mbadala yalipopekwa kwake? Pasco kwanini umeenda kichwa kichwa kisha unakuja na ujinga huu? Umeshaanza kupokea mshahara toka kwa nape na mwigulu? Kwa nini unaitetea jf? Jf haipaswi kutetewa na watu inajitosheleza yenyewe. Ni sawa na kumtetea mungu wakati mungu anapaswa kujitetea mwenyewe ( hapa inategemea kama unasoma bible vema au kama unahudhuria ibada vema - ninavokujua wewe hata kusali hupendi ) sasa nakutuma tena nenda kwa tendwa muulize alielewa maneno ya kilatini ulotumia au alijibu kama walivyozoea kujibu wenzake. Tafadhali njoo tena humu uje useme kitu.
 
Teh!teh!teh! Utajuta kukisajili CHADEMA na huwez kukifuta kwani nisawa na kumzaa mtoto umlee, akue nakujtambua kisa hakubaliani na utahira wa wazazi waamue kumuuaa,mzee fikiria kwamakin jinsi ya kunisaidia CHADEMA chama ambacho umekisjili wewe mwenyewe. Akili za mbayu wayu changanya na zako.
 
Ni kweli inaweza kuwa ngumu de jure, lakini kwa vile chadema wamejimilikisha kesi binafsi ya Lwakatare kwahiyo de facto hukumu ya Lwakatare inakuwa hukumu ya chadema.

Chadema kitaonekana chama cha ajabu kuliko vyote duniani iwapo Lwakatare akikutwa na hatia wataamua kumkana. Kwahiyo mkanda ukishathibitika kisheria kuwa ni "bonafide genuine" basi chadema wanakuwa na kesi ya kujibu kama chama. Na hapo ndipo Tendwa atakuwa standby na kalamu yake nyekundu...
Vijana inabidi watafute sehemu nyingine ya kujipatia viroba mapema
 
TUKO tatizo la
Ze Marcopolo ufahamu wake kuhusu MUNGU wa Mbinguni upo chini sana.anajua sana mipango ya shetani.Ndungu Ze Marcopolo hakuna watu waliopata taabu,shida,dhiki ,maumivu kama watu wa MUNGU.Fuatilia habari za Mitume na Manabii maisha yao na aina ya vifo walivyokufa katika vitabu vya MUNGU.Nakupa mfano mmoja tu kati ya mingi Wana wa Israeli walikaa utumwani misri kwa miaka 400.

Kwa hiyo Dr. Slaa ndio mtume? Kweli bavicha mna mambo!!!
 
Mtu yeyote atakayefurahia chadema kufutwa atakuwa haipendi nchi yetu. Lakini hii haimaanishi kuwa chadema ipewe licence ya kuvunja sheria zenye adhabu ya kufutwa. Kinachojadiliwa hapa ni iwapo chadema itakutwa na hatia ya kupanga na kutekeleza utekaji.

Halafu hii tabia ya wafuasi wa chadema kuonyesha kuwa Mungu kachagua chadema inaonyesha mapungufu makubwa sana kwenye fikra. Hii yote ni kutaka sympathy based on faith, jambo ambalo modern politics linalikataa kwa sababu ndio linalozaa wanasiasa desperate wanaotumia misingi ya imani kuomba kura. Mungu hana chama Tanzania, na hata angekuwa nacho kisingekuwa chadema. Chama cha Mungu hakiwezi kukaa miaka 21 kwenye upinzani.
kaka ni modern politics zipi unazozungumzia wewe? za kutengenezeana kesi za ughaidi? za matusi ya nguoni ndani ya vyombo vya kutunga sheria? hatujawahi kuona CCM ikihaha ku-deal na vyama vya msimu.
 
Ndugu yangu Pasco

Sio kila apumuae ni mzima,

Msajili wa vyama vyasisa hana authority ya kufuta chama cha siasa,

Yeye ni mlezi wa demokrasia na halazimishi chama kimsikilize yeye!

Soma vizuri katika inasemaje juu ya usajili na ufutaji wa vyama vya kisiasa nchini!

Tuwe makini sana kukurupuka na kutamka maneno ya aina hii!

Angelikuwa na mamlaka hayo leo hii angeshakifuta chama cha mapinduzi ambacho hakijasajili katika mfumo wa vyama vingi!

Ulishindwa kumhoji kama analo faili la usajili wa ccm?
 
mkuu pasco mimi binafsi sioni kwani umeleta mada hii kwa kumnukuu msajili na kuilenga chadema wakati miongozi ya msajili inasema hivyo kuwa chama kitakachothibitika na uvunjifu wa amani kitafutwa iwe ccm au chama chochote tofauti na ulivyobainisha hapa .kwa upande mwingine kama una chuki binafsi na chama cha demokrasia na maendeleo ya watanzania hapa ujiweke wazi .Napata tabu kidogo kuelezea jinsi sababu zinavyotafutwa ili chama fulani kifanane nazo .tumeona suala la udini,tumeona suala la ugaidi sasa karata iliyobaki ni kitisho cha kufuta .serikali ina mihimili mitatu ,bunge ,mahakama n serikali hapa mihimili hii inatakiwa kusiwepo na muingiliano kiutendaji .tunaona serikali inaamua nani awe spika ,nani awe jaji mkuu ,jaji mkuu huteuliwa na rais ,vivyo hivyo kwa wengine .tunapoona serikali inachukua nafasi kubwa katika mihimili hii mitatu ya uwajibikaji tunakosa imani ,imani tunaikosa kama msajili ambaye ni mlezi naye anapokuwa mfurukutwa wa chama fulani na hivyo kumnyima hadhi ya kuwa msajili .Katika hili katiba mpya tunapaswa tuangalie hili huyu msajili apatikane vipi ,atoke wapi uraiani au wapi ,pia kwa kumalizia nakosa imani na pasco anatumika kuhujumu baadhi ya vyama vya siasa ,ushahidi rudia kusoma andiko lake hapo juu nawasilisha
 
Tendwa hana kazi kwa hiyo akili yake inaweweseka; Tunafahamu kwamba hiyo ni moja ya tactics katika survival kit ya CCM kama wataendelea kusambaratishwa kwenye majukwaa;

But Let him try it, lakini ajue fika kwamba anaweza kufuta CHADEMA jina; afterall what is in a name?! lakini katu hawezi kuifuta CDM katika roho na akili za watanzania ambao kila kukicha wanazidi kujitambua na wanataka kujikomboa kutokana na udhalimu wa chama hicho tawala.

Maskini Tendwa hajui kwamba kutokana na dictates za historia; it is only naturala kwamba CCM itakufa sooner rather than later, it is a natural phonomenon. kama amesahau aangalie nchi zote zinazotuzunguka ni chama gani cha uhuru ambacho bado kiko madarakani au kina uhai!

KANU (Kenya); UNIP (Zambia); MCP (Malawi) UPC (Uganda); just to mention a few! hiyo Tendwa ndiyo destiny ya CCM unataka hutaki. period
 
Ndugu yangu Pasco

Sio kila apumuae ni mzima,

Ulishindwa kumhoji kama analo faili la usajili wa ccm?

Mkuu, hili swali hawezi kulijibu, iwe ni huyo mganga njaa ana mzee Tendwa,
kichwa na habari kinatofatiana na yaliyomo, ndio waandishi wetu hawa...

Ok amuulize pia kwa umri wake, ni kwanini Tendwa hataki kuachia ofisi ya umma?
 
Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa
Hivi msajili wa vyama kwa mujibu wa katiba ya nchi hii anaruhusiwa kujiunga na chama chochote cha siasa?
 
Hivi ndugu Pasco ulipokuwa unaongea ( siyo kuzungumza kama ulivyodai wewe Mwenyewe ! ) na John Tendwa unadhani kwa umri alionao ( yaani UZEE ) , Bado Uwezo wake wa Kufikiria uko SAWASAWA ?
 
Ni kweli inaweza kuwa ngumu de jure, lakini kwa vile chadema wamejimilikisha kesi binafsi ya Lwakatare kwahiyo de facto hukumu ya Lwakatare inakuwa hukumu ya chadema.

Chadema kitaonekana chama cha ajabu kuliko vyote duniani iwapo Lwakatare akikutwa na hatia wataamua kumkana. Kwahiyo mkanda ukishathibitika kisheria kuwa ni "bonafide genuine" basi chadema wanakuwa na kesi ya kujibu kama chama. Na hapo ndipo Tendwa atakuwa standby na kalamu yake nyekundu...

Hivi ile kesi ni who against who JAMHURI VS CHADEMA au against Lwakatare? mi naona kama watu wanabwabwaja tuuuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom