Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Kufutwa Kwa Mujibu wa Katiba!... Endapo ...!

Status
Not open for further replies.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Wanabodi,

Iwapo itathibitika pasipo shaka, (proven beyond reasonable doubt), kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi toka ndani ya daftari la vyama vya siasa, (scraped from the book of political parties), mara moja na bila huruma yoyote!.

Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifyonyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia mara kwa mara, ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.

Katika maongezi yetu kuhusu hali ya siasa hali ya siasa nchini, niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana " proved beyond reasonable doubt!" by "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA walihusika kwa kujua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili wa vyama nchini, Jaji John Tendwa, atakuwa hana option nyingine, bali kukifuta rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini, yaani CHADEMA, toka ndani ya daftari la vyama vilivyosajiliwa, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo sheria ya vyama vya siasa inavyoelekeza kwa mujibu wa katiba ya nchi hii! ambayo yeye ameapa kuilinda.

Kwa kifupi amemaanisha iwapo chama cha siasa kitathibitika kufanya ugaidi, kitafutwa!.

Hata hivyo nikadadisi zaidi, iwapo tuhuma za ugaidi zatathibitika kufanywa na chama tawala CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Baada ya swali hilo, kwanza Msajili alisita kidogo na baadae kusema kuwa kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa ya ugaidi, hatakifuta right away eti kwa sababu ni chama tawala!, kukifuta chama tawala ni kuvunja serikali iliyopo madarakani!, CCM kikifanya ugaidi, hata kivunja, bali atakipeleka mahakamani ili mahakama ndio itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!.

Hii inamaanisha as of now, Tanzania bado hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali iliyopo madarakani nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni serikali dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata chama hicho kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.

My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio ya double standards za mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kustahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake kwa kuvifuta, watu wakaishia kupiga kelele na kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki, waki vyama vingine, vikifanya makosa yale yale, vikiachwa eti kwa sababu ni chama tawala!.

Pia nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na baadhi ya wachangiaji ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa serikali na viongozi wa taifa hili!. Nilimwambia hiyo ndio maana halisi ya social forums, watu kujiachia watakavyo!.

Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha kwa watu wote wakiwemo viongozi wa kitaifa!.

Najua kuna wenzetu humu, kwao JF ni just their favorite past time na huja humu wakati hawana shughuli au kitu kingine chochote cha kufanya!, nawaomba mtuhurumie sisi ambao kwetu JF ni zaidi ya nyumbani kwetu, jf ni sebuleni kwetu, jf ni chumbani kwetu, jf ni kitandani kwetu, tunashinda JF, tunakula jf, tunalala JF, tunaamka JF, in short kwa sisi wengine wetu, jf ndio kila kitu kwetu, tunaiishi JF, yaani kwetu JF is our life that we are living for!.

Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.
 
Kumuita fisadi/dhaifu yeyote yule kutokana na matendo yake si tusi. Miaka ya nyuma kulikuwa na wahujumu uchumi hawa pia waliitwa hivyo kutokana na matendo yao ya kuhujumu uchumi, labda ingekuwa vizuri ungemuuliza hayo matusi anayozungumzia ni matusi yepi.
 
Kwavile mkanda ni bonafide genuine na kwavile chadema wamekataa kujitenga na mambo binafsi ya Lwakatare, basi Tendwa asilaumiwe huko mbeleni...
Mkuu Ze Marco, kuwa bonafide genuine ni one thing!, addmissibility as evedence before the court of law is something else and establishing 'actus reus' na 'mens rea' is something else and finally proving beyond reasonable doubt is quite another! and its not that simple kama establishing the bonafide genuine kwa macho tuu!.
Pasco
 
Anajidanganya huyu Mkuu wanadhani Tanzania ni nchi ya chama cha magaidi. Watumie sababu zisizo na kichwa wala miguu kukifuta CHADEMA baada ya propaganda zao za chama cha kidini, kikabila, chenye kutaka kuleta umwagaji wa damu nchini na cha magaidi kushindikana. Kama wanadhani kukifuta CHADEMA ni rahisi kihivyo wanajidanganya sana.

Mwalimu wangu wa uraia amewahi kuniambia maneno haya: "Bangi ukivuta leo itakusumbua na kukuendesha miaka 20 Ijayo".. Amini usiamini,.. Hapa TZ kuna ofisi zinaendeshwa kwa nguvu ya bangi za miaka 20 iliyopita.
 
Pasco,
uvivu wako wakusoma nakukubali cheap answers utakupa tabu sana ktk maisha siku sheria zipo wazi msajili hana
ubavu wa kufuta chama na kama angekuwa nao angeshafanya hivyo siku nyingi hana ubavu huo. msajili inambidi aende mahakamani kabla alivyozungumzia kwy issue ya CCM kuishawishi mahakama kuhusiana na hayo anayowashutumu nao na mahakama ikubaliane nae kitu amabacho hana ubavu nacho ndio maana unamuona amekuwa kama junk dog kupiga kelele tu na mara nyingine kudhalilishwa na tume ya uchaguzi kwa kuingilia kazi zisizo za kwake.
kwa ufupi ofisi yake ingebidi ifutwe kwani ina limit uhuru wa watu kujumuika kwa namna wanavyotaka wenyewe.
 
Mkuu Ze Marco, kuwa bonafide genuine ni one thing!, addmissibility as evedence before the court of law is something else and establishing 'actus reus' na 'mens rea' is something else and finally proving beyond reasonable doubt is quite another! and its not that simple kama establishing the bonafide genuine kwa macho tuu!.
Pasco

Ni kweli inaweza kuwa ngumu de jure, lakini kwa vile chadema wamejimilikisha kesi binafsi ya Lwakatare kwahiyo de facto hukumu ya Lwakatare inakuwa hukumu ya CHADEMA.

CHADEMA kitaonekana chama cha ajabu kuliko vyote duniani iwapo Lwakatare akikutwa na hatia wataamua kumkana. Kwahiyo mkanda ukishathibitika kisheria kuwa ni "bonafide genuine" basi CHADEMA wanakuwa na kesi ya kujibu kama chama. Na hapo ndipo Tendwa atakuwa standby na kalamu yake nyekundu...
 
Mkuu Ze Marco, kuwa bonafide genuine ni one thing!, addmissibility as evedence before the court of law is something else and establishing 'actus reus' na 'mens rea' is something else and finally proving beyond reasonable doubt is quite another! and its not that simple kama establishing the bonafide genuine kwa macho tuu!.
Pasco

You keep repeating this bonafide genuine bullshit....what exactly is it?

And FYI, it's bona fide as in two words and not 'bonafide'.
 
WTF?

So, if bonafide =genuine

And bonafide genuine = genuine indeed

Is genuine = indeed?

NN its not mathematics, its communication skills. Languages do evolve, ndio maana umeandika WTF na nimekuelewa ingawa hilo sio neno rasmi ila umeweza kulitumia kucommunicate. Kwahiyo usingoje yule aliyeanzisha WTF aje akuanzishie na bonafide genuine au usingoje mpaka usikie fox news ndio uamini kuwa inaweza kutumika kucommunicate...
 
NN its not mathematics, its communication skills. Languages do evolve, ndio maana umeandika WTF na nimekuelewa ingawa hilo sio neno rasmi ila umeweza kulitumia kucommunicate. Kwahiyo usingoje yule aliyeanzisha WTF aje akuanzishie na bonafide genuine au usingoje mpaka usikie fox news ndio uamini kuwa inaweza kutumika kucommunicate...

WTF is just an abbreviation for' What the f*$k'. Just like USA is for 'United States of America'.

Sasa bonafide genuine ndo kitu gani hicho? Kwanza hamna neno "bonafide". Kuna maneno 'bona fide'.

Ni communications skills za wapi hizo? Ukiniambia ni suala la 'style' hapo naweza kukukubalia.

Lakini communications skills na logic? Nah bruh!

It's just like saying ‘They spoke in turn, one after the other.' It's tautological.
 
Ni kweli inaweza kuwa ngumu de jure, lakini kwa vile chadema wamejimilikisha kesi binafsi ya Lwakatare kwahiyo de facto hukumu ya Lwakatare inakuwa hukumu ya chadema.

Chadema kitaonekana chama cha ajabu kuliko vyote duniani iwapo Lwakatare akikutwa na hatia wataamua kumkana. Kwahiyo mkanda ukishathibitika kisheria kuwa ni "bonafide genuine" basi chadema wanakuwa na kesi ya kujibu kama chama. Na hapo ndipo Tendwa atakuwa standby na kalamu yake nyekundu...
Nyinyi kweli magamba,yunaweza kuthubutu kuwaita sikio la kufa halisikii dawa.

Itawrzekanaje hsdi sasa smbapo,jaji mkuu wa mahakama wa mahakama kuu,keshafuta shitaka la pili,la tatu na la nne ambayo ndiyo yalkkuwa ya ugaidi na kabakiza shitaka moja tu la kwanza,ambalo ni la jinai ya kawaida,nyinyi muendelee kumwita,Lwakatare kuwa ni gaidi??!!

Vile vile inafahamika beyond reasonable doubt,kuwa,msajili wa vyama,John Tendwa,ni kada wa CCM,kwa hiyo utekelezaji wa majukumu ya kali siku,yana maelekezo kwa kiasi kikubwa toka Lumumba.

Ni dhahiri pia kwa sasa,wishes kubwa ya Tendwa na CCM,ni kuhakikisha wanaifuta CHADEMA,before 2015,kwa kuwa hiiyo ndiyo option pekee iliyobaki,kama wanataka kuendelea kutawala,baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Lakini CCM wanachosahau ni kuwa kuna tofauti kubwa,kati ya matakwa ya binadamu,na mapenzi ya Mungu.

Yeye Tendwa na maCCM,wenzake,wangetamani hata lkesho,wawe tayari weshaifuta CHADEMA,from among the registered political parties in our country,lakini lea kuwa Mwrnyezi Mungu,bado anailinfa CHADEMA,hasa ukizingatia ndiyo chama pekee hapa TZ,kwa sasa kinachosimamia kwa dhati maslahi ya wanyonge,wa nchi hii,basi CCM,watambue kuwa hiyo ndoto yao ya kuifuta CHADEMA,haitatimia kamwe!!
 
Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu wa Chadema, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi, scraped from the book of political parties, mara moja na bila huruma yoyote!...
Pasco, hapo ni 'itathibitika' au unamaanisha 'endapo itathibitika'? Kwamba Tendwa ameshajua kuwa itathibitika au ametoa condition kuwa iwapo itathibitika?
 
Nyinyi kweli magamba,yunaweza kuthubutu kuwaita sikio la kufa halisikii dawa.

Itawrzekanaje hsdi sasa smbapo,jaji mkuu wa mahakama wa mahakama kuu,keshafuta shitaka la pili,la tatu na la nne ambayo ndiyo yalkkuwa ya ugaidi na kabakiza shitaka moja tu la kwanza,ambalo ni la jinai ya kawaida,nyinyi muendelee kumwita,Lwakatare kuwa ni gaidi??!!

Vile vile inafahamika beyond reasonable doubt,kuwa,msajili wa vyama,John Tendwa,ni kada wa CCM,kwa hiyo utekelezaji wa majukumu ya kali siku,yana maelekezo kwa kiasi kikubwa toka Lumumba.

Ni dhahiri pia kwa sasa,wishes kubwa ya Tendwa na CCM,ni kuhakikisha wanaifuta CDM,before 2015,kwa kuwa hiiyo ndiyo option pekee iliyobaki,kama wanataka kuendelea kutawala,baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Lakini CCM wanachosahau ni kuwa kuna tofauti kubwa,kati ya matakwa ya binadamu,na mapenzi ya Mungu.

Yeye Tendwa na maCCM,wenzake,wangetamani hata lkesho,wawe tayari weshaifuta CDM,from among the registered political parties in our country,lakini lea kuwa Mwrnyezi Mungu,bado anailinfa Chsdema,hasa ukizingatia ndiyo chama pekee hapa TZ,kwa sasa kinachosimamia kwa dhati maslahi ya wanyonge,wa nchi hii,basi CCM,watambue kuwa hiyo ndoto yao ya kuifuta Chadema,haitatimia kamwe!!

Mtu yeyote atakayefurahia CHADEMA kufutwa atakuwa haipendi nchi yetu. Lakini hii haimaanishi kuwa CHADEMA ipewe licence ya kuvunja sheria zenye adhabu ya kufutwa. Kinachojadiliwa hapa ni iwapo CHADEMA itakutwa na hatia ya kupanga na kutekeleza utekaji.

Halafu hii tabia ya wafuasi wa CHADEMA kuonyesha kuwa Mungu kachagua CHADEMA inaonyesha mapungufu makubwa sana kwenye fikra. Hii yote ni kutaka sympathy based on faith, jambo ambalo modern politics linalikataa kwa sababu ndio linalozaa wanasiasa desperate wanaotumia misingi ya imani kuomba kura.

Mungu hana chama Tanzania, na hata angekuwa nacho kisingekuwa CHADEMA. Chama cha Mungu hakiwezi kukaa miaka 21 kwenye upinzani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom