Chalinze yapata hati mfululizo kwa kuwa kinara ukusanyaji mapato kimkoa, kitaifa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Halmashauri ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani yenye Mbunge wake Ridhiwani Kikwete, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, leo Ijumaa Novemba 24, 2023 imetunukiwa hati ya pongezi kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani kimkoa.

Hati hiyo imetolewa na Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi wa kusoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, kuanzia Machi 2021 hadi Juni 2023.

Katika Mkutano huo uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha chini ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani ndugu Mwishehe Mlao, Halmashauri ya Chalinze ilionekana kuwa kinara wa ukusanyaji wa mapato ya ndani na kufikia malengo kila mwaka tangu iliyoanzishwa Halmashauri hiyo mwaka Julai 2016.

Hata hivyo Halmashauri ya Chalinze imekuwa kinara mfululizo kwa kukusanya mapato ghafi ya ndani kimkoa na kitaifa kwa kuwa kinara kwa Halmashauri za wilaya nchini kwa miaka kadhaa. Halmashauri hii ilianza kukusanya mapato ya Bilioni 3 mwaka 2016/2017, chati iliendelea kupanda mwaka hadi mwaka na kwa sasa Halmashauri ya Chalinze inakusanya zaidi ya Bilioni 15 kwa mwaka.
 

Attachments

  • FB_IMG_1700846749229.jpg
    FB_IMG_1700846749229.jpg
    52.4 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1700846751197.jpg
    FB_IMG_1700846751197.jpg
    80.1 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1700846753963.jpg
    FB_IMG_1700846753963.jpg
    73.7 KB · Views: 3
Back
Top Bottom