Hivi NEMC ina msomi mmoja tu kwamba akiamka na kukurupuka akiwaza kitu fulani ni uchafuzi wa mazingira basi wote wanaona ni sawa? Mfano ni hii approach yao ya kipuuzi ya kufungia mabaa eti yanapiga muziki kwa makelele! Mabaa yanafungiwa bila critical thinking matokeo yake amri zao zinapuuzwa na wasomi wenzao na wameanza kuyafungua. NEMC wakapambane na jukumu lao hasa la uharibifu wa mazingira. Mazingira ya ardhini, majini na anga, ukataji miti hovyo, usafi wa mazingira, madampo ya kiholela, utupaji taka za sumu, uchafuzi wa maji na hewa. Waachane na kelele za buruduni na kelele za shangwe na burudani wataonekana ni wendawazimu. Ni kama wamedandia gari kwa mbele, kupanda mtumbwi wa vimbwengo. Kelele za shangwe na ibada ni mfupa mgumu NEMC haitaweza kuutafuna