Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Cetshwayo Kampande

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
998
2,217
Kasema leo, Dar ni jiji la biashara, wasiopenda kelele waende Dodoma, watu watafute pesa, wale bia, mziki mnene. Maana wanachangia maendeleo ya jiji.

==========

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Akiongea wakati wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema “Kikubwa Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipiga kwa nguvu asiye Mkristo atasema ni kelele, miziki ya Baa ikipigwa Mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe"

 
Sema viongozi wetu bana Sheria wanapitisha wenyewe zikianza kutekelezwa wanakuja mbio mbio kuzuia. Tukichekea huu uhuni wa viongozi kugomea Sheria/ kanuni ipo siku li mtu litakatalia madarakani na hamtakua na chakulifanya.

Hata akina kagame, museveni, Mugabe n.k msifikiri waliruka tu mpaka kubadili katiba/sheria no!
Mkuu embu tueleze.

Nani anatunga sheria za nchi yetu.. na wanapatikanaje, na elimu yao ikoje? Embu anzia hapo kwanza kabla hujaendelea.
 
Alipoteuliwa tu Dar nikajua ni mkakati walioupanga kuwadhibiti NEMC
Hakuna nchi yenye sheria mbovu kama hii

Halafu mmekazana mnataka Katiba
Wanasigina iliyopo na sheria zake itakuwa hiyo mpya

Wanaapa kwa vitabu vya dini, unafiki tu
Liko wazi kaletwa kwa ajili ya kelele
 
Mkuu embu tueleze.

Nani anatunga sheria za nchi yetu.. na wanapatikanaje, na elimu yao ikoje? Embu anzia hapo kwanza kabla hujaendelea.
Mkuu kwani hujui sheria zinatungwa wapi?
Hawa wakuu wa mikoa kazi Yao ni kutekeleza na kusimamia sheria zilizotungwa (kuanzia bungeni)

Anyway tutafurahia watu tule Bata vizuri lkn haya mambo ya kuchekea viongozi wanapovunja/ kujaribu kunja shria/ kutofuata sheria, tunajiandalia bomu la nyukiria la kutuangamiza sisi wenyewe.
 
Alipoteuliwa tu Dar nikajua ni mkakati walioupanga kuwadhibiti NEMC
Hakuna nchi yenye sheria mbovu kama hii

Halafu mmekazana mnataka Katiba
Wanasigina iliyopo na sheria zake itakuwa hiyo mpya

Wanaapa kwa vitabu vya dini, unafiki tu
Liko wazi kaletwa kwa ajili ya kelele
Ndio maana Mimi nikiona watu wanalilia katiba mpya nawaona kama machizi tu. Tatizo la hii nchi sio katiba ila ni usimamizi wa hiyo katiba. wanao taka katiba mpya wangehakikisha kwanza katiba na sheria zilizopo zinafuatwa kiuhakika.

Ni mara chache sana kusikia viongozi wetu iwe wa chama tawala au upinzani wakisimama na kukemea usinginaji wa katiba/ sheria
 
Ndio maana Mimi nikiona watu wanalilia katiba mpya nawaona kama machizi tu. Tatizo la hii nchi sio katiba ila ni usimamizi wa hiyo katiba. wanao taka katiba mpya wangehakikisha kwanza katiba na sheria zilizopo zinafuatwa kiuhakika.

Ni mara chache sana kusikia viongozi wetu iwe wa chama tawala au upinzani wakisimama na kukemea usinginaji wa katiba/ sheria
Ukiona sheria zinavunjwa na viongozi wenyewe basi ujue kuna tatizo kubwa sana
Ndio maana unaona CAG anatoa ripoti wao wanacheka tu

Na hii inapelekea mpaka wananchi nao wanafanya mambo ya ajabu kabisa crimes za kutisha na maadili mabovu kama Kaliua huko wale watoto mapacha aliechunwa ngozi na kuatwa ulimi
Unafikiri ni mara yao ya kwanza?

Mwingine kaamua kumtoboa macho mke wake kisa kachepuka
Kama viongozi wanachezea nchi watakavyo unafikiri wananchi watafanya nini?

Yule mama sijui wa wilaya gani nae akakurupuka kutoka kitandani kufika mbele ya watu akatunga sheria hapo hapo eti marufuku kumuacha mwanamke

Maajabu hayaishi na hakuna wa kukemea, hivi huyo bado yuko ofisini na anasubiri watakaoachana sijui atawafungia chumbani?

Wanakera mpaka basi
 
Back
Top Bottom