Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,882
- 3,168
View: https://www.youtube.com/watch?v=4-CwMyWk3wk
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amekiri kwamba Jiji hilo ni chafu, akisema Viongozi walijisahau kwa muda katika suala la usafi.
Chalamila ameyasema hayo Septemba 17, 2026 mbele ya Waandishi wa Habari, akizungumzia hatua zinazochukuliwa kuhakikisha Jiji linakuwa safi na salama wakati mamlaka zikijiandaa kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua zinazotarajiwa katika msimu wa mwaka huu.
Chalamila amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi zinazohusika na usafi wa mazingira pamoja na Wananchi katika kuhakikisha taka hazizuii mifereji na njia za kupitisha maji Jijini.
Soma pia: Rais Samia: Dar es Salaam ni kuchafu, ni aibu