CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Akina Anna Kilango wamejaribu kuipinga ila Mungu ameisimami na imepita. Saa tuombee sehemu iliyobaki nayo iende kwa amani na kwa mapenzi ya Mungu Mwenye enzi

Mungu hashindwi jambo mkuu.Hata hapa tulipofika ni kwa uweza wake
 
Umemsahau kwenye Orodha Kamanda John Mrema Mkurugenzi wa Utafiti na Bunge wa CHADEMA hata Lissu ametambua mchango wake katika hotuba ya upinzani.

Pia Mnyika ambaye hoja yake binafsi ndio ilitaka jambo hili lianzie bungeni kwa kutungwa sheria badala ya Rais kuanza mchakato kwa kuunda tume yake mwenyewe kama Kikwete alivyotangaza awali. Mnyika ametajwa tajwa sana humu JF kuhusu masuala ya katiba ikiwemo juu ya mazungumzo na Rais.

Bila kuwasahau maprofesa Majembe Baregu na Safari na mzee wetu Arfi nao wametoa mchango mkubwa kwa kuwepo kwenye kamati maalum ya kamati kuu ya chama chetu.

Kwenye CCM anayestahili shukrani ni Kikwete pekee kwa kuepusha shinikizo la maandamano.

serayamajimbo

Nashukuru mkuu.Nisingeweza kuwataja wote.Ndio maana nimewataja wabunge wote wa CDM kwa ujumla wao.Lakini kiujumla zaidi kila kiongozi wa CDM ana sehemu yake kwa mafanikio haya.
 
walisema ooh wameenda kufunga ndoa na ccm...ooh cdm wameenda kunywa kahawa ikulu nafikiri sasa ni aibu kwao cdm ina watu makini sana......umakini huu udumu

Hakika CDM ina viongozi makini sana
 
Good analysis by fmpiganaji, viva. Sina hata kimoja cha kuongezea hapo, yote umedhungumza.
R.I.P kamanda Regia Mtema, huku mapambano yanaendelea kamanda, hakuna kulala mpaka kinaeleweka.
2015 for changes.

Asante sana mkuu.Pamoja sana
 
kazi nzuri siku zote lazima ipate sifa, big up wabunge wote wa chadema kwa msimamo wenu katika hili, pongez pia zimfikie JK kwa kuweka itikadi zake pembeni na kuwasikiliza wadau wote waliofika kwake.

Hakika kwa hili JK atakumbukwa
 
Akina Anna Kilango wamejaribu kuipinga ila Mungu ameisimami na imepita. Saa tuombee sehemu iliyobaki nayo iende kwa amani na kwa mapenzi ya Mungu Mwenye enzi
Jamani mimi niliuliza lakini sijajibiwa ivi huyu mama anaitwa ana kilanga au Ana Kilango?
 
Watanzania wenzangu! mimi nimsomaji tu humu na sijawahi kuchangia sana ila naomba na mimi kwa hili niingie kwenye historia ya wawakilishi wachache wataopata fursa ya kupongeza viongozi wetu makini waliofanikisha marekebisho haya kupita kwa ajili tu ya masilahi ya Watanzania.. Kwanza kabisa napenda kwa dhati kumshukuru na kumpongeza RAIS wetu J M Kikwete kwa ujasiri na pengine moyo wa usaliti aliouonyesha kwa chama chake na kuweka maslahi na uzalendo mbele kuridhia mawazo na mapendekezo yaliyowasilishwa kweke na CHADEMA. Ni ukomavu wa hali ya juu sana katika ulimwengu wa waliostaarabika. ni dhahiri siasa za dunia ya tatu ni tete mbovu hasa kwenye masuala ya msingi kitaifa kama hili. Ni historia Rais na utaishi na raha hiyo milelePili Nachukua fursa hii kuwapongeza CHADEMA NA WANA CHADEMA kwa kazi nzuri inayofanywa kuinua taifa letu changa linaloelekea kupotoshwa na kuyumbishwa na walafi wachache! ni hatua ya hali ya juu iliyotukuka inayokifanya CHADEMA kuimarika kila kukicha pale inapokumbatia Utaifa na uzalendo wa kweli kwa kila wazo au jambo linalofanywa. Nawapongeza sana na ninawahakikishia historia itachukua mkondo wake pale muda utakapotimia.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Asante sana mkuu.Umeguswa na mada.Pamoja tutapata katiba bora
 
jana mbowe aliongea kwa ukali sana na kutahadharisha kuwa kama mkitushinda bungeni kwa kura sisi tutaenda kwa wananchi,ikafika kipindi aliinuka na kwenda kwa mwanasheria mkuu nafikiri alipeleka wazo la kuwaweka wote wawili dc na ded baada ya kuona ccm wamekomaa na dc..kuna kipindi kilango aliwalazimisha vilaza wenzie wasimame kuunga mkono hoja na kumlazimisha speaker wapige kula ni kama aliogopa kuruhusu hilo maana anajua kwenye kura ccm watashinda halafu wananchi hawatamwelewa..hata mwanasheria mkuu hakuwa tayari kwa hili mpaka wenyewe wakazikimbia kura...........viva chadema

Hakika kwa hili pamoja na matatizo yote ya spika lakini alisoma alama za nyakati mapema.
 
umenena vema ndugu muwasilishaji, hakika chama cha ******* kimepata fundisho..
TAIFA KWANZA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
mwisho natoa laana kubwa kuliko zote kwa spika wa bunge anne makinda, mungu amlaani milele kwa kuweka jitihada za makusudi kukwamisha mambo ya msingi bungeni alaaniwe yeye na kizazi chake chooote kama kipo maana ninamashaka kama anandugu huyu mama!
Ndugu tuliza munkali, hasira haijengi!! ni kweli kuwa huyu mama anatuyumbisha sana katika harakati zetu za kujiletea uhuru lakini hata hivyo si vizuri kuchukia kiasi hicho, inabidi tumsamehe tu! na nakuomba uitengue laana yako ili awe salama, maana umemlaaani kwa kiwango kikubwa yaweza kumletea madhara!
 
kamanda naomba pia Moses Machari, Kafulila, na wabunge wengine wa NCCR waingie kwenye hiyo list kwani nao walionyesha uzalendo na kutoka nje wakati vilaza wa ccm walipolazimika kuimba mashairi waliyoandikiwa na Antiphas Lisu
 
Thread hii imenikuna big up!!! Namshukuru sana JK kwani wakati mwingine anasoma alama za nyakati. Na sasa nakubali kuwa mambo mengi anapotoshwa na malaghai wa kisiasa waliojaa CCM. JK usiogope waachie tu Chadema nchi 2015 ili tupate mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu. Na usiogope kwani tutakulinda na utaingia kwenye historia ya Tanzania kwa kuasisi mabadiliko.
 
1. Namshukuru Mungu kwa kutusaidia Watanzania hata hili likafanikiwa.
2. Nakupongeza Fmpiganaji kwa Thread yenye akili unastahili pongezi
3.Nawapongeza MAKAMANDA wote walioongoza mapambano haya wakiongozwa
na VICHWA DR. Slaa na Kamanda Mbowe.
4.Nawapongeza wabunge wa CDM kwa kuwa na akili nyingi ambazo leo watanzania
hata wale ambao waliwalaumu kwa kutoka kwenu nje Bungeni leo wanawakubali
kuwa nyinyi ni VICHWA.
5. Namshukuru Mungu kwa ajili ya watanzania wote kwa uvumilivu na maombi kwa
Tanzania yetu hatimaye Mwanga umeanza kuonekana.Bila kuwasahau wana JF wote.

"GOD BLESS OUR COUNTRY TANZANIA"
 
Hoja za msingi vs ushabiki ,kweli viva CDM chama kubwa pamoja sana. wakati umefika sasa tutoe maoni ya katiba mpya bila kuogopa maana hiyo ndio itabadili mustakabali wa nchi yetu.
 
kamanda naomba pia Moses Machari, Kafulila, na wabunge wengine wa NCCR waingie kwenye hiyo list kwani nao walionyesha uzalendo na kutoka nje wakati vilaza wa ccm walipolazimika kuimba mashairi waliyoandikiwa na Antiphas Lisu

Hakika mkuu wangu kwa ujumla wabunge wa NCCR nao wanahitaji pongezi nyingi kwa jinsi walivyoungana na CDM
 
Thread hii imenikuna big up!!! Namshukuru sana JK kwani wakati mwingine anasoma alama za nyakati. Na sasa nakubali kuwa mambo mengi anapotoshwa na malaghai wa kisiasa waliojaa CCM. JK usiogope waachie tu Chadema nchi 2015 ili tupate mabadiliko na maendeleo katika nchi yetu. Na usiogope kwani tutakulinda na utaingia kwenye historia ya Tanzania kwa kuasisi mabadiliko.

Nashukuru sana mkubwa.JK atakumbukwa sana kwa hili
 
Back
Top Bottom